Je, msamaha wa Rais Magufuli kwa DED wa Kahama umewaponya Wakurugenzi wote walionunua magari ya Tsh 460 milioni?

Tamko la rais lime-specify anayesamehewa na sifa za mwenye kusamehewa zikatolewa hadharani kwamba ni mchapakazi, mbunifu, anatumia mapato ya ndani ya halmashauri vizuri, anavutia wawekezaji kwa kutoa ardhi bure na zaidi anapigwa majungu tu na baadhi ya viongozi. Kwa sifa hizo hadi akaagiza gari V8 ya milioni 400+ arudishiwe.

Je hao wakurugenzi wa halmashauri za Geita, Chato wana sifa hizo.
Wanasifa kama zake na tabia
 
Wanasemaga "bahati ya mwenzio isikufanye ulale mpango wazi..." Huo sio msamaha wa jumla, usitake kuanza kujifariji! Magu alikuwa 'very specific' wa kahama!
 
Rais Magufuli amesema haya

''Mkurugenzi wa Kahama Mji unafanya kazi kubwa sana, ka kosa kale kadogo kamesamehe dhambi zako zote. Unafanya kazi sana najua unapigwa vita ila wanaokupiga vita kuanzia sasa wakuogope.

Nimemsamehe Mkurugenzi huyu, amefanya makubwa! Mkurugenzi hongera Sana. Na hilo gari nitamrudishia aendelee kuliendesha lakini asirudie kununua gari nje ya utaratibu".


--
Nauliza tu iwapo uchapa kazi wa mkurugenzi wa Kahama na madiwani wake umewaponya pia Wakurugenzi wa Geita, Temeke na wengine waliorudisha magari ya bei ghali kwa waziri mkuu.

Wajuzi wa itifaki za misamaha tafadhali.

Pia soma > Kahama: Mkurugenzi anunua gari la gharama kubwa

Maendeleo hayana vyama!
Ukweli ni kwamba hakuwa na makosa maana mchakato ulifuatwa alikuwa katolewa kafara kwa mileage za kisiasa na aliyezianzisha ndye huyo aliyemrudisha.

Kuna wengine wanasamehewa na wengine wanatumbuliwa.
 
Ukweli ni kwamba hakuwa na makosa maana mchakato ulifuatwa alikuwa katolewa kafara kwa mileage za kisiasa na aliyezianzisha ndye huyo aliyemrudisha.

Kuna wengine wanasamehewa na wengine wanatumbuliwa.
Aliyeanzisha mambo ya V8 ni mbunge Musukuma wa Geita vijijini
 
Aliyeanzisha mambo ya V8 ni mbunge Musukuma wa Geita vijijini
Aliyemwambia waziri achukue hatua ni nani? Kwani mambo managapi uwa yanasemwa anafumbia macho na kuziba masikio? Lakini hili ametembea nalo na mwisho kamrudisha.
Ila ukweli huyo mkurugenzi hakuwa na kosa kama waliona gari halifai basi wasingempa kibali.
Wanasiasa bwana wanajua kucheza na akili za wadanganyika.
 
Wakati anaagiza aondolewe alifoka sana kuonesha ulifanyika ubadhilifu mkubwa sana!

Wakati anamrudishia hilo gari ameonesha ni kakosa kadogo sana,

INATEGEMEA KAAMKAJE
 
Back
Top Bottom