Je, Mtoto wa kambo ana haki ya kurithi mali?

David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
2,674
5,205
Habari wapendwa?

Tuna watoto 4, ila mtoto mkubwa wa kwanza sio wangu nilioa mke wangu akiwa tayari ana mtoto, watoto watatu ndio nilizaa naye. Huyu mtoto wa kufikia tangu akiwa mdogo miaka 2 nimemuhudumia kila kitu hata shule hajawahi kusoma hizi shule za kata, sasa hivi yupo kidato cha 3.

Wakati namuoa nilimpa masharti sitaki mawasiliano na baba mtoto wako, hata yeye anadai hawezi kuwasiliana naye maana aliikataa mimba. Miaka minne iliyopita niligundua anawasiliana na mzazi mwenzie ikafikia hatua kipindi nipo safari alikuwa akimpeleka mtoto kwa mzazi mwenzie nikaona haina shida maana ni damu yake, ila nikamuuliza baada ya miaka 11 leo hii mtoto amekua mkubwa ndio ameona umuhimu wake?

Alikataa mimba leo unamuona wa maana? Ndani ya miaka 2 naona amebadilika sana amefikia hatua anaanza kumwambia mtoto baba yake ndiye anayemuhudumia kila kitu, huyu mtoto ameanza kupunguza upendo kwangu ni tofauti na zamani.

Kiuchumi MUNGU amenisaidia nipo vizuri nilichofanya mali zangu zote pamoja na pesa nimewaandikishia watoto wangu wa damu, huyu wa kufikia nimeachana nae sijampa chochote licha ya kumlea kwa miaka 12. Je, kuna kosa kisheria? Maana mama yake anataka kwenda mahakamani ili na yeye mtoto wake apate sehemu ya mali.

NB: Katika mali zangu huyu mwanamke hana mchango wowote wakati namuoa kila kitu alikikuta
 
Dah! hawa viumbe hatar sana, sio sheria ya dini sio ya dunia huyo mtoto hana mamlaka ya kirithi chochote kwako labda uamue,pili mkuu nakushauri kuanzia sasa huyo mtoto mwache kumsomesha mwambie mama yake umejitoa kwa sababu ameshavunja mkataba mlopanga.

Sasa ahudumiwe na baba yake wewe umetoa msaada mkubwa sana hadi hapo sasa inatosha, halafu kuwa makini nae anaweza akaku rest in peace hujui wanaongea nini na bwana wake. Hii nje ya mada huyo jamaa anakula mzigo sorry mkuu.
 
Kosa kubwa sana amefanya mkeo hapo.

Binafsi sijaona kama mtoto huyo ana stahili kubeba madhila yalio tokana na starehe za mama yake hadi wakamzaa.

Nakushauri uanze mchakato wa kuachana na huyo mke wako, utakuja kufa kabla ya siku alizo kupangia Mungu.

Kwa mtazamo wa mwanzo, namuona mkeo akiangalia sasa namna ya kumpenyeza huyo mtoto ili awe sehemu ya uzao wako kwa 100%, kitu ambacho sio sahihi.

Na mbaya zaidi ni MKEO KUWASILIANA NA MZAZI MWENZIE, hili ni kosa la jinai.
 
Kuhusu suala la mtoto was kambo kurithi mali za baba mlezi hayo ni maamuzi yako....ukipenda unampa kidogo ila usipopenda bado pia hujafanya kosa. (,Huu no uelewa wangu, naweza kosolewa).

Ningependa kuwashauri vijana wenzangu, inapotokea mmemumimbisha mdada wa watu in vizuri mkachukua maamuzi ya kulea na sio kukimbia majukumu yenu.

Naamini matatizo mengi yanatokana na kuvunja maagizo ya dini na tamaduni zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najibu hapo mwisho kwenye mchango wa mwanamke. Mke wako ana haki na mali zako hata kama amezikuta.. mchango wake sio lazima uwe pesa..Kama anateleza majukumu ya kulea familia na kukutunza huo ni mchango tosha. Haki anayo kama hajakiuka mambo mengine ya mahusiano yenu.
Kuhusu mtoto wa kambo subiri wanasheria wabobezi waje...
Nakusifu wewe ni mwanamke mwenye hekima sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna kitu kama mtoto wa kambo. Kila mtoto ana Baba na Mama yake na ana haki ya kula urithi /jasho la hao wazazi wake. Kama kuna sheria inasema tofauti basi waliotunga hiyo sheria hawapo sawa kichwani.
Kwa issue yako huyo siyo mtoto wako. END OF STORY.
Sheria sidhani kama ipo lakini mtu anaweza mrithisha akipenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitakachouua wewe ni mkeo, mume aliyezaa naye na huyo mtoto wa kambo.

Mtoto msomeshe hujui kesho yake.

Mali hauondoki nazo, wagawie watoto wote sawa,

Mkeo naye ana haki hata kama alivikuta, si anakupikia, kukufulia, kuzaa, kukuandalia hata maji uoge, naye mgawie.

Ila, ikitokea umetangulia kufa hao wanao wako taabuni.

Hakuna mtoto mbaya kuliko mtoto wa kambo japo siyo wote.

Mtoto wa kambo wa mume wangu nilieenda kwa mguu wangu kumkomboa kwa bibi yake kule tpc na lile jua tena nikiwa mja mzito,

alichonifanyia ni aibu kusema na mwisho hapo alipofariki mr alinitafutia wahuni nusura waniuwe mie na watoto wangu siku tumetoka makaburini,

tena vita hiyo yote ni kajumba tulikojenga ujanani na mr na kagari kamoja,

Anyway, chukua comments zetu changanya na zako,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi siku hizi akili zinauzwa ghali sana kiasi kwamba wengine tunashindwa kununua? Mbona majibu yako wazi?

Mtoto wa kambo anamrithi MAMA YAKE MZAZI na sio baba wa kambo. Sehemu ya urithi atakayopata mama ndiyo atamgawia mwanaye huyo. Hauzuwii kumpa kama wosia na sio mirathi! Pili mama hana ushirika kwa vitu alivyovikuta!

Hata ulivyopata akiwepo mchango wake lazima uwe calculated! HAKUNA AUTOMATIC 50-50! Usiogope kwenda mahakamani hiyo ndio sheria. Tafuta family lawyer mzuri ulinde haki zako!
 
Pole sana mleta mada.

Ndoa hizi zina mambo sana.

Ila ninachoamini familia ni kitu chema, ni kitu tunakipambania kwa roho na mwili na kwasababu ni jambo la 'Ki-ungu' familia inapokua vyema hudhihirisha ukuu wa Mungu na ufalme wake.

Shetani hawezi akarelax aache tu familia ziwe salama. Atatafuta namna ya kuvuruga, na hapa kama ilivyokuwa tangu mwanzo, wake zetu ( japo huwa si mara zote ) huwa lango rahisi, chokochoko hupitishwa kwao. Wangu mimi huu ni ukweli mchungu. Tunajua kuwa tutajaribiwa katika hili.

Nikirudi katika kisa chako japo hatujasikia upande wa pili lakini nadhani mkeo amekua lango, shetani kashapenya na anagusa panapouma zaidi. Anajua hapo kuchomoka sio rahisi.
Ushauri wangu brother tulia, tena tulia hasa.

Mtoto kumjua baba yake si kosa, kosa ni kutokukushirikisha, na vile wewe umeshiriki kumlea ni mwanao pia.

Zungumzeni hili jambo litaisha tu - ipo namna. Mungu yupo atafanya wepesi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom