Je Mnyika Amevunja katiba au kanuni za bunge kusema Raisi Dhaifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Mnyika Amevunja katiba au kanuni za bunge kusema Raisi Dhaifu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by William Mshumbusi, Jun 19, 2012.

 1. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tusiliangalie kiushabiki swala hili.

  Kwa mujibu wa kanuni za bunge nasikia ni marufuku kwa mbunge au bunge kujadili mwenendo wa raisi bungeni au nje ya bunge.

  Je kanuni hii inagusa mienendo binafsi yani ya raisi na mkewe na watoto wake au ata mienendo inayoweza kuigarimu nchi kama kutafuta ugonvi na nchi jirani kama ilivyokuwa kwa hitra idd amin na wengine?

  Pia katiba hairuhusu raisi kustakiwa mahakamani akiwa madarakani au akistaafu. Je raisi akianza wizi wa waziwazi au kulinda wezi mtamrekebishaje?

  Kuwa na sheria zisizotenda haki ni hatari. Sheria zilinde watu kwa manufaa ya Umma. Kama inamlinda raisi iwe kwa manufaa ya wananchi wote. Lkn kama raisi akipotoka akifanya kwa maslahi yake yanini kuzifuata shelia. Raisi ni Nafsi mmoja tu. Umuhimu wake upo tu kwa manufaa ya uma. Ila kama ataenda atakavyo turudi nyuma tuone mwonekano wake kuwa Thamani ya nafsi yake na ya masanja mNG'WINAMILA yule kichaa anayekuwa anakula majalalani ni sawa? Zote zilindwe kwa nguvu zote
   
 2. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mara nyingi tunapozungumza habari za raisi tunazungumzia taasisi siyo mtu. Mimi nina imani kuwa mnyika alikuwa anazungumza habari za power ya raisi kikatiba na matokeo yake. Kama angesema JK ni dhaifu labda hiyo ingekuwa mbaya. Hata hvyo nafikiri kanuni zenyewe za bunge zina udhaifu mkubwa. Kwa nyongeza tu, ingekuwa bora kama ungetaja vifungu kama alivyofanya mnyika mwenyewe! Hata hivyo toko pamoja!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kwani angesema ni udhaifu wa rais aliyeko madarakani si bado angewakilisha kuwa ni kikwete ndo alikuwa anasemwa?


  Tatizo halipo kwa John Mnyika wala kwa Lukuvi au kwa Job Ndugai. Tatizo ni kanuni za bunge ndiyo zinazo dictate wabunge kusema.
  Hizi kanuni zilitungwa kwa ajili ya wajinga wajinga wa kipindi kile, mfano akina Lusinde, Ngonyani, Lameck. hizo kanuni ndo ziliwafaa.
  Leo hii bunge letu linaongozwa wabunge wasomi, ambao wapo very intellectual, na kanuni ni za wale wale wa kipindi kile za middle school na waganga wa kienyeji wapi na wapi!

  Kusema kuwa Rais Jk ni mdhaifu, na ccm ni wapuuzi ni ukweli siyo kuvunja kanuni hapa tuache unafiki, tuangalie maslahi ya nchi yanaibiwa na hawa miungu watu wanaoitwa wawekezaji kupitia kwenye mgongo wa ccm!
  Hivi watanzania wote wakiokoka hizo kodi za kutegemea mauzo ya pombe itakuwaje? au ndo tutakuwa tumezikwa?
  SHINDWA SHETANI SHINDWA!
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kwanza nikiri wazi kwamba sheria zetu zilitungwa kwa ajili ya kumuenzi Nyerere tu. Hii ndiyo sababu Mwalimu aliwahi kusema msitunge sheria kwa ili mmkomoe mtu fulani au ili mmlinde mtu fulani.

  Katika hali ya maadili ya kawaida alichokisema Mnyika ni sawa kabisa, hakina shida. Ila pale penye nidhamu ya woga, na hofu ya mwanadamu hili ni kosa. Mnyika kasema kitu ambacho tafsiri yake inaweza kuandikiwa vitabu ishirini na kuendelea. Na kwa kweli si Mnyika ndiye wa kwanza kusema jambo hili.

  Mtu wa kwanza kusema hivi kwa kumbukumbu zangu ni Swamweli Sita, wakati raisi Kikwete alipohutubia bunge kuhusu epa kama sikosea ilikuwa 2008, aliposema, "Mheshimiwa raisi, mimi nadhani unapaswa kuwa mkali kidogo katika mambo haya." Hii ilikuwa dhahiri kwamba Sita aliona udhaifu wa raisi.

  Haikuishia hapo, wabunge, wananchi na hata kagame aliwa kusema akipewa Tanzania kwa miaka mitano ataibadilisha iwe kama US.
  Katika nyakati zote hizo, raisi hakuwahi kuchukua hatua zinazoonesha kwamba yeye si zaifu. Badala yake EPA, Richmond, Meremeta, Jairo, nk.

  Tukiangali kiundani tunagundua kwamba raisi, ameambiwa kwa kutumia tafsiri kwamba yeye ni dhaifu, lakini hakuna hatua aliyochukua kuimarisha utwala wake.

  Kutokana na hali hii, Mnyika kaona tabia ya kutumia tafsida, labda inamfanya raisi asielewe kama yeye ni dhaifu, hii ndiyo maana ameamua kusema wazi kwamba raisi ni dhaifu.

  Na kimsingi hili si tusi kwani udhaifu ni hali ya kutomudu vyema kitu fulani. Unaweza ukawa mnene sana lakini ukawa dhaifu wa kupigana. Udhaifu kwa maana nyingine ni kupwaya.
   
 5. a

  andrews JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1 CD YA UKABILA
  2 CD YA UDINI
  3 CD YA UKANDA

  KWA KUWA WATANZANIA WENGI NI WAELEWA CCM IMEANGUKIA PABAYA KWA KUKOSA WANUNUZI WARNING:SASA CCM INAWATUMIA UAMSHO KUWAGAWA WATANZANIA BILA KUJUA WAZANZIBARI WAMEINGIZWA MJINI HIYO NI HUJUMA YA CCM KUOGOPA MABADILIKO YANAYOKUJA 2015 THE ONLY WAY NI KUWAGAWA WATANZANIA KWA KUWATUMIA AKINA SHEIKH MPONDA NA WAJINGA WENZAKE:bump:
   
 6. SONGOKA

  SONGOKA JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 1,710
  Likes Received: 877
  Trophy Points: 280
  nakumbuka wakati ule nilipomaliza masomo yangu kilichofuata ni kuanza kuomba kazi..katika interview zote nilizofanya kulikua na swali lililojirudia mara zote,tofauti ni muda na mpangilio lakini kila interview swali hili liliulizwa, ni kwa msingi huu mpaka leo nalikumbuka vizuri kabisa, nalo ni ..WHAT ARE YOUR WEAKNESSES?....kuna wakati liliulizwa ..DO YOU HAVE ANY WEAKNESSES?..sikujua kama hawa watu walikua wananikejeli na kunitusi ....mpaka leo zaidi ya miaka kumi na tano ndo NATAMBUA HILO...kweli akutukanae hakuchagulii tusi (think)
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kanuni na sheria ni kama kipofu, havioni. Nilikuwepo Bungeninwakat sakata hili linatokea. Kwa maoni yangu, nadhani Naibu Spika alipaswa kumpa Mnyika Nafas kuelezea anamaanisha nini anaposema kuwa Rais ni dhaifu. Kama angesindwa kuthibitisha ndi alitakiwa aadhibiwe. Kmlazmisha afute kauli kabla hajaelezea alichomaanisha na kuitetea, n unevu. i kweli kanuni zinasema hivyo na ndizo zimetumia kumfukuza Mnyika, ndio maana nasema sheria na kanuni ni kama kipofu
   
 8. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  JJ Mnyika ni shupavu anayebidi apewe support,tena ana hakika alichotaka kukizungumza ndio maana hakutaka kufuta maneno yake.Ni kweli rais ni dhaifu,bunge lake ni zembe na chama chake ni cha kipuuzi.

  Dhaifu kwasababu serikali yake imeshindwa kuwafikisha mafisadi papa mpaka leo mahakamani,mbaya zaidi inatumia wabunge wake dhaifu kuwachagua kuwa wenyeviti wa kamati za bunge za kudumu bila aibu.Mbaya zaidi wafanyabiashara wameiweka serikali yake kwenye mifuko yao na serikali imekuwa bubu kwa kila watachoamua wafanyabiashara hao.

  Bunge zembe kwasababu ndilo linalo pitisha sheria zinazokinzana na maendeleo ya nchi kwa kutumia wingi wa wabunge vihiyo wa CCM na wasomi uchwara wanao dhalilisha taaluma ya elimu kw kujenga hoja kihiyo kwa maslahi ya watu wachache wenye uroho wa mali na ukiritimba wa madaraka.

  Chama kipuuzi kwa kushindwa kuisimamia serikali yake iliyoko madarakani hali inayo pelekea kila mmoja kuchukua chake mapema.Chama legelege ndicho tu kitacho zaa serikali legelege kama serikali yetu ilivyo.Hivyo basi alichosema JJ Mnyika ni sahihi zaidi ila kwa kuwa bunge ni la kishabiki zaidi hakupewa muda wa kufafanua kauli yake ili kuthibitisha udhaifu wa rais,uzembe wa bunge na upuuzi wa CCM
   
 9. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama rais hajadiliwi je, kura ya kutokuwa na imani na rais kwa mujibu wa katiba inapigwa vipi?
  Watu wengi wanatumia neno rais ni taasisi, kujaribu kuficha udhaifu wa kiuongozi. Ukweli ni kwamba rais ni mtu, anayechaguliwa na watu kuwatumikia watu hao katika wadhifa wa urais. Wadhifa huu hauna ubia, ndio maana ni rais pekee anayetia saini utekelezaji wa hukumu ya kifo, ni rais pekee anayetangaza vita, na kadhalika. Kutokana na shughuli na unyeti wake ziko baadhi ya kazi zake anaweza kukasimu madaraka yake kwa watu wengine. Kushindwa kwa serikali yake kutekeleza majukumu yake ni kushindwa kwake moja kwa moja.
  Tuache propaganda za ooh rais ni mchapakazi ila watendaji wake ndio wanaomwangusha. Yeye ndie mwajiri mkuu, kauli yake ni sheria, kama hawezi kujua nguvu zake, huyo ni dhaifu.
   
 10. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Naona ukimsifia rais bungeni kanuni haiangaliwi lakini ukimkosoa tu wkt rais ni binadamu na wala si Mungu basi majinga kadhaa yanakutolea mimacho kama mjusi kabanwa na mlango.
   
 11. Imam Yussuf Shamsi

  Imam Yussuf Shamsi Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni vizuri kuwa na busara wakati ukizungumza mbele za watu, matusi hayasaidii na wakati mwengine inaweza kukuharim
   
 12. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Ukweli utabaki kuwa ukweli daima na wakati mwingine tunahitaji roho ngumu kuusema ukweli kwasababu kweli yoyote ina machungu kwa makundi fulani ya watu wakati wowote. Katika kisa cha mnyika ukweli una machungu kwa kundi la watu wenye mamlaka naye. Lakini ni ushujaa kusimamia ukweli hata kama ni kinyume cha taratibu. Ni dhahiri kuwa taratibu zimetengenezwa na watu, hazikuzaliwa tangu uumbwaji wa dunia hivyo wakati mwingine (na hasa kwa nchi yetu) taratibu hizi zinatengenezwa kuwalinda watu fulani au kundi flani linachomeka maslahi yao kwenye taratibu hizo. Kwa kufanya hivyo unashindwa kuongea ukweli kwasababu tu wao walishaona mwanya huo na maslahi yao yanakuwa hatarini. Unahitaji ushujaa kuusema huo ukweli na mnyika amefungua njia. Hali hii ni kuibaka demokrasia na kwa hulka ya wanadamu watafika wakati watachoka. Amani tunayodhania tunayo itaondoka kwaajili ya vitaratibu vya ajabu ajabu vya kubaka demokrasia yetu
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Hivi kazi ya Lukuvi bungeni ni nini?? Maana kila likizuka jambo huwa nasikia Lukuvi anatajwa pamoja na makamu wa spika!!
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,582
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Alichokuwa anataka kufanya Mnyika ni kueleza moja wapo ya wasifu wa rais wetu.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii nchi imepitia kurasa nyingi na baadhi yake zina za aibu. Tulishakuwa na 'zidumu fikra za mwenyekiti' na tukio la bungeni linaonesha bado tuna chembechembe za zama hizo za 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Kama wangemuacha Mnyika amaliziea hoja yake wangeweza kuona udhaifu uko wapi.

  Kwa mtazamo wangu Mnyika alikuwa anaongelea "presidency' kama taasisi iliyobuni mpango wa maendeleo ya miaka 5 na baadae ukaridhiwa na bunge. Sasa kwa miaka miwili mfululizo serikali hiyo hiyo inawasilisha bajeti inayopingana na mpango huo! Mwaka jana walisema the reason hawakutenga 35% kwa ajili ya kutekeleza mpango huo ni kwasababu ulikuwa mwaka wa mpito, sasa mwaka huu ni mwaka wa kitu gani?

  Lakini hebu wanasiasa wetu waache kuwa too sensitive na kudeka deka. Kuna kulia lia kwingi sana bungeni utadhani ni watoto wadogo.

  Kwenye kanuni, neno 'kuudhi' limeachwa bila ufafanuzi. Wabunge wanatakiwa kufafanua ni wakati gani mbunge atahukumiwa kuwa ametoa ligha ya kuudhi? Ni lazima kanuni kuangalia upya hizi kanuni ili ziendane na halisi ya sasa. Wananchi wanataka majibu ya uhakika, hatuna muda wa kuwa na bunge la kubembelezana na kulia lia. Lazima wanasiasa waanze kubadilika kifikra.
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Yule mwenyekiti hakutaka mnyika aoneshe udhaifu wa jk.

  Kila mtu anajua jk ni dhaifu.
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  mnyika hajamjadili rais... Amempa sifa stahiki. Angemsifia ungesema amemjadili?
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kamanda wa ukweli akitolewa nje ya bunge la matusi!
  [​IMG]
   
 19. Msambaa mkweli

  Msambaa mkweli Senior Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wamerekani wanasema Mr President. Je Mnyika kataja Taasisi au Mr President? Kisheria hakuna hukumu ya one to one kuhusu Mnyika. Swala la msingi alikuwa atoe ufafanuzi zaidi ya hapo kanuni za bunge pia zina udhaifu mkubwa. Nawasilisha.
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapa inaonesha kuwa na naibu spika nae ni dhaifu!
   
Loading...