Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,087
- 6,568
Ni swali ambalo mtu kwa haraka unaweza kudhania ni swali ambalo halina logic. Lakini kiuhalisia hili ni swali la msingi ambalo wachumi wanaoishauri serikali walipaswa kujiuliza kabla ya kushauri serikali kutekeleza miradi inayoigharimu serikali yetu matrilioni ya Tsh.
Mradi wa JNHP utakuwa na tija kwa mtanzania ambae mpaka sasa ni mtu anayeishi maisha duni? Mtu ambae anaishi kwa kusaka chakula tu.
Je Sgr itakuwa na manufaa ya kumletea ahueni mtu ambae anaishi kwenye lindi la umaskini? Hana pa kulala pazuri,hana elimu ya kutosha na anakaa kijijini au mjini kwenye slums?
Daraja la Busisi je litawasaidia nini wananchi wa Tanzania? Ambao hata ada za shule, gharama za hospital na malazi ni tabu kuzipata!
Kama nchi ambayo ni masikini, tulihitaji treni ya umeme kwa sasa? Tulihitaji mradi kama JNHP wakati mahitaji yetu kama nchu hayazidi Mw 1000? Je tulihitaji kujenga madaraja makubwa kama Busisi na Oysterbay?
Mtazamo wangu, sisi ni nchi maskini, tulihitaji kuboresha sekta ya afya, elimu na miundombinu sio kwa kiasi kikubwa cha pesa namna hii. Mfano tulitakiwa kujenga SGR kama ya Jirani zetu Kenya ambayo haina gharama kubwa, hakukuwa na umuhimu wa madaraja kama Busisi na Oysterbay. Bora tungeboresha elimu na afya kwa kuzifanya ziwe bure.
Nawakilisha.