Je, ni salama kutuma michango kwa Tundu Lissu kupitia akaunti ya CRDB? Nahisi wenye mamlaka toka juu wanaweza wakaifrizi

ni wapumvavu tu watamchangia Huyo antpass lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya mwerevu, wacha sisi watanzania tumchangie mtanzania mwenzetu aliyepigwa risasi 38 na 16 kupenya kwenye mwili wake na kupona kwa muujiza wa Mungu pekee.
Acha sisi wajinga tumchangie mtanzania mwenzetu aliyezuiliwa stahiki zake za kimatibabu na nyinyi kwasababu hajafuata utaratibu wa kimatibabu huku daktari wa serikali na wasamalia wema wachache wakimuwahisha hospitali kuokoa maisha yake.
Acha sisi watanzania wapumbavu tumchangie baada ya nyinyi werevu kuzuia mshahara wake akiwa matibabuni huku mkisema kuwa hamjui alipo.
Acha sisi wajinga tumchangie mtanzania mwenzetu nyinyi werevu mnaotaka afe na familia yake ipotee kwakukosa maradhi, pesa ya ada na makazi kwa watoto wale wakitanzania wasiokuwa na hatia.
Mungu akubariki wewe mtanzania mwerevu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mpo serious kabisa kumchangia Huyu MTU? Kweli nimeamini mwenye nacho huongezewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie endeleeni kupanga uovu. Hatumchangii kwa sababu tunazo nyingi, wala hatumchangii kwa sababu tunabariki dhuluma anazofanyiwa na serikali/nchi (maana najua wewe na wenzako hamjui tofauti ya serikali na nchi). Tunamchangia kwasababu ni Mtanzania mwenye uhitaji wa kutengenezewa na serikali. Tunataka watoto wake wasome nae aishi hata baada ya kupotea haki zake za kufanya kazi(kwa risasi) ambayo ingempa kula, haki yake ya matibabu, haki zake kama mbunge. We endelea kupanga uovu mimi na wengine tutamchangia just kama tulivyomchangia matibabu na imewezekana kwa msaada wa Mungu. Kwa sasa ni Bora kukwepa kulipa baadhi ya K.di ambazo MATUMIZI yake ni ya kuwalipa nyie na kina Lipumba, na Konoike na takataka nyingine kama Channel X, nimchangie Lissu mzalendo wa kweli kwa Taifa. NB ni msimamo wangu sio lazima ufanane na wako
 
Ni kweli watoe account ya nje kabisa hapa bongo kwanza wachangaji tunaweza kufuatiliwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona Lissu mwenyewe tayari keshatoa account ya nje?

Ni hii hapa: <www.patreon.com/LISSU>

Kuchangia kwake ni rahisi tu. Ukiingia una-click maneno haya: BECOME A PATRON. Hii website ya patreon ni kama ile ya gofundme. Lakini kwa hii patreon atakuwa analipwa kule Belgium kila mwezi na mtu yoyote anaweza kuchangia hata ukiwa hapa Bongo kupitia credit card.
Kima cha chini ni Dollar 10, lakini bora ingelikuwa Dollar 5, kwani Dollar 10 kwa sisi wengine kwa kila mwezi ni nyingi. Kama yupo kaka Lissu hapa ukumbini basi tunamuomba aweke Dollar 5 tu, ili na sisi wanyonge tupate kumchangia.
Kwahivyo, tumsaidie mwenzetu jamani bila ya kufikiria yeye yupo upande gani wa siasa. Ni Mtanzania mwenzetu na sisi Watanzania tunatabia yakusaidiana. Leo ni yeye, kesho ni sisi. Mtu hajui maradhi yatampata wakati gani au lini atalala kitandani hospitalini.
Tumemsikia LIssu tarehe 9 February kule Marekani na tumemsikia tena kwenye video clip yake ya hivi majuzi kuwa anatuomba Wasamaria Wema tumchangie tena kama tulivyomchangia siku zile za mwanzo. Mtu mzima mwenye akili yake timamu ukimsikia anataka msaada basi ujue anautaka kweli msaada na kwahivyo ni wajibu wetu kumsaidia ndugu yetu na mwenzetu.
Pengine tukimchangia anaweza kubadilisha mawazo yake na akarejea nyumbani (CCM) kama mzee wetu Lowassa!
 
Kama hawakuZuia kwa ruge, basi kwa lisu hawataweza na wakifanya hivyo nyeti Zao Zitazidi kuonekana ukweni, kwani watakuwa wanapiga tiktak huku wamevaa msuli ilihali hawajavaa boksa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe hawa nyoka wa kijani hawajali wanaweza. Double standard ni kawaida. Mfano ni mingi tu. Mikutano kwao ruksa tena hadharani, lakini wengine wanapigwa mabomu mpaka mikutano ya ndani,
Vyeti feki wengine wanatimuliwa wengine wanaitwa wachapa kazi,
Kimara walibomolewa mita Mia na zaidi bila fidia kisa mbunge ni upande wa pili lkn Mwanza wakaambiwa hao ni wapigakura walibomolewe, Ukitukana upande wa pili ruksa mfano Msiba lkn ukijibu kazi unayo. Kwa haya tu ni mfano kuwa hawashindwi
 
Kwa scenario hii akijaribu, atazidi kujionesha kwamba ni suspect.no1 behind lisu attempted assassination

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni mihemko tu.....ngoja mda usogee mambo yatarud kwenye equilibrium...
 
Kwa scenario hii akijaribu, atazidi kujionesha kwamba ni suspect.no1 behind lisu attempted assassination

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kwa sasa ni ipi inamtoa kuwa suspect no 1??
1. Hajawahi kutoa pole (binafsi sijasikia popote kwenye TV au gazetini au live)
2. Aliamuru anyimwe matibabu eti kwa kukiuka kupitia Mhimbili wakati wote tunajua haikuwa yeye anaeamua cha kufanya
3. No suspect to date
4. Ulinzi na CCTV kutolewa.
5. Kupigwa marufuku kumwombea tu !!!!
6. Marufuku T-shirt
7. Marufuku uchunguzi huru
8. Kauli za spika na yeye au yeyote from bunge kwenda kumwona.
9. Kutaka akamatwe akiwa bado mgonjwa
10. Kufutiwa posho zote na mishahara yake.
11. Amehoji issue ya MO ( japo napo suspect ni wao) lkn issue ya Lissu nayo kwa mtizamo wangu ni sensitive sawa au kuliko ya MO
12. Nguvu inayotumika na viongozi wote wa serikali kuzima issue ya Lissu na kutaka kutuaminisha kuwa ni adui wa Taifa.
KWANGU SUSPECT NO 1 hao
 
Unaweza kuwa sahihi au kinyume chake vilevile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushapigwa pesa wewe tulia hivyo hivyo nyu.mbu wengine wapigwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuliza mshono. Kuna mahali umeshikwa mikono ukalazimishwa uchangie? Ukiona vipi mchangie magufuli sisi tusio na roho za shetani tutamchangia Mtanzania mwenzetu anayefanyiwa dhuluma na serikali yetu

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Back
Top Bottom