Je, mkataba kati ya serikali na kampuni ya wahindi wa TRL... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, mkataba kati ya serikali na kampuni ya wahindi wa TRL...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Sep 14, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  ...unawaruhusu kununua mabehewa ya mitumba? Kwani Watanzania hatustahili kusafiri kwa mabahewa mapya?

  TRL yapata mabehewa mitumba
  Evance Ng'ingo
  Daily News; Sunday,September 14, 2008 @00:03

  Mabehewa 23 ya abiria yaliyoagizwa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka India yamewasili nchini tayari kwa safari za Kigoma na Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Bandari ya Dar es Salaam wakati wa upakuaji wa mabehewa hayo, Ofisa Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez, alisema kuwa mpaka jana tayari mabehewa sita yalikuwa yamepakuliwa kutoka melini.

  Mabehewa hayo yamewahi kutumika huko India. Maez alisema kuwa kila behewa lina uwezo wa kuhudumia abiria 48 ambapo wakati wa mchana behewa linaweza kutumiwa kwa kukaa kama daraja la tatu, na usiku hutumika kama vitanda vya kulalia.

  Maez alisema kuwa mafundi wa Reli kutoka nchini India wanatarajia kuwasili nchini wiki ijayo kwa ajili ya kufanyia marekebisho mabehewa hayo kabla hayajaanza kazi mwezi ujao. Maez alisema kuwa mabehewa hayo yatasafirisha abiria zaidi ya 1,104 hivyo inatarajiwa yataboresha safari za kwenda na kutoka mikoa ambako TRL inatoa huduma. Maez alisema kuwa kama TRL ingeagiza mabehewa hayo kutoka viwandani ingechukua zaidi ya miaka miwili hivyo ingesababisha mtafaruku kwa watumiaji wa huduma hiyo ya treni.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  Huu ni ufisadi mwingine kama ule wa IPTL na Richmond. Wahindi wanalipwa mabilioni na serikali ambayo yanawawezesha kabisa kununua mabehewa mapya lakini wanaenda kununua mitumba ili kuongeza faida yao. Kama hawana uwezo wa kununua mabehewa mapya basi mkataba utenguliwe na mapema badala ya kutuletea pollution ya mabehewa mitumba toka India. Si ajabu hata TBS hawajayakagua mabehewa hayo.
   
 3. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Lazima kuna mkono wa mtu hapa, tuliza boli sio mbali utasikia kigogo fulani ana kula tenda ya hawa wahindi, inakuwaje serikali inalipa mpaka mishahara ya wafanyakazi wa hii reli?!
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2008
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi ninachoshangaa ubinafishaji wa hii kampuni haujabadilisha quality ya reli na service. Tunatakiwa kubinafisha kampuni kwa kampuni itakayo badisha ushafirishaji wa reli kama kuweka mabehewa na trani za umeme.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  Na wahindi kwa kuhonga ndiyo wenyewe, lakini tuuvalie njuga huu mkataba kama uliwaruhusu wahindi wakanunue mabehewa yaliyochoka kwao ili wayalete Tanzania. Si ajabu wanaweza kuonyesha 'wameyanunua' kwa bei karibu na bei ya mabehewa mapya. Kampuni ya Reli India wanapata michuzi ya kununua mabehewa mapya halafu bongo wanatushushia mitumba. Tutalala mbele na mkataba huo mpaka kieleweke. Tumeshachoshwa na mikataba ya kifisadi. Hata kabla EPA, Meremeta, Richmond, IPTL, Kiwira, Ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi bado haijamalizwa utata wake wameenda kuibua mkataba mwingine wa kifisadi.
   
 6. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  watieni moyo wawekezaji.hapa naona zimejaa chuki utazani walikuja kuomba kuwekeza kumbe ni wizi wenu wenyewe ndio umewaponza mpaka mkaua makampuni yenu.
   
Loading...