Je, miaka 7 bado ni umri sahihi kumuanzisha mtoto shule ya msingi?

Kumamsha mtoto wa miaka 3 SAA 12 ili aende shule ni kumtesa mtoto.

Mtoto anatakiwa aanze shule na miaka kuanzia 6-7 darasa la kwanza

Hakuna faida kumuwahisha
Faida zipo za kumuwahisha mojawapo na muhimu zaidi ni ukuaji wa watoto wa siku hizi.
Akianza na 5 by 12 amemalizana na primary. Anakua akiwa secondary. Sasa unataka mtoto akue akiwa bado msingi? Hatari.
hahahahaaa
mkuu anakula madini light weight tu.
 
Bado wako kiuononi? Sasa mwanao awe na 7 anos halafu yuko darasa moja wenzie wote wako na 5 anos hapo umemaidia kweli?look at it this way. Wewe kubwa halafu uko na wadogo na wote mnafundishwa aame thing halafu wewe huelewi, morali ya kusoma utakua nayo? Soma alama za nyakati.
Noted!
 
mtoto wangu alianza chekechea na miaka2 na miez 9 na ameanza la kwanza na miaka5 na miez8
Nilipata mtoto wakati nipo kidato cha 4, aliofikisha umri wa miaka 5 alianza chekechèa, now hajaanza mwaka 8 ( mpaka mwezi 8) lakini yupo darasa la pili na anapeta vizuri sana. Namshukuru Mungu kwa kweli.
 
issue serikalini ni resources za kusomesha vijitoto vidogo, wale wa miaka 7 hata 100 wanakaa darasani
 
Nawashangaaga sana wanaosemaga watoto wao wako vizuri kichwani, usimguarantee mtoto yuko vizuri darasa la 1 hadi la 5, akili ya mtoto inapimwa kuanzia la 6.

japo nimewaona wengi sana waliokua wanakimbiza shule ya msingi lakini wanapitwa sekondari na waliowakimbiza msingi
 
Tatizo wabongo wanaona misifa kumpeleka mtoto mdogo sana shule(miaka 2 au 3).Huo ni umri wa mtoto kupata makezi full ya wazazi ikiwemo kudeka si muda wa kumpa shuruba,Unataka akamdekee mwalimu??atakula mbata kila siku mwisho wa siku ooooh amekuwa nunda!!
Kwa mjini, hayo malezi ya wazazi anayapata saa ngapi?! Hata kwa mama ambae hajaariwa, huo muda ambao unasema mtoto angekuwa anapata malezi yake, mama atakuwa anatembeza matembele mitaaani!!

Issue sio kuona sifa bali ya nini zee zima unaliacha nyumbani linacheza badala ya kulipeleka shule eti unasubiri afikishe miaka 7?
 
Kwann kwa wenzetu watoto wanaanza shule wakiwa na umri mdogo na bado wanafanikiwa kielemu?
Wakati tunajiuliza hao wenzetu ni kina nani lakini pia tuangalie mazingira ya mfumo wa maisha yao ukoje pia, je unafanana na sie ! Nadhani ulivyosema wenzetu unamaanisha nchi zilizoendelea? au wenzetu wa Africa yaani kusini mwa jangwa la sahara
 
Kwa mjini, hayo malezi ya wazazi anayapata saa ngapi?! Hata kwa mama ambae hajaariwa, huo muda ambao unasema mtoto angekuwa anapata malezi yake, mama atakuwa anatembeza matembele mitaaani!!

Issue sio kuona sifa bali ya nini zee zima unaliacha nyumbani linacheza badala ya kulipeleka shule eti unasubiri afikishe miaka 7?
Mkuu michezo ni afya mkuu pia ni sehemu ya mchakato wa ukuuaji kwani hata asipokwenda shule muda huo inakuwa kama sehemu ya makuzi na kufahamu mazingira yanayomzunguuka pia
 
Ubora wa elimu unashuka siku hadi siku kwa kuwa watoto wanaanza shule wakiwa wadogo, wasio na upeo/ uwezo wa kuelewa mambo magumu. Mimi watoto wangu wote wataanza shule na miaka saba. Sitaki mtoto amalize mbumbumbu. Nataka aelewe kile anachokisoma.

Daaa sijakuelewa. Bint yangu ameanza na miaka mitatu, she is super genius anaelewa mambo mpaka anatisha. Sasa ana miaka mitano na atanza grade one this September. Hajui chochote zaidi ya masomo. Anzisheni watoto wakiwa wadogo waanze kujifunzo nyimbo za namba na za herufi badala ya nyimbo za mapenzi.
 
Nawashangaaga sana wanaosemaga watoto wao wako vizuri kichwani, usimguarantee mtoto yuko vizuri darasa la 1 hadi la 5, akili ya mtoto inapimwa kuanzia la 6.

japo nimewaona wengi sana waliokua wanakimbiza shule ya msingi lakini wanapitwa sekondari na waliowakimbiza msingi
Tena sio la 6 tu maana hata kama yuo vizuri bado kuna kipindi kingine cha changamoto cha elimu ya secondary unakuta mtu amepoteza focus kabisa
 
Mkuu michezo ni afya mkuu pia ni sehemu ya mchakato wa ukuuaji kwani hata asipokwenda shule muda huo inakuwa kama sehemu ya makuzi na kufahamu mazingira yanayomzunguuka pia
Mkuu wangu hivi kuna mahali kulikojaa vurugu za michezo/kucheza kwa watoto kama shuleni?! Au umesomea shule za kishua? Tulizosomea sie wengine ni full kucheza... darasani, kucheza... ukitoka nje, kucheza! Ukisikia kengele ya kurudi home ndo balaa kwa kwenda mbele!!

Sasa kucheza kupi unakozungumzia?!

Sema mnataka watoto wenu wawe wababe darasani... manake hicho nakifahamu kwa watoto wenye umri mkubwa wakichanganyika na watoto waliowazidi umri!
 
Mimi nadhani umri wa kuanza shule unafaa uwe mdogo ili amalize shule ukiwa bado na uwezo wa kumlea. Akianza akiwa mkubwa kama enzi zetu mtu anaanza la kwanza akiwa na miaka 12 inakuwa vigumu kumbana
 
Tena sio la 6 tu maana hata kama yuo vizuri bado kuna kipindi kingine cha changamoto cha elimu ya secondary unakuta mtu amepoteza focus kabisa
Akichelewa kuanza ndo pale unakuta sekondari anapoteza focus! Unakuta mtoto kamaliza darasa la 7 akiwa 14; akifika 16 ndo kwanza yupo Form II... kama ni mtoto wa kike, hapo hisia hazikamatiki!

Kichwani shule ndogo!

Maumbile yashaanza kuleta balaa lake!

Ukichanganya yote hayo, ni tafurani tupu!

In contrary, akianza mapema unakuta hiyo 16 yupo busy na mitihani! Anafika 17 tayari yupo Form V, angalau kichwani shule ipo ya kuweza ku-take care of her/himself! Na watoto wa aina hii, kwa wale wenye tabia njema unakuta wengi ngono wanaenda kuanzia chuoni!
 
Ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto analelewa vizuri.

Majukumu yamesababusha tunapata kizazi cha ajabu maana watoto twawaona jumapili asubuhi pekee.
Anaondoka ukiwa umelala, unarudi akiwa amelala
 
Back
Top Bottom