Bexb
JF-Expert Member
- Oct 24, 2016
- 655
- 1,390
Asante kwa nyongeza mkuu, lakini tukumbuke kesi nyingi za madai ya aina hii ya 'kukopeshana mtaani' zikienda mahakama za mwanzo ambako wakopeshaji wengi hukimbilia mahakimi wengi wamekua wakijikita zaidi katika hii hii sanctity of contract na pale inapoonekana kama riba ilikua unfair basi hu'disregard hiyo na huamua kiwa mkopaji arejeshe kile kiasi pekee alichopokea.Hii ya kukopesha fedha, ukisoma hukumu ya Mahakama ya Rufaa haijaruhusu perse kuwa hata watu wasiosajiliwa wanaruhusiwa kukopesha kibiashara, kilichoelezwa ni kuwa nia ya mkopo inazingatiwa kama mkopo wenyewe haujakaa kibiashara.
Mfano, Katika kesi hiyo unayoizungumza, mkopaji alikopa Tshs. 2,600,000/= na kuahidi kuzirudisha kama zilivyo baada ya muda fulani, isipokuwa akishindwa kurudisha baada ya muda huo itampasa kurudisha na riba ya asilimia 30 kwa kila mwezi. Kwa hiyo hakukuwa na nia ya kibiashara tofauti na mkopo ungekuwa ni Tshs. 2,600,000/= inayotakiwa kulipwa baada ya miezi 3 ikiwa na riba ya asilimia 30. Hapo lazima leseni ya biashara ingehitajika.
Lakini pamoja na hilo tunaona kuwa watu wanaendelea kudhurumiana kutokana na hizi precedents mbili japo ninaona zinawapa nafuu wakopeshaji wa mtaani kutoka kupoteza fedha zao kwa wakopaji wasio waaminifu.
Halafu pia kama hutajali naomba uweze kuishare hapa hiyo case maana najaribu kuperuze lakini siioni.