Je mmliliki wa theutamu kadakwa?

Absolute

JF-Expert Member
Jan 19, 2007
333
61
Mkuu;
Poleni kwa majukumu ya kila siku ktk kujenga inji hiii...

Eti ni kweli kwamba mmliki wa theutamu (Malecela Peter Lusinde) amedakwa?

Naomba unijulishe maana nimeona kwenye kablu flani (http://mpoki.blogspot.com/2009/06/utamu.html) wameandika as below;

BREAKING NEWS

Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa

(Interpol),wamefani kiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana

asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa

miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu. Ndugu

Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa

kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahil na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na

wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata

ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara

ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania

mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na

Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job

Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za

utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa

Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa

unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu

udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo

ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya

Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya

Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya

picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni

wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania. Licha ya Ndg. Malecela

Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika

miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani, ambao pia wanahusishwa

na Mtandao huo wa Ze Utamu.
--------------------------------------
Mwenye ufahamu kuhusu hili plz atusaidie with details.
 
Eti ni kweli kwamba mmliki wa theutamu (Malecela Peter Lusinde) amedakwa?

niliwahi kusoma hii habari kwenye magazeti hapa bongo. sikuwahi kuona ikiendelezwa. nna mashaka kama hata walifanikiwa kumleta hapa wamshtaki maana iliripotiwa kuwa huyu bwana ana uraia wa uingereza.

kama mtu ana data zaidi atumwagie.
 
tembelea www.whois.ws andika theutamu.com click on who is utapata taarifa ya tovuti hiyo kuanzia hapo ndio uanze uchunguzi wako .

Kwa tovuti kama hiyo njia rahisi zaidi ilikuwa ni kuifungia isiweze kuonekana hapa nchini ingawa wengine wanaweza kuitembelea kwa njia zingine usiulize ni zipi , kitu kingine tovuti hiyo inawezekana imesajiliwa sehemu ambapo sheria zinamruhusu kufanya hivyo , kwahiyo ukitaka kumshitaki yote hayo inabidi uyajue sio ukurupuke tu .

.........................

Nikupe kisa kimoja , si unajua nchi ya uholanzi watu wanaruhusiwa kutumia bangi wakati uingereza hiyo ni marufuku ? huko uholanzi kuna tovuti zina uza bangi watu wa uingereza wananunua kwa njia ya mtandao na wanapelekewa
 
ndio ndugu yangu wewe agiza bangi uholanzi utatumiwa ingawa lina tatizo la kisheria sawa na hiyo zeutamu kwetu inawezekana alikuwa anafanya makosa lakini kule ambako tovuti hiyo ilisajiliwa ni haki yake kufanya hivyo -- unaona ??
 
Huyo jamaa hajakamatwa na wala hakuna proof yoyote iliyoonekana kuwa yeye ndio TheUtamu. Story nzima ilukuwa uzushi inaelekea. Soma habari yenyewe, Interpool waache mambo ya maana waanze kumtafuta mmiliki wa blog ya kipumbavu?
 
Ndugu ile ilikuwa ni kutangaza blogu fulani hivi na kama ulivyoona ilivyotangazwa tu ikawa linked na sehemu nyingine kwa maslahi ya kibiashara zaidi
 
Back
Top Bottom