Je, mkopo wa tril 1.3 wote umetumika kujengea madarasa? Vipi kuhusu madarasa yaliyokuwa yanajengwa kwa tozo za miamala? Ukaguzi ufanyike tupate ukwel

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Ni suala ambalo watanzania bado linawaumiza kichwa maana kwa tozo tunazokamuliwa alafu tukaambiwa na Ummy Mwalimu kuwa tozo zinatumika kujenga madarasa, zahanati vituo vya afya na kununua vifaa tiba.

Ghafla bin vuu tukasikia ili kukabiliana na uhaba wa madarasa mkopo wa Uviko upatao tril 1.3 umekopwa na madarasa yatajengwa, kweli yamejengwa. Lakini je tril 1.3 zote zimetumika kujengea madarasa?

Wastani wa darasa moja kwa forced account ni mil 35 za kitanzania. Sasa je kwa kata moja zimetumika mil ngapi? Je tril 1.3 ndio zote zimetumika kwa huu ujenzi wa madarasa?

Je, ndio ule usemi umetimia kuwa bunge letu ni dhaifu?
image_search_1641235094633.jpg
 
MKIONA HAMUELEWI YANAYOENDELEA NCHINI KWENU HAMENI, Tena hamieni Congo!.
 
Tozo unakusanya taratibu, inachukua muda kujaza kibubu cha kutosha kujenga hayo madarasa yanayokusudiwa ndio maaaana tunakopa nyingi zinazotosha kufanya hayo mambo sasa hivi kisha tunawakusanyia kuwalipa hao tuliowakopa tukiwa na madarasa tayari.

Unataka ukamuliwe tozo kwa miaka 5 ndio madarasa uyaone mwanao akiwa kamaliza shule?

Kuhusu thamani ya pesa na idadi ya madarasa fuatilia almashauri idadi ya madarasa yaliyojengwa nchi zima kisha thaminisha.
 
Walivyotangaza kuwa huwa wanazitafuna tena kupitia TV ya Taifa,hukupata taarifa?Huko kwenu hakuna TBC Taifa?🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom