Je, Mume na Mke kushirikiana kwenye ugomvi wa ndugu wa upande mmoja ni Mapenzi au ni ukosefu tu wa maadili?.

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,392
4,468
Unakuta Mume au Mke anahitilafiana na ndugu au hata Wazazi wake, lakini unakuta Mume au Mke bila kujali kama kosa ni la mwenza wake basi nae anaunga tela na kukosana na hao Wakwe/Shemeji zake.

Hivi haiwezekani Mume au Mke kuonyesha msimamo tofauti haswa kama tatizo lililopo chanzo ni huyo Mwenza wake?.
 
Mwanaume atamwacha baba na mama yake, wataungana na mkewe kuwa mwili mmoja! Sasa nyie wazazi ndugu viherehere vya nini kuwaingilia wanandoa?
 
Mapenzi upofu
Inatesa sana Mtu na Kaka yake wananuniana kisa Mke wa Mdogo Mtu kapishana kauli na Mke wa Kaka Mtu....Kila Mke kaungana na Mume wake bifu la kufa Mtu.
 
Mwanaume atamwacha baba na mama yake, wataungana na mkewe kuwa mwili mmoja! Sasa nyie wazazi ndugu viherehere vya nini kuwaingilia wanandoa?
Actually sio kuingilia, ngoja nitoe mfano...Baba na Mwanae wanabishana juu ya jambo fulani...mathalani Baba anataka Mtoto wake ajenge kwanza, lakini Mtoto anadhani muda bado atajenga huko baadae, bifu linakuwa kubwa mpaka Baba akipiga simu Jamaa hapokei.

Sasa kwa bifu kama hilo Mke nae ana haki naye kuona Mzee ndiye mkosaji?.
 
Unakuta Mume au Mke anahitilafiana na ndugu au hata Wazazi wake, lakini unakuta Mume au Mke bila kujali kama kosa ni la mwenza wake basi nae anaunga tela na kukosana na hao Wakwe/Shemeji zake.

Hivi haiwezekani Mume au Mke kuonyesha msimamo tofauti haswa kama tatizo lililopo chanzo ni huyo Mwenza wake?.
Mara nyingi mwanaume bwege ndy anakuwa wa namana hiyo,,
Kudhihirisha ubwege wake..ktk ndoa au mahusiano..
Nadra Sana kukuta mwanamke wa hivyo.
 
Back
Top Bottom