Je Michezo hii ya Bahati Nasibu ktk Mitandao ya Simu ina ukweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Michezo hii ya Bahati Nasibu ktk Mitandao ya Simu ina ukweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Analyst, May 18, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Amani iwe juu yenu wanajamvi wenzangu?

  Kwa miaka kibao sasa makampuni ya simu za mkononi hapa nchini (pengine hata nje ya nchi) yamekuwa yaki-promote biashara zao kwa michezo mbalimbali ya kubahatisha. Makampuni haya yamewahi kutoa fedha nyingi tu, magari mengi tu, muda wa maongezi na kadhalika. Mengi ya matukio makubwa ya utoaji wa zawadi yamekuwa yakioneshwa kupitia runinga.
  Swali ambalo baadhi ya jamaa zangu wamekuwa wakiuliza na mwishowe hata mimi binafsi kuanza kujiuliza ni je Michezo hii huwa ni ya kweli? Je inafuata taratibu zote za haki kwa washiriki wote au kuna ujanja ujanja?

  Najua michezo hii inaratibiwa na taasisi ya kiserikali (Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu au kitu kama hicho) lakini Tz kwa rushwa tunatisha sasa, hapa pia napata swali; Je Kama Makampuni haya yatafanya janja ili kutoa zawadi kwa upendeleo (kwa watu maalum waliopangwa) au kiusanii (mfano show tupu mbele ya kamera halafu zawadi halisi ziro) msimamizi atasema nini akipewa chake? Na je wenye swali hili hapo juu watajuaje kama ni viini macho?
  Samahani kwa nitakaowakera, lengo langu ni kupata maoni yenu tu.

  Kuna watu wanaotumia fedha nyingi kujaribu kupata bahati na zawadi hizo. Ni imani yangu basi watu hawa wanastahili kuendeshewa mchezo au bahati nasibu hizo kwa haki na kutodanganywa hata kama hawataibuka washindi.

  Tafadhali naomba kuwasilisha.
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,548
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  wizi mtupu1 kwa kuwa nipo nji hii ya sisi wadanganyika nimeliwa ile mbaya hela
  sijaambulia lolote zaidi ya maswali ya kijinga na kukatwa hela zangu kinyemela!kila niamkapo asubuhi! sitaki hata
  kusikia upatu huo kama deci vileeee
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  natumia pesa nyingi lakini sijasikia mahali mtu akishinda,afadhali zichezwe kimkoa
   
 4. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Jamani jamani kama mnazisjkia DEC ndo hizo naungana na mtoa mada hii kwa asilimia mia nimeliwa pesa yangu nyingi sana kwenye prmosheni ya kwanjuka inayoendeshwa na airtel nikiwa na jumla ya point 111280 lakini mwisho wa siku nachezeshwa na mtu aliyecheza mara moja mwenye point 20.Tunadanganywa kuwa wao ndo waliotoa hizo zawadi kumbe ni pesa zetu tunazokatwa kwenye hayo ma dec yao.Niliwapigia juzi nikawaambia umefika wakati waache huo wizi wao waendeshe promotion zao kwa kuwaiga watu wa makampuni ya vinywaji zawadi zao waziweke kwenye vocha ukikwangua ukikutana na kitita hapo poa itakuwa wametoa pesa yao ya halali
   
Loading...