Je! Mmejifunza nini kutokana na habari hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je! Mmejifunza nini kutokana na habari hii?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Oct 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Jamaa mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza kuwa si uyoga wa kula.
  Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe, halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule waliobakisha nao wale.

  Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya kwanza,ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga uliobakia nao wakala.

  Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa wao amekufa.

  Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa maisha yao umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula uyoga kama mbwa alivyokula.

  Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya. Kwanza msichana wa kazi waliomfukuza akiwa na ujauzito, ule ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.

  Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nani nitubu Kwako. Huyu mtoto wa kiume mdogo si wakon nilizaa na Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji wetu humu ndani.

  Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa mule ndani.

  Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza ,Baba na mama mnagombania nini humu ndani,badala ya kwenda kuona mbwa wetu amekufa kwa kugongwa na gari kule nnje?

  Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.

  Chanzo: Mzizimkavu
   
 2. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watu hawatubu hadi wafikwe na umauti??? u made my day
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Tumejifunza kwamba tusiwe na tamaa ya manenge na mandawa.!
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Tusifanye maamuzi ya haraka,think first
   
Loading...