Je Mrithi wa Regia ilikuwa lazima atoke kasikazini??

Kuna watu ninapata shida kujua uwezo wao wa kujenga hoja! Haya bana nawahi bar
 
Is an option lakini kama ni hivyo kwani kuna uharaka gani??kwakuwa sheria sawa na za mbunge wa kuchaguliwa!!mbona wakuchaguliwa inachukua hata miezi??sasa kwa mbunge wa viti maalumu wiki??hapana hata ndugu wamarehemu tukienda kwenye arobaini watatunyoshea vidole!!kwa hili sitaacha kusema!
Nakuunga mkono KK. CDM iajipaka matope chenyewe badala ya kusubiri kipakwe matope na opponents. Walichofanya siyo rahisi kueleweka
 
Aziza Masoud na Ellen Manyangu

WIKI moja tangu kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Regia Mtema kilipotokea, mchakato wa kumtafuta mrithi wa nafasi yake umeanza.

Regia alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuzikwa Jumatano wiki hii nyumbani kwao Ifakara, mkoani Morogoro.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zinasema tayari maofisa husika ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameanza kushughulikia suala hilo la kuziba nafasi ya mbunge huyo kijana ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alisema jana kwamba ofisi yake itatumia orodha ya majina yaliyopendekezwa na Chadema mwishoni mwa mwaka juzi.

“Nadhani tunayo orodha ya mapendekezo ya Chadema, basi kwa jinsi taratibu zilivyo, tutarejea katika orodha hiyo na pale tulipopitisha msitari ndipo tutakapoanzia, lakini lazima huyo anayefuata katika orodha awe na sifa za kuwa mbunge,” alisema Mallaba kupitia simu yake ya kiganjani.

Hata hivyo, Mallaba alisema hivi sasa ni mapema mno kufahamu ni lini uteuzi huo utafanyika na kwamba taratibu za ndani zikikamilika, mamlaka husika zitaarifiwa ili umma pia uweze kufahamu.

Awali, Mallaba alikataa kuonana na waandishi wa habari na mmoja wa maofisa wa Tume hiyo alisema: “Amesema majina yametoka hukohuko Chadema ndipo yakaja huku kwa hiyo kama mnayahitaji mnapaswa kwenda katika ofisi za Chadema ili muweze kupata majina hayo.”

Dk Slaa, Zitto wanena
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema chama chake hakifahamu atakayechukua nafasi hiyo na kwamba hiyo inatokana na ukweli kwamba jukumu hilo liko mikononi mwa NEC.

“Majina ya wagombea wa viti maalumu yapo NEC na wao ndiyo wanaoangalia kuchagua nani anayefuata katika orodha iliyopo Tume, kwa utaratibu, mgombea anayefuata ndiye atakayechukua nafasi hiyo,” alisema Dk Slaa.

Alisema Chadema kilipeleka NEC orodha ya majina 28 ya wabunge wa viti maalumu, Desemba 30, 2010 na kati ya hayo majina 25 tayari wameshachaguliwa ni jukumu la NEC kuangalia jina gani linalofuata kwenye orodha hiyo iliyopo.

Alisema kati ya hayo majina matatu yaliyobaki yeyote atakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi hiyo kulingana na vigezo vya NEC na kulingana na utaratibu na Katiba ya Chadema.

“Sina mamlaka ya kujua nani anayefuata na ofisini kwangu hata majina sina majina yapo NEC mimi nawategemea wao waniletee jina kwa mujibu wa taratibu zao nitaliangalia kama muhusika bado ni mwanachama hai nitawajibu na nitawarudishia na ndiyo watalitangaza kwa wananchi,” alisema Dk Slaa.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, jina watakalopewa kama muhusika atakuwa amefukuzwa katika chama, basi jina litakalofuata baada ya huyo mwanachama ndilo litakaloandikwa na kufanyiwa kazi.

Alisema si rahisi kwa NEC kumtangaza mrithi wa nafasi hiyo bila kuwasiliana kwanza na chama na kuthibitisha kuwa bado ana sifa za kushika nafasi hiyo.

Alisema NEC inajua wazi kuwa haiwezi kumtangaza mtu moja kwa moja pasipo baraka za chama kwa sababu siku hizi kumekuwa na wimbi la migogoro ndani ya vyama vya siasa nchini na wengine kujivua uanachama au kufukuzwa.

Wakati Dk Slaa akisema jukumu hilo ni la NEC, Naibu Katibu wake, Zitto Kabwe alitaja jina la mmoja wa madiwani wa viti maalumu wa chama hicho kuwa ndiye anayefuata katika orodha iliyopelekwa NEC.

Akizungumza jana, Zito alisema kwa mujibu wa orodha yao ya viti maalumu anayefuata baada ya wabunge walioteuliwa mwaka juzi ni diwani huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.

“Kwa mujibu wa orodha tuliyonayo ya wabunge wa viti maalumu anayefuata baada ya Regia ni diwani kutoka (anataja wilaya na jina lake), ndiye atakayechukua nafasi ya kiti hicho kilichoachwa na marehemu,” alisema Zitto.

 
Ni ujinga kutetea kitu ambacho unajua kabisa kinakumaliza na unaendelea kukifanya...hii harufu ya ukaskazini ipo ata kama tunakipenda vipi chadema,cha muhimu ni kuona namna ya kuiondoa machoni mwa watu.
 
mtu unapoleta hoja hapa ufanye utafiti kwanza ndio uposti, mtoa hoja alitakiwa kuchunguza utaratibu wa kupatikana wabunge wa vitu maalumu kwa upande wa CDM na NEC aone kama kuna kasoro ndio aposti au aombe msaada hapa namna wanavopatikana au kuziba nafasi zao sio kukurupuka kama mtu alieenda haja kubwa ili mradi umeposti
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!

Mkuu mrithi kutoka kaskazini ni kawaida tu kwani CDM ni chama cha Kanda hiyo: wamesahau nn mpaka waende ZnZ, Mtwara, Songea. Katiba mpya inabidi ivi BAN vyama vyote ambavyo vinaexist kikanda huku kanda zingine havipo kabisa
 
Ni ujinga kutetea kitu ambacho unajua kabisa kinakumaliza na unaendelea kukifanya...hii harufu ya ukaskazini ipo ata kama tunakipenda vipi chadema,cha muhimu ni kuona namna ya kuiondoa machoni mwa watu.
unajua namna wabunge wa viti maaalum wanavopatikana kiseria au unaharisha tu?? hii dhambi ya kutenga watu wa kasakazini itawatafuna muda si mrefu. pia haijalishi mtu katoka wapi jadili uwezo wake na jadili njia iliyotuma kumpata sio umjadili kwa kuwa anatoka kaskazini, kwani kaskazini sio Tanzania?? kaskazini lazima tuwapongeze na kuwaiga ndio chachu ya mageuzi na sasa tuisambaze nchini kote na sio kuwatenga na kuwabagua kwa ukanda
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!

ushindwe kwa kuleta majungu humu.kaanzishe chama chako ili ukiendeshe bila utaratibu kama kichwa chako kinavyokutuma
 

Nilichokisikia ni kwamba uteuza utafuata orodha iliyoko tume ya taifa ya uchaguzi na siyo kuitisha uchaguzi mpya,kama kwenye orodha hiyo baada ya mtu wa mwisho ni huyo wa karatu tatizo nini?
Siyo ulichosikia, huo ndio utaratibu ulivyo na haujaanza leo, kumbuka hata Geturde Lwakatare aliingia bungeni baada yakifo cha Salome Mbatia, na yeye katika ile orodha jina lake ndio lilikuwa linafuatia.
Kumbe huyu Kakakiiza ni sehemu ya vilaza hapa JF? mbona hakuwahi kuhoji kwa nini mkoa wa Morogoro uwe na wabunge wa viti maalum wawili Regia Mtema na Suzan Kiwanga wakati mkoa wa Lindi hauna hata mbunge mmoja wa viti maalum!!?? huku ni kufikiri kwa kutumia kijambio.
 
Is an option lakini kama ni hivyo kwani kuna uharaka gani??kwakuwa sheria sawa na za mbunge wa kuchaguliwa!!mbona wakuchaguliwa inachukua hata miezi??sasa kwa mbunge wa viti maalumu wiki??hapana hata ndugu wamarehemu tukienda kwenye arobaini watatunyoshea vidole!!kwa hili sitaacha kusema!

Mapenzi ya CDM yanawatia wengi upofu; wengi wenu mnaishia kujitoa ufahamu
 
Ni ujinga kutetea kitu ambacho unajua kabisa kinakumaliza na unaendelea kukifanya...hii harufu ya ukaskazini ipo ata kama tunakipenda vipi chadema,cha muhimu ni kuona namna ya kuiondoa machoni mwa watu.

ujinga wa kufikiri kaka
 
Dr. Slaa anatoka Karatu, nyie watu wa Mtwara, Ruvuma, Pemba CDM haiwahusu nendeni CUF na CCM

karatu? Duu. Hiv mtwara, lindi, pemba, unguja, nk kuna wawakilishi wowote wa viti maalum. Mi binafsi sio haja ya kuwa na wabunge 2 moja wakati kuna sehemu nyingi hakuna hata mbunge. Kama cdm wanataka kujitanua na wanadhamira ya kweli! Sisem mingi nicje nikashambuliwa.
 
Nimesikia mrithi wa Hayati Regia amepatikana kutoka Karatu! Je ilikuwa lazima wapitie kwenye kumbukumbu za chaguzi zilizopita?? Kwa nini hawakufanya uchaguzi mwingine ili kuleta uhalisia wa usawa kwenye chama na kuondoa dhana kuwa ni chama cha kanda ya Kaskazini??

Na ninafikiri ilikuwa vyema wangeenda Zanzibar,Mtwara,Songea,nafikiri wangepata watu wakuwakilisha viti maalumu na kuziba nafasi iliyoachwa na Regia! Hapakuwepo na uharaka kiasi hiki!

Kwani hata wiki haijaisha tangu marehemu azikwe mimi hapo nimeona kwajicho latatu nimeona kulikuwepo na upungufu!! Kwani Jambo hili limepelekwa haraka sana!

Toa mapendekezo ya watu active wanaotoka mikoa hiyo
 
hapa CHADEMA ilitakiwa kutumia mwanya wa kujijenga katika mikoa mingine ambayo haina wabunge kama ya kusini na singida, zanzibari na Pemba. hapo ungepanda mbegu nzuri sana na mavuno mengi ungeyavuna. inaonesha kwa jinsi gani ubunge unavyotafutwa kinguvu, . Maiti hata hajafikisha arobaini, watu washepiga kampeni ya kuomba nafasi hiyo! Chadema acha uregionalism!

Jamani humu ndani, I mean JF huwa naamini kuwa watu wengi ni waelewa au ni wasomi au hata ni wadadisi wa mambo kidogo. Lakini kuna wakati nashindwa kuamini na hata kuwaelewa baadhi yetu humu lengo na nia la baadhi ya posts ni kitu gani. Hili swala la mbunge wa viti maalumu chama chochote cha siasa kikisha wakilisha orodha ya majina ya watu (hapa niseme wanawake) wanao-qualify kwa vigezo vya chama husika kuwa au kuteuliwa na tume kuwa wabunge wa viti maalumu chama husika hakina tena influence yoyote juu ya jambo hilo bali ni tume ya uchaguzi ndo hutoa orodha ya wabunge wateule kulingana na mgao kwa vyama husika. Ikitokea mbunge wa vitu maalum (hasa wa kundi hilo la wanawake) amefariki tume hutangaza jina la mtu aliyekuwa anafutia katika orodha hiyo bila kujali mtu huyo ametokea upande gani wa nchi. Hii ilishatokea hivi karibuni kwa Salome Mbatia alipofariki kwa ajali ya gari, mtua aliyekuwa anafutia katika orodha ya CCM iliyopelekwa NEC alikuwa ni Getrude Lwakatare (Mchungaji kiongozi, Dr.). Tume wanaangalia aliyefuatia kwenye orodha, na sio vinginevyo, labda anayefuata awe amepoteza sifa kama kufariki, kufukuzwa uanachama au kukoma kuwa mwanachama wa chama husika, n.k. Kwa hiyo chama kama CDM kwa sasa hakina influence yoyote katika jambo hilo. Kama na mimi sijui utaratibu nielimishwe kwa upole na upendo wa kindugu manake JF ndo lengo lake.

Nawasilisha.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Kweli mapenzi upofu; ukipenda ..hata pengo utasema mwanya. WAKE UP WEWE

nimeipenda hii! Sema natumia cmu, ningekugongea "LIKE" Kupenda kwingine duu ni hatar. Kosoa palipo na kosa, na sifia panapostahili kusifia.
 
Mbona Wabunge Wote wa Viti Vya ofa kwa CCM Wanakaa Dar es Salaam na Hatusemi!! Kwani Dar Ni Kanda Gani?
 
Ninachojua mimi hapa JF tunajiita Great Thinkers lakini wengi wetu sio wafuatiliaji wa mambo mazito. Tunajadili vitu vidogovidogo kama ukanda, udini na ukabila. Kabla ya kuleta post hapa ilipaswa mtoa hoja ajiridhishe na sheria ya Uchaguzi inavyosema. Aidha alipaswa kujiuliza kama kama anao uelewa wa kutosha kuhusu Katiba ya Chadema na nafasi ya huyo anayetoka kaskazini katika orodha ya iliyopelekwa NEC na Chadema. Tumeelezwa hapa mara nyingi kwamba kabla ya Uchaguzi kila Chama hupeleka NEC orodha ya wanachama wake watakao kuwa wabunge wa viti maalum. Kinachofanyika baada ya Uchaguzi Mkuu ni kila chama kupewa orodha ya majina kulingana na idadi ya nafasi zilizopo kutokana na kura za Urais na za Majimbo. Kwa upande wa Chadema kilipewa viti maalum 23 kabla ya uchaguzi wa Mpanda Mjini ambapo baada ya kushinda Jimbo la Mpanda wakaongezewa viti viwili ambavyo vilienda kwa Sabrina Sungura (Kigoma), Na Rebecca Mngodo (Arusha) waliokuwa wameshika nafasi ya 25 na 26. Aliyefuata kwenye orodha hiyo ni Cecilia Pareso na Subira Waziri (sijui wanatoka Mikoa gani) na baadae Leticia Masore (Mara) ambaye alijiunga na NCCR Manunuzi baadaye mwaka 2010.
 
Huyu alienzisha hii thread nina hakika atakuwa ni miongoni mwa wale wanafunzi wa kiislamu ambao hawataki ufanyike uchaguzi kuchaguwa viongozi wa wanafunzi bali vyeo vigawanywe nusu kwa nusu kwa wakristo na waislamu. akili matope kabisa hizi.
Hivi kuna mkoa gani uliozuiwa kuweka wagombea katika uchaguzi mkuu uliopita? na ni nani anaedhani ubunge ni zawadi ya kuzawadiana kama tupo kwenye Harusi. mijitu humu ni mipumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom