Je mh.mwanri ana matatizo gani na utawala wa sasa wa Jk?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mh.mwanri ana matatizo gani na utawala wa sasa wa Jk??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajunju, May 8, 2012.

 1. k

  kajunju JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Nimefuatilia uteuzi wa mawaziri wapya,lakini pia nimefuatilia mawaizri wa mh Jk ambao amekuwa anawateua kushika wizara mbali mbali tangu awe rais wa inchi hii.Je mh mwanri ana tatizo gani na mh jk kuhusu kuteuliwa kuwa waziri kamili??nakumbuka alianza kuwa katibu mwenezi wa ccm baadae akawa naibu waziri tamisemi enzi za pinda hadi sasa.Nimekuwa nafuatilia jinsi anavyojibu maswali bungeni,amekuwa anaonekana kuwa na upeo mkubwa kumzidi hata bosi wake aliyepita mh mkuchika kwa kuielewa wizara na kujibu maswali kwa ufasaha pia.licha ya wizara yake kukumbwa na kasheshe la ufisadi, yeye kama yeye sijamsikia na tuhuma yoyote chafu iwe ya kiofisi au binafsi kulinganisha na mh. malima ambaye wizara yake imekuwa na matukio mengi ya ufisadi na yeye binafsi kujiusisha na mambo ya hovyo( ref ziara yake ya morogoro,mara bunduki,pesa,viroba vya pombe nk).Nimejiuliza maswali haya ambayo sijapata majibu yake lakini ninatumaini kuna anayeweza kujua kilichojificha chini ya pazia la mh mwanri.
  • je ni mvivu kiasi kwamba akiongezewa majukumu hawezi kuyatekeleza?
  • Elimu yake haitoshi kuweza kufanya kazi za waziri kamili?
  • Ni muongo kiasi kwamba akiwa ndani ya baraza la mawairi atatoa siri za baraza hilo??
  • Siyo smart kwenye muonekano,mavazi na ni mlevi??
  • Ni mpenda totozi kiasi kwamba atatoa siri za mabosi wake zianze kuzagaa mitaani??
  • Ni mbishi kiasi kwamba analoambiwa hatekelezi hivyo ni bora abaki anasimamiwa??
  • Siyo mbunifu kiasi kwamba ata akipewa uwaziri usio na wizara maalumu hatoweza ku-fit?
  Ninajua mtanisaidia kujibu maswali haya ili tuone uzuri wake na uzaifu wake huko wapi.
  Nawasilisha!
   
 2. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nchi hii inahitaji watu rafu kama Mwanri, abembelezi mtu.
   
 3. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hakati na harudishi chenji na cha juu kwa bosi wake.
   
 4. k

  kajunju JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  kanga ina maana hapandishwi cheo kwa kuwa hatoi 10% kwa mabosi wake? je inawezekana hali rushwa hivyo he never mind taking bribes?nauliza hivi kwa sababu kama haendekezi huu ujinga wa kupeana pesa then atakuwa mzuri kwenye utendaji na anaamini anachokitenda
   
 5. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,129
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Namshukuru mleta mada kwa maoni yake kwa sababu hata mimi sikupendezwa Mh Mwanri kuachwa nje ya uteuzi. Mh Mwanri ni mchapakazi mzuri na amejizolea uzoefu mkubwa wa utendaji kazi wa halmashauri zetu za wilaya. Alikwenda Muleba akajionea uchakachuaji wa injini ya boti la halmashauri, pia alikwenda wilaya ya makete akashuhudia nyumba za wafanyakazi wa halmashauri zilizojengwa chini ya kiwango.Sifa nyingine nzuri aliyo nayo Mwanri ni diplomasia ya kujibu maswali bungeni. Kwa hayo yote angefaa kuteuliwa waziri TAMISEMI kwa sababu anaufahamu utendaji wa halmashauri za wilaya. Sijaona mpaka sasa sababu ya mama Hawa Ghasia kupewa uwaziri TAMISEMI.
  Ni nini kimemyima Mwanri kupandishwa cheo na kuwa full waziri? Mwenye mwanga atufunulie
   
 6. j

  julisa JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata nadhani mh mwanri angefaa hata uwaziri mkuu..a no nonsense man
   
 7. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  'Shhhhhhh!!!! naogopa kuchema, changanya na zako utapata jibu'
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwanri Aggrey siyo mzuri ki hivyo kama unavyomsikia kwenye TV. Wanaomjua kuanzia akiwa DC wanasema ni mfu wa kelele kelele tu na kulazimisha mambo. Alifikiri akifanya kazi na vyombo vya habari angepata promo lakini sasa nafikiri ameshajua kuwa mambo yake hayana impact bali ni ksele tu.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kwa utawala huu wa sasa hiyo wizara inamfaa mzee wa misifa John Pombe Magufuli!
   
 10. M

  Mtokambali Senior Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Bora wewe utupe upande wa pili wa shilingi! Utendaji haupimwi kwa matukio machache ya tv.
   
 11. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Bnafsi nlikuwa namkubali Huyu Mhe.ny hii ndo Sirikali bwana.wanampika awe mkuu wa Mkoa badae
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Namjua toka enzi hizo. . kwa kazi zake na binafsi maana ni mtu wa nyumbani. Siku zote amekua akijitahidi, japo sifagilii sana yeye kuwa magamba ila ndio sababu pekee ya baadhi ya watu wa huku kwetu kubaki magamba, kwasababu wanajua chama sicho kinachoharibu watu ila watu ndio wanaoharibu chama.
   
 13. papason

  papason JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Inasemekana yuko kwenye kambi ya EL kimtindo
   
Loading...