Je, msioamini uwepo wa Mungu, mnaamini uwepo wa Shetani?

Na vipi kuhusu kutumiwa majini au kulogwa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya Majini na Kulogwa nayo siamini,Majini na Kulogwa ni matatizo ya kisaikolojia na issue ya "sintofahamu"

Matatizo ya Kisaikolojia
Kabla ya watu kuanza kufanya utafiti wa mambo ya kisaikolojia,matukio ya Majini yalikuwa mengi sana,Makanisa kama Roma Catholic walikuwa wanaombea watu na kufanya mission za exorcism,miaka 1920s uelewa wa saikolojia ukiwa umeongezeka watu kama Sigmund Freud waliweza kuelezea issue ya Majini ni matatizo ya kiakili tu na yanawagusa wanawake zaidi kuliko wanaume,na matibabu yake yapo na watu wengi wameshatibiwa na kupona.

Conversion disorder - Wikipedia

Exorcism - Wikipedia

Issue ya sintofahamu na Kulogwa,hakuna mtu anayesema nina malaria au Ukimwi so nimelogwa,watu wanakimbilia magonjwa makubwa na ambayo hatatibiki au matatizo makubwa ambayo hayatatuliki kiurahisi na kusema ni uchawi kwasababu inasaidia kutoa sababu rahisi kwanini matatizo fulani yamekupa.

Btw tukishapata ufumbuzi wa hayo matatizo,tunaacha kusema uchawi na tunatafata tiba inayotakiwa.
Wakati wa biblia ukoma ulikuwa ugonjwa wa laana lakini leo hii inajulikana ni maambukizi ya kibacteria ambayo yanahitaji dawa na hakuna mtu anayehangaika na maombi

Binadamu ni kiumbe ambaye ana uwezo wa kutafuta pattern,mtu akiangalia mwezi anaona mama na Mtoto,akiangalia michirizi ya maji kwenye ukuta anaona sura ya mtu,kwenye Toast za mkate watu wanaona sura ya Yesu.
So kurogwa ni jibu rahisi kwa maswali magumu

Sorry kwa Majibu marefu........

Sent from my LG-H990 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom