Je, mtoto wa kike hana mamlaka ya kufuatilia mirathi?

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
Habari za wakati huu,

Kwetu tumezaliwa 6 wakike tuu na babayetu alifariki mwaka2002 na akatuacha tukiwa wadogo na mama yetu ambaye aliugua kipindi kirefu mpk ikampelekea matatizo ya akili kidogo, baba enzi za uhai wake alikua mwalimu mkuu wa shule ya msingi

Baada ya kifo chake ndugu walianza kufuatilia mirathi bila kutushirikisha sisi wakidai kwamba watoto wa kike hawawezi kudai mirathi ni watoto wa kiume tuu

Kipindi hicho tulikua tunasoma wengine sekondari na wengine shule ya msingi dada yangu mkubwa aalivomaliza kidato cha nne alianza kudai hela hizo , mashamba na mali zingine alizoacha marehemu baba lkn walikua hawataki kuweka wazi kuhusu kinachoendeleaa,

Baada ya kuona kwamba tumekasirika ndipo walianza kurudisha baadhi ya nyaraka za kudaia mirathi na kumtaka dada yangu afuatilie yeye, baada ya kupewa alianza kufuatilia mahakamani alivofika aliambiwa kua mirathi ina migogoro kwamba mtoto wa baba mkubwa aliyekua amepewa mamlaka ya kufuatilia alienda na kuleta vurugu ndipo dada aliomba msamaha na wakamwambia aanze upya ndipo alipoanza upya kufuatilia


Alifuatilia akafikia hatua za mwisho ambapo aliambiwa atafute salary slip ya mwisho ya baba ndipo alirudi nyumbani kuitaftaa , kumbe akati amekuja kuitafta,, yule mtoto wa baba mkubwa alirudi tena mahakamanii na kuomba kuelewesha kinachoendelea alivoelekezwa kwamba dadaagu ndiye anayefuatilia mirathi kwa sasaa aliwaambia mahakamani kua yeye na familia yote hawamtambui dadayangu kwa sababu ameshaolewa hivyo yupoo kwenye ukoo mwingine sa hv akaomba atenguliwe kwenye kufuatilia mirathi hiyoo.

Alifanya hivo bila kumpa taarifa dadayangu , dada Alitafta salaryslip akaikosa ndipo Alipoamua kurudi mahakamani Kuomba msaaada mwingine , alivofika ndipo akaambiwa mirathi yenu ina migogoro kakayako kakutengua wewe ndipo alikasirika na kuamua acha afuatilie yeye

Imepita miaka mingi sasaa tulivomuuliza tena alikasirika na kusema Tusimsumbue hajui hakukaa kufuatilia tena ana mambo mengi ya kufanya

Baada ya kusema hayo tunaombeni ushauri jamani tufanye nini tupate haki ya marehemu baba yetuu ni miaka mingi sasa tumehangaika sana.
 
Marehemu alikuwa Muislam, Mkristo, au Mtu wa kawaida mwenye mchanganyiko wa dini na ukabila?
 
Back
Top Bottom