Je Mkapa, Bomani na Prof. Shivji mawakala wa Dr. Slaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Mkapa, Bomani na Prof. Shivji mawakala wa Dr. Slaa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 7, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Jambo Leo la leo lina kichwa cha habari kisemacho.........."Mkapa, Bomani na Prof. Shivji wasiwe mawakala wa Slaa"

  Swali la kujiuliza hapa ni hivi harakati za kutaka katiba mpya zamilikiwa na Dr. Slaa au na raia wote hata kuwafanya wale ambao wanashauri mchakato wa katiba mpya una masilahi makubwa kitaifa sasa kuvikwa joho ni mawakala wa Dr. Slaa?
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jibu sahihi hapa kwa swali hilo ni HAPANA.

  Nijuavyo mimi, akina Mzee Mkapa, Prof Shivji, Jaji Mstaafu Warioba, Balozi Salim Ahmed Salim, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, Prof Baregu, Dr Rweitama, Tanzania Law Society, Mama Nkya, Tundu Lissu, Jamii Forum, UDASA, Peter Maina, Prof Safari, miongoni mwao Wa-Tanzania wengine wengi tu ni kwamba wamejiamulia tu kuwa MARAFIKI WA SAUTI YA HAKI ambayo, kipekee, ndio sisi vijana tumeamua kutii na wala si sura wala cheo chamtu.

  Japo hilo gazeti mimi silifahamu kabisa na wala sitohitaji kujua wamiliki wake kwa leo lakini ingekua vema wakarudishiwa jibu sahihi kwamba hao watu hapo juu na wengine wengi ambao wataendelea kujitokeza kuunga mkono msimamo wa mabadiliko si MAWAKALA WA DR SLAA BALI NI MAWAKALA WA 'SAUTI YA HAKI' tena kwa kujichagulia bila kununuliwa na fisadi yoyote.

  Hebu ngoja kidogo ndani ya wiki kama mbili toka sasa mambo makubwa yatakavyojitokeza na misimamo ile migumu ya serikali kutoweka kabisa huku wananchi na taasisi mbalimbali zenye kuheshimika sana nchini mwetu zikiendelea kutoa misimamo isiotetereka kuhusu mabadiliko ya kweli na kukataa UFISADI.
   
 4. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Napenda katiba mpya,tena ambayo itapunguza nguvu za rais,tena ambayo itatoa mwelekezo wa jinsi wa mawaziri watakavyo patikana,tena ambayo itaweka uko wa wizara,tume huru ya uchaguzi n.k....Lakini nauliza hivi katiba mpya ndio muharubaini wa matatizo wetu na umaskini au tunahitaji elimu na ufahamu kwanza wa mambo????
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mpishi huhitaji kuwepo kwanza CHUNGU ndipo akaweze kuonyesha upishi wake na ubingwa wote. Chanzo cha moto nacho ni muhimu lakini anaweza kujichagulia ama jiko lakuni, la china , la umeme na kadhaliko.

  Kwa maendeleo ya maendeleo ya nchi KATIBA MPYA na Tume Huru ya Uchaguzi ni zaidi ya Muarubaini sana sana labda tukabuni neno lingine kama MTHEMANINI wa kuelekeza uchumi uendeshwe vipi, VIONGOZI wa kusimamia maendeleo ya kiuchumi ndani ya nchi wapatikane vipi BILA KUPITIA MILANGO YA NYUMA, na pia waondolewe vipi.

  Hivyo KATIBA MPYA na Tume Huru ya Uchaguzi si tu MUARUBAINE bali pia ni MTHEMANINI wa kuweza kuhakikisha utulivu na amani isilazimishwa kwa kukandamizana na kuiba kwingi kila sekseni ya nchi kama ambavyo ilivyo sasa. Vyombo hivyo viwili, kama nguo huchakaa na kuhitajika mtu kushona nyingine tena kwa kuzingatia fesheni ya wakati huo.

  Swali nyingine mheshimiwa???
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Inakuaje mzee wa kukandya kokoto [MKAPA] kuwa dalali wa kokoto hizohizo?
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani Kikwete kuna siku alisema au kutangaza kuwa hataki katiba mpya?

  Mimi nashangaa sana kwa jinsi watu wanvyorusha madongo kwa vitu vya kawaida na vinavyoongeleka. Si wabunge wapeleke mswada Bungeni, huko ndiko kunakojadiliwa sheria na kama ni katiba mpya si lazima ianzie Bungeni?

  Ya nini watu kuanza kupaka matope wakati JMK hana cha ku lose kwa kuwa na katiba mpya. Sioni hata sababu moja ya kumfanya JMK akatae kuanza mjadala wa Katiba mpya. Nadhani hata yeye wazo hili analiunga mkono.

  Hili si wazo la Slaa au Chadema, ni wazo lililotolewa siku nyingi na Serikali ya CCM ilisha liundia tume. Sioni cha ajabu wala cha kushinikiza. Labda wapuuzi wachache wanataka lionekane hili ni wazo la Chadema.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Leo nadhani kuna topic muhimu hapa, topic of the day, ila wonderful enough, utamuona Dar es salaam na malaria sugu waki-comment negatively in favor of somebody; hilo gazeti linachonganisha watu huku advantage ikiwa ni kwa wananchi, yes it is obvious that we need a new constitution not the ammended one, pesa ipo na watu watu, V8 kumi tu, tayari katiba!!!! karibuni tuchangie
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Leo nadhani kuna topic muhimu hapa, topic of the day, ila wonderful enough, utamuona Dar es salaam na malaria sugu waki-comment negatively in favor of somebody; hilo gazeti linachonganisha watu huku advantage ikiwa ni kwa wananchi, yes it is obvious that we need a new constitution not the ammended one, pesa ipo na watu wapo, V8 kumi tu, tayari katiba!!!! karibuni tuchangie
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Usitoe hadithi za kubembeleza, mkapa aliunda tume hatimaye akaja kuitukana kuwa imevuka mipaka, mkapa ni CCM na JK ni CCM lao moja, labda tofauti yao ni kwamba mkapa kwa sasa anahusika na usuluhishi wa migogoro ya kisiasa sudan, yawezekana amefungua macho na akili zake kisha kagundua ubaya wa kubakia na katiba ya mkoloni.Huyu katoka katika pazia walilofunikwa CCM kama kina CELINA KOMBANI NA KINA CHILIGATI.

  Muda sasa umewadia wenye uelewa mpana watakubaliana na hata Kikwete anaweza kubadilika pia kwani RAILA ODINGA kawaambia kuwa kama watanzania watahitaji katiba mpya hilo halina ubishi wataipata tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hi 'Dar es Salaam',

  Hivi Malaria Sugu na Batman wako wapi kwenye mjadala kama huu?? Au ndio tuseme wenzetu nao wanatumikia lupango la JF??
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Sasa mpwa wangu SAFARI NI SAFARI!! hio ramani hapo juu hayo maandishi yaliandikwa kwa bahati mbaya au kidhungu changu ndio hicho cha kuunga unga. The country formerly known/called Tanzania?!!! au ndo nchi imeshauzwa mie sijui???
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Ndio hivyo tena TANZANIA siyo tena ile tuliyoienzi zama hizo.....soon tutakuwa kama SOMALIA
   
 14. coby

  coby JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35


  Ukipinga ufisadi na rushwa unaambiwa wewe ni CHADEMA, ukimtuhumu JK kwa uongozi mbovu unaambiwa wewe ni Mdini/Mkabila, na sasa ukionesha umuhimu wa kuwa na katiba mpya unaambiwa wewe ni mfuasi wa Dr. Slaa!!


  Hii ndio TZ nadhani kuna haja ya kuwa na maraisi wawili walioapishwa kama Ivory Coast
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Aaaahhh huko mbali bana, tuombe na tufanye jitihada tusifike huko!!! au unasemaje mpwa? si ndio kazi ya JF kuhamasisha AMANI? Tutumie elimu na uwezo wetu wa fikra wa kuwaondoa hawa wachache, we have magnitude support behind Us, mie nadhani hii ndo nzuri, hata kama wachache watatangulia kwa ajili ya wengi, basi iwe kwa amani! a noble death maybe!!! *ASANTE
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Trust my words....tunapoteza dhana ya UONGOZI na badala yake tunaleta UTAWALA....MTAWALA daima hujifikiria yeye na wanaomzunguka na wala hafikirii anaowatawala...KIONGOZI huangalia namna bora ya kuongoza....MTAWALA hakosoleki na hivyo si rahisi kuwajibika na matendo yake tofauti na KIONGOZI...Tanzania yetu ya kale VIONGOZI walikuwa wanatayarishwa pale Kivukoni na Monduli siku hizi WATAWALA wanapeana nyadhifa tu katika hali ya kulindana...leo hii miezi miwili baada ya uchaguzi Dar es Salaam haina Mkuu wa Mkoa kwa sababu tu Rais hajui ampe nani huo wadhifa
   
 17. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ukipinga sana rushwa utaambiwa wewe Chadema. Sasa tufanye nini?
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukisema KATIBA MPYA na Tume Huru ya Uchaguzi ni lazima utasikia eti mnafikiri hayo yote ni MUARBAINE. Haki ya Mungu ....!!!
   
 19. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimecheka sana baada ya kusoma gazeti hilo linalodai eti limewahoji watu kadhaa ambao wamesema hakuna haja ya katiba mpya. Lakini hao ndio waandishi wa habari tulionao. Tufanyeje? Waandishi wa habari wa aina hii wamechangia sana kuifikisha nchi hapa ilipo kwa sababu hawajui kuchambua mambo na badala yake wanaimba nyimbo za wamiliki wa magazeti yao, na hivyo kuipotosha kabisa jamii. It's very unfortunate!
   
 20. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Wala usishangae mmliki wake ni Ridhiwan na Juma Pinto ndiye aliyewekwa kama Kivuli kuliendesha, sasa unategemea nini?

  Ukionyesha kukubaliana na mabadiliko basi jua kuwa wewe utaitwa wakala wa ...... hata kama hoja ni ya msingi ilimradi haiwavutii wao CCM ya JK na Makamba
   
Loading...