Je, mnajua kama Tanzania kuna kokoa?

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,695
2,553
Zao la Kokoa hutokana na mti wa kakao (Theobroma cacao) ni maarufu sana katika nchi za Cameroune, Ivory Cost, Ghana na Nigeria na huko ndiko zaidi ya nusu ya kakao yote duniani inazalishwa kikubwa zaidi inamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi na wananchi. Zaidi ya tani milioni 2.5 zinazalishwa Ghana na Ivory Cost pekee, Tanzania inakadiriwa kama Tani 7,000 zinazalishwa kwa mwaka.

Wilaya ya Kyela na Rungwe zinazalisha zaidi ya 95% ya kakao yote inayozalishwa Tanzania Pia Morogoro-Ifakara na Tanga-Maramba nako inalimwa kokoa na ndio kwenye uwezekano wa kuongezeka mashamba pia kuna maeneo ya hali ya hewa inayofaa kwa kokoa kama Kigoma.

Najua mko na kazi nyingi na kilimo hakipo katika priority zenu lakini kokoa ni zao la mti (kama miembe, korosho, michungwa na minanazi)ukipanda once, replacement baada ya miaka arobaini na kila mwaka utapata kipato cha kutosha lakini unatakiwa kusubiri miaka 3 mpaka 5 kuanza kuzalisha. Mti mmoja unaweza kutoa sichini ya kilo2 kama utatunza vizuri unaweza pata mpaka kilo 3, kilo moja kwa sasa inauzwa Sh. 2,000 kakao iliyokaushwa. (Ukivuna tunda la kokoa, unalipasua na kuvundika mbegu kwa siku 6 na kuanika kwa siku 5 ndio unaziuza). kwa ekari ni miti isiopungua 400 mche mmoja Olam wanauza Sh. 100 Kyela. Kwa kifupi kipato kinazidi Tshs. 1.5 kwa ekari kama utazingatia kanuni za kilimo bora. Shamba hilo hilo pia unaweza panda migomba.

Kakao inatumika kutengenezea chokolate, tofauti na kakao zingine ya Tanzania inatokana na kilimo Hai (hakuna kupiga dawa au kutumia mbolea za viwandani), kwa hiyo soko la vitu ambavyo ni organic linakuwa kila kukicha na bei nzuri.
 
nadhani ni zao zuri katika uwekezaji na nadhani ukilipanda pengine faida yake kimapato inweza kuzidi hata ya matunda ya miti kama embe ambazo huwezi kuzitunza kwa muda mrefu na pia kuna wadudu waharibifu kama inzi wa matunda ambao wanasababisha soko la matunda (fresh fruits) kushuka kila kukicha. Kama inastawi Kyela bila shaka mikoa yote ya ukanda wa pwani inaweza kustawi. Sasa pengine mdau utuambie kama kati ya korosho na kakao tulime kipi?
 
Suala ni soko! Hicho kipato cha 1.5 m kwa eka unakuwa umeuza kwa nani; mbona unaongelea kipato gharama zake kwa ekari je?
 
Gharama ni capital investment zaidi na kijana atakaye kutunzia shamba, madawa hakuna na mbolea hakuna. Sasa gharama hazifiki Tshs. 500,000. Vinginevyo wakulima wasingeweza tunza, gharama kubwa kununua shamba na kupanda kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Anyisile amesema kwao ipinda atakwambia gharama na kutoa ushuhuda ndizo zinazo endesha maisha ya kina Mwanafyale na vurugu zote hizi mjini. (Jokes)
 
Wanunuzi kibao kuliko uzalishaji ndio maana Olam wanatoa miche kwa Sh. 100 wakati mche wa namna hiyo Dar unazidi sh. 1,000.

Sema mkulima kunyonywa ni kama kawa na ndio maana wasomi mkiwekeza mnaweza kuleta tofauti manake mtakuwa hamna njaa kama babu zenu wa Matema/ipinda. Ambao hawawezi subiri siku 15 mpaka kufuata vigezo, Labda wakina Mwa....... watatupa uzoefu zaidi manake tunao humu jamvini.
 
Wanunuzi kibao kuliko uzalishaji ndio maana Olam wanatoa miche kwa Sh. 100 wakati mche wa namna hiyo Dar unazidi sh. 1,000.

Sema mkulima kunyonywa ni kama kawa na ndio maana wasomi mkiwekeza mnaweza kuleta tofauti manake mtakuwa hamna njaa kama babu zenu wa Matema/ipinda. Ambao hawawezi subiri siku 15 mpaka kufuata vigezo, Labda wakina Mwa....... watatupa uzoefu zaidi manake tunao humu jamvini.
Hahaha
Kwa kifupi ni zao tamu sana kwa maana linalipa sana ila mnunuzi ananufaika zaidi
 
Nilipotembelea wilaya ya kyela nilijionea kilimo cha kakao .
Wakulima hali zao ni duni sana,
tatizo lao kubwa ni soko.
Mnunuzi mkubwa ni mohamed enterprises.
Si unaju sifa za wanyonyaji, wanakunyonya hadi mfupa.
Wahindi wananyonya balaa, tena wakiwa wao ndo unawategemea wanunue wanakuumiza
 
Zao hili lina simamiwa na bodi maalumu kama ilivo kwenye pamba, kahawa na korosho? Hii itasaidia kwa mkulima kufanya maamuzi sahihi
 
Mimi nipo huku Kyela nimeyaona hayo makokoa ki ukweli hili zao hadi mkuu wa wilaya analiguatilia na zao ambalo linawalea na kuwasomesha wanyakyusa kuna watu huku ukimuambia niuzie shamba la makakao anachukulia kama vile umemuambia auze ajira yake.
 
Basi si kuna mapori mengi,
serikali itoe ruzuku kulikuza hili zao tuwe tunaexport maelfu ya tani
 
Nilipotembelea wilaya ya kyela nilijionea kilimo cha kakao .
Wakulima hali zao ni duni sana,
tatizo lao kubwa ni soko.
Mnunuzi mkubwa ni mohamed enterprises.
Si unaju sifa za wanyonyaji, wanakunyonya hadi mfupa.
Ukizingatia na kanjibahi
 
Back
Top Bottom