Je, Mtoto wa kambo ana haki ya kurithi mali?

Wewe andikia watoto wako then huyo wake achana nae akarithi kwa baba yake, kama baba yake hajielewi basi. Nikuulize swali dogo tu ukoo wa huyo mtoto wa nje ni ukoo wako au wa baba yake mzazi?
 
Kwanza ieleweke mali ulizomkuta nazo mumeo huna haki nazo,ila mali uliyoanza kuchuma ukiwa nae hizo 100% unayo haki nazo.
Ni utashi tu wa mwanaume kukumegea mali hata ulizomkuta nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalau wewe nakuelewa, wanawake wengi wanaonekana kuamini wanayo haki ya kurithi Mali waliyomkuta nayo mume.

Nabaki najiuliza hivi kwa mfano wanawake hao hao wangekuwa labda warithi kwenye familia ya Mengi alafu waolewe na MTU kama Mimi ambaye tayari Nina watoto 4 huko nje.

Je, watakubali kunipa Mimi nusu ya Mali niliyoikuta ambayo wao wameachiwa urithi na baba yao? Na je watoto wangu niliokuja nao, watakubali kuwapa urithi Wa hiyo Mali niliyoikuta?
 
Angalau wewe nakuelewa, wanawake wengi wanaonekana kuamini wanayo haki ya kurithi Mali waliyomkuta nayo mume. Nabaki najiuliza hivi kwa mfano wanawake hao hao wangekuwa labda warithi kwenye familia ya Mengi alafu waolewe na MTU kama Mimi ambaye tayari Nina watoto 4 huko nje, Je watakubali kunipa Mimi nusu ya Mali niliyoikuta ambayo wao wameachiwa urithi na baba yao? Na je watoto wangu niliokuja nao, watakubali kuwapa urithi Wa hiyo Mali niliyoikuta?
Wanawake ni wabinafsi sana linapokuja swala la hela/mali mkuu, hilo wala usijichoshe kuwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua ni ngumu kukubaliana na hili ila huu ndiyo ukweli,mwanzoni ilikuwa hata mali alizozipata mume akiwa na mke hapati ila sheria ikabadirika na kuonekana mchango anaoutoa mwanamke hata kukupikia,kukufulia unatosha na yeye kupata mali ila siyo kwa mali alizokukuta nazo mwanaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sehemu nimekataa mkuu, Mimi siifahamu sheria vizuri so kama ipo hivyo mimi ni nani nipinge? Sheria ifuatwe sina tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitakachouua wewe ni mkeo, mume aliyezaa naye na huyo mtoto wa kambo.

Mtoto msomeshe hujui kesho yake.

Mali hauondoki nazo, wagawie watoto wote sawa,..
Umeongea deep sana mkuu,na pole pia

Japo kwenye kusomesha mtoto kwa ajili ya wew kufaidi kesho yake(sorry kama nimeelewa tofauti and correct me if am wrong),sikubaliane na wewe sana,kama umeamua/unasomesha mtoto wako au asiye wako..fanya kama wajibu with no expectation of the kid's future

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake ni wabinafsi sana linapokuja swala la hela/mali mkuu,hilo wala usijichoshe kuwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ebu fikiria mtoa mada anaposema mke wake anataka kwenda mahakamani kisa mtoto Wa kambo kanyimwa urithi kwa Mali ambaye mama yake aliikuta, maoni ya wanawake wengi yanatetea huyo mtoto Wa kambo kupewa urithi.

Je, ingekuwa mwanaume aliyekuja na watoto wake ndio anadai huo urithi kwa Mali aliyoikuta, najiuliza hawa wanawake kweli wangetetea hao watoto Wa mwanaume wapate huo urithi.

Wanawake na haki sawa ni unafki mtupu.
 
Hivi siku hizi akili zinauzwa ghali sana kiasi kwamba wengine tunashindwa kununua? Mbona majibu yako wazi?!!! Mtoto wa kambo anamrithi MAMA YAKE MZAZI na sio baba wa kambo. Sehemu ya urithi atakayopata mama ndiyo atamgawia mwanaye huyo...
Mkuu samahani, hebu nisaidie

kama wife ana kipato kikubwa sana na mi mwanaume nkiwa na kipato kidogo hence mchango mdogo compared to wife,je wife tukitengana ntalamba hiyo 50-50 mgao kama wao wanavyolambaga au hii sheria iko kwa wanaume tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mwanamke bado unaye yani wewe mwenye mali hujafaa ameshaanza kutaka distribution ya mali mzee ukitoboa awamu ya pili ya magu wewe kidume!!hivi wanawake wanaoata wapi guts za kuanza kudai mali wakati mwenye nazo yupo hai na buheri wa afya!

N:b kuhusu kuwa huyo mwanamke kutokuwa na mchango wa mali zako lazima uwe na ushahidi kabla mjafunga ndoa ila atakula 1/3 ya kuziendeleza hizo mali juzi kuna hukumu imetoka scenario zinafana na issue yako!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilidhani mali alizokuta mke hana haki nazo, unless iwe imeandikwa. Mtoto wa kambo kisheria hana haki na mali za baba wa kufikia, unless huyo baba awe ametoa will au mama ampe mwanae mali atakazopata toka kwa mumewe.
Kuhusu mtoto wa kambo najua hana haki. Mke sijui , Kama ni hivyo sawaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anatekeleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu.
Kuhusu mtoto wa kambo subiri wanasheria wabobezi waje. Ila mtoto kufahamu baba yake mzazi ni Jambo la kheri..sema bidada kakiuka makubaliano yenu...
Hapa naona mmpeana majibu kiaina,japo hujasema kama jamaa anatoa matunzo.
Vunjeni ukimya muongee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ya ndoa ina ruhusu wanandoa kumiliki mali binafsi.kwa mfano kabla ya ndo mwanandoa alikuwa na nyumba yake hiyo haitabadilika na kuwa mali ya wote pindi watakapofunga ndoa!ila mali zilizotafutwa baada ya ndoa zitahesabika kama mali za wote!

Madeni kabla ya ndo haya takuwa madeni ya familia! Urithi mtoto wa kambo hato pata urithi kutoka kwa baba /mama wa kambo labda kwa hiyari ya mwenye mali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ongeza upendo Kwa mkeo Anza ongeza kumbembeleza. Anza kuanda kombora kimya kimya. Anza kuuza Mali moja baada ya nyingine polepole na kuwekeza kisiri Siri. Au chukulia mkopo mkubwa Mali zako zote ili ukanunue vichache ambavyo mke wako hajui.

Baada ya hapo vunja ndoa baada ya kuona Mali umeshazipoteza. Chukua watoto wako kalee yeye mwache na mwanae.

Hii itakuongezea lifespan otherwise mwanamke ambaye yupo tayari kwenda mahakamani kwasababu ya Mali zako yupo tayari akue kabisa becarefull. Mistake ukiyoifanya ni kubwa Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom