Je mi kweli JK ana nia ya kusafisha nchi?

Nyangumi

JF-Expert Member
Jan 4, 2007
507
17
Nimepata hii e-mail nadhani inatoka bungeni nimeona niipost hapa.
Mimi nasema,kama kweli atafanya anachokizungumza.Atanipa imani ila nitafanya hivyo tu baada kuona Watu wote waliohusishawa na kashfa zooote kubwa wanakamatwa,wanafilisiwa na kufikishwa mahakamani,bila kujali vyeo au majina yao.


Ndugu Spika, ndugu wabunge, ndugu wananchi.
Leo asubuhi nimepokea barua ya Waziri Mkuu ya kujiuzulu kwa masikitiko makubwa kwani tumefanya naye kazi muda mrefu na nilitegemea atumie vipaji vyake vingi kuongoza serikali yangu kwa muda mrefu. Wengi mtakumbuka enzi za Boyz2Men. Nasikitika sana kwa hatua taifa letu lilipofikia.

Aidha, nimepokea na kusoma ripoti ya Dr Mwakyembe kwa masikitiko maradufu ya yale yaliyonipata kwa barua ya ndugu Lowassa. Sina mengi ya kusema, ila jioni hii naomba wananchi mnipe ridhaa yenu kuanza mchakato wa kina wa kuondoa taifa hili kwenye dimbwi la ufisadi, ubadhirifu, wizi, utawala wa ki-imla, na kutojali matakwa na malalamiko ya wananchi.

Awali ya yote nikiri kwamba kwa miaka yote niliyokuwa kwenye shughuli na uongozi wa uma, lazma kuna nyakati chache ambazo nami niliwahi kuterereka kimaadili. Pale matendo yangu hayakukidhi mategemeo ya wananchi naomba msamaha wao. Hata hivyo inafika wakati nchi kusafishwa kwa manufaa ya umma. Bila hivyo nchi yetu itasambaratika kama majirani zetu na nchi nyingine kama USSR, Yugoslavia nk. Nimenuia kuiokoa nchi yetu toka kwenye hatma hii, na kwa hili nitaomba na kuhitaji msaada wenu. Hatua za awali.

Kwanza, nakataa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu kama hakuandamani na kujiuzulu kwa baraza lote la Mawaziri ili nianze upya kuomba kibali cha kuwaongoza wananchi bila fununu za ufisadi na bila dharau kwa serikali yao.

Pili, natangaza kugandisha (to freeze) akaunti zote za mali za wale waliohusika na shutuma za Richmond, na BoT, pamoja na kushika rehani mali zao zote zisizohamishika kwa nia ya kurudishia serikali mali yoote ambayo inaweza kuwa iliibiwa na washutumiwa. Ili wasife njaa serikali itaendelea kuwalipa nusu mshahara hadi uchunguzi au mashtaka kumalizika.

Tatu, nawahimiza viongozi wote waliojihusisha na ufisadi wowote wa kimsingi kama kwenye mikataba ya madini, Netgroup Solutions, Uuzaji wa Mashirika na Raslimali za Umma, Ununuzi wa rada na ndege ya Rais, Ununuzi wa vifaa vya Jeshi, Mikataba na TANESCO kama IPTL, Kiwira, nk, wakiri kwangu kimaandishi kushiriki kwao na kuorodhesha mali walizopata kutokana na matendo hayo. Wakifanya hivyo sitawachukulia hatua za kisheria ila nitawasimamisha kazi ya umma na kurudisha mali ya wananchi panapohusika.

Wasiojitokeza kwa hiari naagiza vyombo vyote vya uchunguzi vya dola kufuatilia kwa undani na waletwe mbele ya sheria mara moja.

Ndugu wananchi, hii vita dhidi ya wabadhirifu itahitaji ushirikiano wenu na naomba mniunge mkono kwa kila namna.

Nimeagiza vyombo husika kuhakikisha watuhumiwa hawawezi kutoroka au kutorosha mali hadi uchunguzi umalizike. Aidha nimeagiza vyombo vya dola viwe macho kudhibiti wakorofi wachache watakojaribu kuleta ghasia.

Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni.
 
Back
Top Bottom