Je mkoa wa Mara hauna wa kuwasemea au mikoa mingine ndiyo ina mafundi zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mkoa wa Mara hauna wa kuwasemea au mikoa mingine ndiyo ina mafundi zaidi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibunago, Aug 15, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mara ya pili nimemsikia Mheshimiwa Zitto, akiongea Bungeni kwa msisitizo kuwa Mwanza Airport ni uwanja nyeti na unatakiwa uendelezwe kuwa Serengeti International Airport hususani kwa ajili ya kuwahudumia wageni (Watalii) na raia kwa ujumla wanaozuru Serengengeti NP.

  Maswali: ni kwa nini Uwanja wenye jina hilo na hadhi kama hiyo usijengwe Mkoani Mara ambako ndiko kuna Serengeti NP? Kwa nini usiweze kujengwa sehemu moja wapo nje ya NP ama ktk makao makuu ya Wilaya (Mugumu) au kuuendeleza ule wa Musoma, kuliko kuandaa Airport Mwanza umbali wa 4-5 hrs drive kwa ajili ya wageni wanaopanga kwenda Hifadhini Serengeti?

  Hivi kwa nini huo Mkoa wa Mara umeachwa sana hata katika huduma za elimu na afya na hakuna wa kuuzungumzia au kuupigania sawia?
   
 2. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wazo lako zuri tu, lakini economy-wise ule uwanja ukiboreshwa pale mwanza kuna uwezekano mkubwa wa kuwasaidia watu wengi zaidi kama vile, migodini kama geita, kakola, buzwagi na mwadui pamoja na nyamongo. Biashara nyingi zikiwemo za makampuni makubwa ya mafuta ambayo yana depot zao mwanza, viwanda vingi na pia wakaaji wa mwanza ambao kwa kupunguza gharama za usafiri wa anga siku hizi ni wengi wanaweza kutumia usafiri huo.
  Vile vile uwanja ukipewa nafasi kubwa ya kutua ndege kubwa zinazoleta watalii moja kwa moja, inatoa fursa nyingine ya uwekezaji kwenye tours and safaris - ingawa kwa sasa imeshikiliwa na wahindi -kitu ambacho kinaongeza nafasi za ajira na pato kwa serikali.
  Kwa yote haya viwanja vya Musoma na Serengeti vinatakiwa kuboreshwa ili kusaidia traffic ya Mwanza -
   
 3. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni siasa uchwara za ccm!!!!! Hakuna economic plannings zozote ya maana hadi ccm ing'oke madarakani!!!
   
 4. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Acha kulalamika!!!!! Tumia vizuri haki yako ya kikatiba ya kupiga kura na kuhakikisha ccm inang'oka 2015. cdm daima!!!!!!!!!!! Ndani ya ccm hamna jipya zaidi ya ulaji na unafiki uliopitiliza.
   
 5. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  moja mambo yaliyodumaza Mikoa jirani ya mwanza ni kutokana na huduma nyingi kupelekwa Mwanza, Musoma nao wanastahili kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa kwani vivutio walivyonavyo Mwanza hata wao wanavyo,wana ziwa ambalo linatoa samaki wanaoweza kusafirishwa moja kwa moja ulaya,wana madini na pia mbuga kubwa ya wanyama ambayo itawafanya watalii kutua moja kwa moja badala ya kupitia Mwanza hii itachochea ukuaji wa ajira na kuongeza kipato kwani hotel nyingi zitajengwa na makampuni ya Tours yataanzishwa pia mkoa huu unapaka na Kenya hivyo wananchi wa Kenya jirani na Mara itakuwa rahisi kwa kuutumia Hivyo sikubaliani na hoja ya kutojengwa Uwanja wa ndege Musoma kwa ajili ya kuimarisha wa Mwanza
   
 6. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mi kwa maoni yangu mpango ungekuwa hivi, Uwanja wa Musoma upanuliwe kufikia hadhi ya kimataifa, alafu kutoka Musoma kuelekea Tarime kuna lami tayari, cha kufanya hapa ni kujenga barabara ya lami kutoka Tarime kupitia Nyamongo kuelekea Mgumu ambapo ndio makao makuu ya Serengeti na kwa kufanya hivyo, maeneo yote Toka Musoma hadi Serengeti yatafaidi sana na Mbunga za wanyama za Serengeti kwani mahoteli yanwezwa kujengwa Musoma, Tarime au Nyamongo na hapo pote watu wakapata ajira na Serikali kuongeza mapato.
   
 7. Manstone

  Manstone JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2017
  Joined: May 12, 2013
  Messages: 387
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  duh kazi kweli
   
Loading...