Je, Mikakati ya kuimarisha Sekta ya Kilimo na Mifugo imewekwa vizuri katika kuongeza viwanda?

byemelwa

Member
Dec 15, 2014
44
3
Nimeona wana JF, tuchangie mada hii muhimu kuhusu kukua kwa sekta ya viwanda nchini.

Nadhani mtakubaliana na mimi hasa wachumi kuw ili viwanda viweze kufufuliwa na kujengwa vipya na viweze kuwa endelevu sekta kubwa za kuangalia na kuziendeleza ni kilimo na mifugo na katika sekta hizi ndo raw materials zinatoka na kuvilisha viwanda na products zikapelekwa masokoni ndani na nje ya nchi.

Nahapo tutaongeza ajira kwa kila kada ya jamii hii na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja. Sasa tujiulize mikakati ya serikali imewekwa katika sekta hizi mbili kilimo na Mifugo? hasa katika badget hizi zinazowasilishwa? Karibuni tuchangie.
 
Binafsi naona hakuna muunganikano wa kitaasisi kati ya wizara ya viwanda na ile ya Kilimo, mfano mzuri ni kigoma,ilitakiwa WIZARA hizi ziwe na joint effort,ikiwa na time frame,moja,wizara ya Kilimo ivutie ukulima wa mawese na ikibidi watoe mbegu bure pamoja na Dawa za kuua wadudu.
....

Wakati huo huo serikali iwekeze au ifanye public private partnership,na waziri atoe special exemption kwa mashine zote za kiwanda au viwanda,hapa inaingia wizara ya fedha,naamini wachina wana machine za kisasa, ni wakati muafaka pia kuwa na mawese estate,litengwe eneo ambalo muwekezaji atapew alime mawese kisasa ili liwe Shamba la mfano lisipungue hekta 5000 ambalo pilitahudumiadia outgrowers
 
Rais akiamua inawezekana.....tatizo kavutiwa na majipu kasahau masuala mazito ambayo yangeifanya kigoma na taifa libadilike..
pia hata alizeti..tuache maneno,tuitupie jicho la Pili,wachina wanasema wana uhitaji wa mamilioni ya tani za muhogo,watu wamesinzia wizarani na mikate yao hapo wizara ya kilimo,wanashindania uprofesa,Ufugaji wa Samaki kwenye maeneo ba
 
SIDO ndio zero kabisa....hawajielekezi kwenye uhitaji wa Kilimo,haijibu mahitaji ya vijana,wamekaa kama panya mashimoni wanasubiri magufuli akawakurupue wamsomeee taarifa zilizoandikwa Mwaka juzi,nadhani mashine za wajasiliamali hasa wakulima na vikundi vya kinamama zipate ruzuku Maalum na walipie robo au nusu....hii Tanzania ya viwanda
 


Hicho ni kiwanda cha kati wakulima awawezi kuki feed either kwa sababu ya poor network system or poor coordination za wazalishaji halafu ohoo mafuta yanaweza kuwa uhaba wakati kiwanda kinazalisha miezi mitatu kisa kukosekana kwa raw materials; jumlisha na umeme wa TANESCO wenye menejimenti inayoua uchumi kama kuna waahini wa taifa basi wale jamaa number 1; yaani kabisa kuna watu wanaweza shangilia kushushwa kwa bei ya umeme kutokana na madeni yao pamoja na matakwa ya wengi kupewa umeme wa uhakika vitu vinavyotaka investment ya hela.

Hivi hawa jamaa sijui huwa wanapanga mikakati gani huko kesho wanaweza leta watu wawekeze kiwanda cha ngozi halafu ndio waanze kuwatafutia ngozi matokeo yake mtu anazalisha miezi miwili kwa mwaka kutokana na rate ya mashine zake na upatikanaji wa ngozi.

Tatizo wataalamu
 
Tanesco janga.....tatizo la nchi ni mifumo,siku ikiunganishwa na kwa kuangalia vipaumbele,tutasonga mbele,sudan kusini ina shida ya chakula,songea mahindi yanaozea ghalani
 
Kama tumeamuwa kuwekeza kwenye mfano mawese,mpunga,miwa,taasisi zote ziwe hapo mfano kigoma,ili ku-guarantee supply,muwekezaji apewe asilimia kubwa ya kulima raw materials,baadae outgrowers ambao sasa ndio ajira wajazie penye
 
Back
Top Bottom