LITA2019
JF-Expert Member
- Dec 18, 2019
- 487
- 1,025
Niliajiriwa mwaka 2013 kama mwalimu wa sekondari, mnamo 2015 nliacha kazi kwa kufuata taratibu na kwenda kufanya shahada ya pili katika eneo lingine ambapo kimsingi nisingeweza kupata ruhusa kwa mwajiri mana ni kada tofauti. Nilihitimu mwaka 2016 na mpaka sasa nafanya kazi katika taasis binafsi.
Sasa nataka kuomba kazi kwenye taasisi ya serikali ambayo inafanana na sifa zangu za Shahada ya pili, je naweza kuomba na kukubaliwa mana nimesikia huwezi kuomba tena serikalini kama uliacha kazi, lakini nimesoma sifa za jumla za muombaji wa ajira serikalini, mojawapo ni awe hajastaafu/kustaafishwa, sio kujiuzulu!
Naomba ufafanunuzi kwa wazoefu

Sent using Jamii Forums mobile appMzee kwanza kabisa ulifuata taratibu zipi? taratibu ni kuomba ruhusa ya bila malipo kwa katibu mkuu kiongozi, ukiacha kazi kwa kufuata taratibu za wakurugenzi tu umeumia hautaweza tena kuajiliwa serikali za mitaa na serikali kuu sababu ulishakua na cheki namba labda mpaka kibali cha katibu mkuu kiongozi.
Ulichotakiwa kufanya ungeomba ruhusa ya bila malipo mkuu.