Je, modem ya tigo inatofauti na zile za airtel na voda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, modem ya tigo inatofauti na zile za airtel na voda?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Soki, Mar 21, 2011.

 1. S

  Soki JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Je, nikinunua modem ya Tigo inayouzwa TSh. 30,000 nitaweza kui-unlock na halafu ikafanya kwa line zingine kama modem za voda na airtel BILA KUPUNGUZA SPEED? Kama jibu ni ndiyo nitawaza kununua modem ya tigo kwa Tsh 30,000 badala ya ile ya voda ya Tsh. 49,000. NAOMBA USHAURI WATAALAM
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  nunua ya voda ndio inatoa speed nzuri kwa Aitel line (baada ya kuichakachua)
   
 3. S

  Soki JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ok ok umenipa jibu la swali langu. Ina maana siyo swala la modem tu ilimradi! Nimeghairi sijui kama nitanunua! Vipi modem ya AIRTEL NA VODA yenye speed nzuri ni ipi?
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  modem ya voda inatoa speed nzuri, lakiti mtandao wa voda hauyoi speed nzuri ndiomaana nakushauri nunua voda modem halafu ichakachue ili uweze kutumia line ya Aitel. modem ya Aitel haina speed nzuri kwa line yoyote ukilinganisha modem ya voda. mimi ninazo zote hizo na nimesha chakachua, so naelewa ninacho ongea.
   
 5. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nisaidie namana ya kuchakachua hiyo ya Voda tafadhali
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  kuna shule kibao humu kuhusu uchakachuaji huu. Sasa fanya homework yako kwa kutafuta.
   
 7. S

  Soki JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Asante kwa ushauri. Nimefaidika!! Ninajua sasa modem ya kununua
   
 8. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii haina ukweli wowote, labda modem ya voda iwe na njia kubwa nikimaanisha kama ya Airtel uwezo wake ni 3.6Mbps na ya voda ni 7.5 mbps, kama ni hivi hapo sawa, ila kumbuka hata kama ya voda ni 7.5mbps ni kwamba hakuna mtandao unaofikia Speed hiyo kwa hapa Tanzania.

  Na kushauri ubane matumizi kwa kununua modem ya tigo ambayo utaitumia kwa Airtel, Airtel speed yake haifiki 3mbps japo wanatumia 3G,kama ukinunua ya tigo fuata maelezo kwenye hii link hapa ili kui-unlock
  https://www.jamiiforums.com/technology-and-science-forum/110615-modem-za-tigo-zina-chakachulika-6.html
   
 9. S

  Soki JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Duh! Uncle Rukus umenifanya nifikirie mara mbili! Mbona BinMgen anasema anatumia zote mbili na ame-observe tofauti za speed zake? Ni nini kinaweza kupelekea tofauti ya speed kwake kama alivyoeleza?
   
 10. C

  CalvinPower JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 996
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  Uncle Rukus yupo 100% sahihi.

  natafuta modem za airtel kama pisi 10 na modem za tigo kama pisi 10 je ninaweza kuzipata wapi kwa dar?
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  usahihi wa 100% haupo, kwani speed inategemea wapi mtu alipo. Speepd unayo ipata wewe uliye kariakoo sio sawa na alie Tegeta au Morogoro, kwa hiyo mtu hutoa majibu kulingana na hali halisi sio matangazo wala kuzania.
   
 12. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mzee alwys rahisi ghali!!mimi natumia tigo hapa!!ila nahisi uimara wake c mzuri!!!halafu haiko that much sensitive,Voda ziko powah!!!
   
 13. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ila tigo is easy to unlock it!!!
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dah,mkuu umenichekesha sana!
  Binafsi sijui kuhusu modem za tigo,ila hiyo ya voda ya 49000 unayo sema sikushauri uichukue maana hata ku-unlock tu ni shida nimejaribu bila mafanikio!

  Bora ukachukua zile za 59000 kama sikosei ni rahisi ku-unlock
   
 15. C

  CalvinPower JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 996
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  Bigmen yeye hajasema anatafuta pa kukaa ili apate speed ya internet bali anasema anataka kuweka line ya airtel kwenye kati ya modem hizi mbili 1. ile inayotolewa na tiGo au - 2. ile inayotolewa na vodaCom. vilevile airtel wana modems zao ambazo ni sawa na hizo walizotoa tigo yaani huawei e153.
  hizi huawei e153 zina Support 7.2Mbps HSDPA services vile vile hata hizo za voda zina Support 7.2Mbps HSDPA services. na ndo maana
  Uncle Rukus akasema hakuna ukweli wowote kwenye maelezo yako labda ukute moja ina njia kubwa yaani 7.2Mbps na nyingine iwe na 3.6Mbps. bado akaendelea kusema kwa tanzania hakuna mtandao unaoweza kufikia hiyo 7.2Mbps.

  kama unazo zote mbili jaribu kuingia kwenye google ulete specifications zake hapa. utaona zina specifications karibu kufanana. kwenye mambo ya speed ndo tunakuja kwenye tofauti ya line utakayotumia na maybe wapi ulipo.
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  @CP Mkuu maelezo yangu sijuwi umayaelewa vp! nilicho sema. line ya Aitel ukiitumia kwenye modem ya voda iliyochakachuliwa inatoa speed nzuri. Suala la Modem hii inatoa 3.6Mbps., na hii intoa 7.2Mbps. mimi hayo kwangu nimatangazo ya biashara tu, ninachoangalia ni halihalisi wakati ninapo itumia. mambo ya google anasemaje kuhusu modem hiyo mimi wala siyazingatii. hizo modem zote 3 ninazo na zote nimesha zickachua, ninachofanya ni kubadilisha line na kuangalia speed ninayoipata sio mambo google kasemaje. kama Mkuu unaongelea mambo ya utaalam zaidi, Ah! mimi huko siko nipo kwenye halihalisi.
   
 17. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Za tigo unaweza kupata pale mlimani City.... Mkuu naona umeanzisha kamradi sio vibaya tukashirikiana kama kuna mlo mzuri mkuu.
   
 18. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Ahsante kwa ufafanuzi wako.
   
 19. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kumbuka modem ni njia tu yaani kwa lugha nyingine tunaweza kusema ni kama barabara, barabara ambayo ina ukubwa flani na inatakiwa ipitishe magari ambayo hayazidi kiwango cha barabara pia kuna kikomo cha kupitisha magari yenye uzito flani kulingana na ubora wa barabara...


  Kuhusu swala la modem ya voda kuwa na speed kubwa pale inapotumika kuwekwa line ya Airtel , hiyo haina ukweli kumbuka kama Airtel wana toa Speed ya 1mbps kwa 3G ndiyo hiyo hiyo ambayo utaipata kwa kutumia modem yoyote ile iwe ya tigo, voda, airtel.... Hivyo ndivyo navyojua mimi .
   
 20. S

  Soki JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,308
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu hizo za 59000 ni za voda au airtel?
   
Loading...