Je, mnakumbuka yale ya kamati ya Bunge iliyochunguza madini ya Tanzanite na taarifa ya kamati kukabidhiwa kwa Rasi bila Bunge kuijadili?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Sakata la CAG na Spika limenikumbusha hii habari ambayo nayo ilizua ubishani mkubwa ambapo wapinzani walipinga jambo hili huku wale wa chama tawala wakitetea na kudai Spika alikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo (kumkabidhi Raisi).

Inawezekana kweli Spika alikuwa na mamlaka ya kufanya alichokifanya.Swali ni je, ripoti ile imefanyiwa kazi gani?

Je, ingeingia Bungeni na kujadiliwa, leo hii Bunge si lingeweza kuwa na walau haki ya kuhoji hatua zilizochukuliwa?

Waacha niishie hapa nisije nikaharibu.
 
Hivi walipomuita Zitto Kabwe kwenye kamati ya maadili, akawapa facts zao, walimpa adhabu gani? Nakumbuka Edo Kumwembe akisema kwamba inaonekana alipokuwa akiwapa yao, mioyoni wanasema "Lakini kweli"
 
Hivi walipomuita Zitto Kabwe kwenye kamati ya maadili, akawapa facts zao, walimpa adhabu gani? Nakumbuka Edo Kumwembe akisema kwamba inaonekana alipokuwa akiwapa yao, mioyoni wanasema "Lakini kweli"
Nimecheka sana mkuu!!
 
Wakiambiwa dhaifu wananuna yaani hawa ni dhaifu dhaifu dhaifu kabisaa hamna kitu kuanzia supika na wenyewe
 
Kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake, hapa hapa duniani naisubiri hiyo Siku kwa hamu sana, maana siku hazigandi
 
Back
Top Bottom