Je, Mpango Kazi na Bajeti ya 2021/2022 itafumuliwa tokana na ujio wa awamu ya sita?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Inadaiwa mojawapo ya jambo kubwa lililokuwa linapita bila hata kujadiliwa katika bajeti hii na hata Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi walishajulishwa na wakanyamaza kimya ni kutokuwa na nyongeza ya mishahara. Vyama vya wafanyakazi kwa kupitia TUCTA walishakuwa kimya kama wamenyeshewa mvua kwa kuacha tu awamu ya tano ifanye ifanyavyo na mpaka ingeamua yenyewe ni lini ingepandisha mishahara.

Mabaraza ya Wafanyakazi ambayo huhusisha Waajiri, wafanyazi na vyama vyao yalishakaa kwa nchi nzima, wizara hadi Taasisi na kupitisha mpango kazi na bajeti zao ambazo hazikuwa hata na nyongeza za mishahara hata kiduchu tu na kwenye vikao woga ulikuwa ni mwingi mno mno kuhoji. Wapangaji Bajeti wanadai walipewa ukomo wa bajeti hizo toka Wizara ya Fedha - kwa Doto James, yaani yule kaka yake na Heri James wa UVCCM, na hakuna mtu aliyekuwa akidiriki kuhoji kuhusu nyongeza. Hata Mei Mosi ilitarajiwa kuja ikiwa imepooza sana sana. Pengine awamu hii inaweza ikaichangamsha!

Sasa je kwa ujio wa awamu hii ya sita - tutaendelea na dude hilo hilo la awamu ya tano. Waziri wa Utumishi Mohamed Mchengerewa umeongea kwa maana kubwa sana baada ya kuapishwa - je huoni kwa kutumia taaluma yako ya sharia na kwa nafasi yako sasa una haja ya kuifanya serikali ifikiri na hilo isiwe mambo ya kupandishana vyeo tu ndiyo yanastahili nyongeza. Tafadhali tamka kitu angalau hiyo bajeti ipanguliwe na nyongeza hata 0.5% ikiwekwa itasaidia sana hawa wafanyakazi angalau waweze hata kukopa benki.
 
Back
Top Bottom