Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .

Dotori

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
544
24
Wadau,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala inayoendelea katika forum hii. Nataka kutoa changamoto kwa wadau wenzangu ili tujadili swali lifuatalo:


Je, ni mtanzania gani ana SIFA na VIGEZO vya kuiongoza Tanzania? Wachangiaji wanaweza kupendekeza majina MATATU.


Itakuwa vyema kama wachangiaji watatoa sababu zinazowafanya watoe mapendekezo hayo?


Nawasilisha hoja:

UPDATE:

Majina Matatu (makubwa) Yaliyopendekezwa:

  1. Jakaya Kikwete - CCM
  2. Willibrod Slaa - CHADEMA
  3. Ibrahim Lipumba - CUF
 
Madela Wa Madilu.

Mwadilifu, siyo Fisadi.
Ni haki yangu ya kikatiba
Nina agenda kabambe juu ya kubadili mwelekeo wa kiuchumi.
Kipaumbele Umeme, Maji, Viwanda,barbara,Kilimo

Naahidi kuwabana Mafisadi wote.
 
Unataka majina au sifa? Kama ni sifa, turejee makala ya Ulimwengu na Hotuba ya Mwalimu Nyerere ya 1995 pale Mbeya. Kama ni majina, hapo tena ni kasheshe!
 
Bw.Dotori pamoja na Wadau wote naomba nianze kwa Kuomba Samahani,na Msamaha huu ni kuwa ntatoka nje ya Mada hii Kidogo.

Tumekuwa hadi hii Leo na Viongozi(Watawala) tulowachagua ktk Awamu nne tofauti(Zingatia Kung'atuka kwa Mwalimu)ndani ya misingi 'safi kabisa ya Kidemokrasia',na dhamira Kuu ya Watanzania wote kwa kuwachagua Watawala hawa ni ili basi watujengee Mazingira na Misingi bora Tujikwamue katika Dimbwi la Umasikini wa: Hali, Kiakili, Mali.

Tofauti yake ni kwamba:

Dimbwi hili la Umasikini limekuwa likiongezeka KINA kila Awamu,na watanzania walio Vijijini na hata Mijini, wazidi Kuzama kwasababu ya Afya Duni,Ujinga na Ulofa ulokidhiri,matokeo yake
Watanzania tunaishi Kimiujizaujiza tu,hakuna mipangilio,bora Liende!kwa mfano:Upo ndani ya daladala, kwa wale tunaoishi kati ya maeneo ya Magomeni(Mapp) na Fire, kila siku ya Mungu Unaona Kundi la watu,hawana vikapu mikononi,mabegi,au hata Ndoo za maji basi, likiwa kwa miguu linakatiza maeneo ya jangwani linaelekea katikati ya Jiji,watu wanajikusanya na kukaa katika vikundi ili kupiga Gumzo tu(Vijiweni)kwa kweli Nnajiuliza Maswali mengi sana pasipo majibu!!

Kuna usemi kuwa Muda kamwe Hauongopi!
Labda ni Uzee Unaingia au napatwa Na Wendawazimu sijui!,lakini yapata Miaka 40 hivi, kwa kweli sijaona Umuhimu/Sababu ya KUWA NA RAIS NCHINI TANZANIA.Nnaelekea kufikiri basi hata tukaweka PAKA MWITU pale Ikulu,bado hilo li-Nchi litakwenda tu!!
 
Raia Wa Tanzania, mwenye miaka zaidi ya 35, ana akili timamu, hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu, na anayependekezwa na chama cha siasa.
 
^^ hizo ni requirements ambazo mtu anatakiwa ameet wakati wa uchaguzi, lakini kama ni hivyo, basi na mie nafaa kuwa rais wenu wazee, nianzishieni mipango ya kuwa rais !
 
sasa kama unakula kiazi kimoja, kuna ubaya gani nikikuongezea kimoja kingine ama viwili ? si ndio developmenti hiyo ! au wee unataka ubweche mkononi ?
 
nionavyo mimi, Rais as an individual pekee haitoshi kumfanya mtu afae, nionanvyo mimi. Tunahitaji powerful, effective governing structures kama bunge ambazo zinaweza kumfanya hata rais wa kawaida sana aendeshe nchi kwa namna inavyotakiwa...wabunge wasio watumishi wa serikali, wanaoweza kumdindishia rais na kumwambia kama atafanya hicho au kile, wanaweza kummwaga kwa kura za kutokuwa na imani naye...

Kama mtu atakayefaa atakuwa mzuri kwa namna yeyote, njia yake ya kwenda ikulu itajaa vigingi, kwa kuwa wapinzani wake watamwaga "vipeperushwa" ili kumdhibiti, maana ataharibu mirija yao. Namna mojawapo ya kuondoa hilo, ni kuwa na powerful structures zinazoweza ku demand hali hii, mathalan, kwa kutumia hata upigaji kura kwa kufikia maamuzi fulani.

Vyombo kama bunge vitaweza kuwa powerful kama wabunge wenyewe watakuwa rushwa-free...na hatimaye wanakuwa na uthabiti wa kudai hata taasisi ya kupambana na rushwa iwe chini yao...kumbuka, wao ndo law makers. Nchi nyingine, maamuzi mazito hutegemea sana bunge, na si individual character peke yake.

Rais akifaa sana bila supporting system, ni kazi bure. supporting system ndiyo inayomfanya rais afae, na akishindwa anatolewa. Maana rais anaogoza nchi kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.
 
Madilu, powerful and effective structures kama bunge, na mahakama ndiyo zinafanya kiongozi aongoze nchi nchi kwa mujibu wa sheria. Kama rais akiwa mzuri na akaongeza nguvu kwa utendaji wa structure hizi, basi huyo anafaa zaidi. lakini kiongozi mzuri kwa mfumo wetu hapa, hawezi kufanikiwa kwa kuwa supporting systems kama bunge ni very weak...wawakilishi wa wananchi ndiyo watendaji wa serikali...na mfumo waliojitumbukiza una kansa ya rushwa...kila mtu anafanya kuharibu kivyake...
 
Ukiangalia kila kiongozi Tanzania ni FISADI.Na kila siku humu watu tunakaa na kujadili na kulalamika sana kuhus viongozi wetu hawa.

Swali ni je tumekaa na kufikiria ni nani atafaa kuingoza Tanzania kunako 2010?.Maana hiyo 2010 siyo mbali atii, hivi sasa tupo tunaingia april 2009 inamaana sasa hivi ni wakati muafaka wa kuandaa wagombea wa kiti cha uraisi 2010 (iwe CCM or Chadema,CUF etc).

Mimi nadhani ni wakati muafaka akijitokeza mwanamke hii 2010 kugombea hicho kiti cha raisi, it doesnt matter anatokea chama gani.Wako smart women kwenye Tanzanian politics wengi tuu ambao wana qualify.Mfano akina Anna Makinda (very smart and strong woman) na wala siyo FISADI.

Ukiangalia kwenye uchaguzi wa marekani watu wengi walikuwa hawaamini kabisa marekani ingeweza kuongozwa na mwanamke.Look at Hilary alikuwa kidogo tuu achukue uraisi,she never back down no matter what ali-stand up strong.I believe kuna wamawake Tanzania wako strong and smart kama Hilary Clinton.
 
Oh yeah...Hillary...damn I wish she was the president..Madame President Hilary Clinton....
 
Hey Kelly pole na mitihani dadangu anyway,
Uwezo bila kujali chama ama jinsia.Kwanza uwezo wa yule mgombea mwenyewe si kuchagua tu kwa kuwa ni CCM ama Mwanamke ama handsome or Beautiful au ana pesa.hii ndio inayowachanganya wengi katika nyakati za uchaguzi.wagombea huchukua advantage pale anapoona pana mapungufu.wengi hutumia uke wake ama chama ama amani kwa CCM kule kwetu.Wapiga kura wanatakiwa kuelimishwa ili wafaidi matunda ya kura zao na si kuzijutia. Think Twice.


SAHIBA.
 
Ukiangalia kila kiongozi Tanzania ni FISADI.Na kila siku humu watu tunakaa na kujadili na kulalamika sana kuhus viongozi wetu hawa.

Swali ni je tumekaa na kufikiria ni nani atafaa kuingoza Tanzania kunako 2010?.Maana hiyo 2010 siyo mbali atii, hivi sasa tupo tunaingia april 2009 inamaana sasa hivi ni wakati muafaka wa kuandaa wagombea wa kiti cha uraisi 2010 (iwe CCM or Chadema,CUF etc).

Mimi nadhani ni wakati muafaka akijitokeza mwanamke hii 2010 kugombea hicho kiti cha raisi, it doesnt matter anatokea chama gani.Wako smart women kwenye Tanzanian politics wengi tuu ambao wana qualify.Mfano akina Anna Makinda (very smart and strong woman) na wala siyo FISADI.

Ukiangalia kwenye uchaguzi wa marekani watu wengi walikuwa hawaamini kabisa marekani ingeweza kuongozwa na mwanamke.Look at Hilary alikuwa kidogo tuu achukue uraisi,she never back down no matter what ali-stand up strong.I believe kuna wamawake Tanzania wako strong and smart kama Hilary Clinton.

Mi bado sijaona mwanamke wa kuwa president Tanzania (mtanisamehe). na huyo Clinton naye, ALMOST IS EQUAL TO NOTHING (politics ni none or all principle mama).
Mi nitafurahi ukiingia mfumo wa wagombea binafsi, kwani mambo ya kuingia kwa chama yanaweza yakawa yanatuzuia kupata kiongozi bora.
Kwa hayo machache- 2010 bado ni ya CCM, most likely Kikwete.
 
Mi bado sijaona mwanamke wa kuwa president Tanzania (mtanisamehe). na huyo Clinton naye, ALMOST IS EQUAL TO NOTHING (politics ni none or all principle mama).
Mi nitafurahi ukiingia mfumo wa wagombea binafsi, kwani mambo ya kuingia kwa chama yanaweza yakawa yanatuzuia kupata kiongozi bora.
Kwa hayo machache- 2010 bado ni ya CCM, most likely Kikwete.

Swadakta mwanangu, hapo umesema.
 
Kelly,

I think you are loosing track of gender politics of US and TZ, as their realities are far fetched. The value of choosing a Tanzania president can not be based on gender or smartness, rather is informed with social and basic needs. This is not about the women's issues; it is about reshaping the consciousness of the state and its people. If there is a woman president to do that, why not! I think, I need a president with vision, guts, and motivation; to make Tanzania believe once again we can get hold of ourselves.
 
Kelly,
... I need a president with vision, guts, and motivation; to make Tanzania believe once again we can get hold of ourselves.


Mimi Nilidhani Kelly thread yako unge edit kichwa that is ki read
Sasa ni mwanamke gani Anafaa 2010?
kwani details zimebase kwenye gender.
Otherwise according to Petu Hapa, mimi ninaona watu wachache tu wenye guts kama Magufuli. Vinginevyo apewe one of the JF members kama Invisible, Mzee mwanakijiji etc...then watakuwa in a position to chose some others members ambao hawana chembe ya ufisdi toka hapa JF then wawe ministers. Achana na manyama CCM.
 
Back
Top Bottom