Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,695
- 2,553
Zao la Kokoa hutokana na mti wa kakao (Theobroma cacao) ni maarufu sana katika nchi za Cameroune, Ivory Cost, Ghana na Nigeria na huko ndiko zaidi ya nusu ya kakao yote duniani inazalishwa kikubwa zaidi inamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi na wananchi. Zaidi ya tani milioni 2.5 zinazalishwa Ghana na Ivory Cost pekee, Tanzania inakadiriwa kama Tani 7,000 zinazalishwa kwa mwaka.
Wilaya ya Kyela na Rungwe zinazalisha zaidi ya 95% ya kakao yote inayozalishwa Tanzania Pia Morogoro-Ifakara na Tanga-Maramba nako inalimwa kokoa na ndio kwenye uwezekano wa kuongezeka mashamba pia kuna maeneo ya hali ya hewa inayofaa kwa kokoa kama Kigoma.
Najua mko na kazi nyingi na kilimo hakipo katika priority zenu lakini kokoa ni zao la mti (kama miembe, korosho, michungwa na minanazi)ukipanda once, replacement baada ya miaka arobaini na kila mwaka utapata kipato cha kutosha lakini unatakiwa kusubiri miaka 3 mpaka 5 kuanza kuzalisha. Mti mmoja unaweza kutoa sichini ya kilo2 kama utatunza vizuri unaweza pata mpaka kilo 3, kilo moja kwa sasa inauzwa Sh. 2,000 kakao iliyokaushwa. (Ukivuna tunda la kokoa, unalipasua na kuvundika mbegu kwa siku 6 na kuanika kwa siku 5 ndio unaziuza). kwa ekari ni miti isiopungua 400 mche mmoja Olam wanauza Sh. 100 Kyela. Kwa kifupi kipato kinazidi Tshs. 1.5 kwa ekari kama utazingatia kanuni za kilimo bora. Shamba hilo hilo pia unaweza panda migomba.
Kakao inatumika kutengenezea chokolate, tofauti na kakao zingine ya Tanzania inatokana na kilimo Hai (hakuna kupiga dawa au kutumia mbolea za viwandani), kwa hiyo soko la vitu ambavyo ni organic linakuwa kila kukicha na bei nzuri.