Je, Mgao wa umeme ndio umeisha?

The Finest

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
21,607
6,071
Leo ni takribani siku ya nne sasa umeme haujakatika sasa najiuliza mgao umeisha au kuna jambo jingine.
 
haujaisha....umepungua tu
mitambo imepata mafuta,mafuta yakiisha,unarudi.....
 
haujaisha....umepungua tu
mitambo imepata mafuta,mafuta yakiisha,unarudi.....
Itakuwa ya IPTL si ndio? Maana nasikia ile ya Symbion inatumia mafuta malaini sijui ndio yapi hayo, halafu hadi yajaribiwe kwanza
 
weeee thubutu yako, mgao siku hizi ni wiki kwa wiki, subiri wiki hii ni zamu yako labda wiki ijayo ndio tutakua nao sie, nyie nanyi mtabaki gizani kwa wiki nzima.....
 
weeee thubutu yako, mgao siku hizi ni wiki kwa wiki, subiri wiki hii ni zamu yako labda wiki ijayo ndio tutakua nao sie, nyie nanyi mtabaki gizani kwa wiki nzima.....
Elli yaani mgao umehama kutoka kwa siku kwenda kwa wiki
 
Teh teh teh....bongo hiyo bana. Eti nayo ni nchi ya wenye akili. Wenye akili lakini hawawezi kutatua matatizo madogo madogo kama umeme, maji, mivumbi, na mitope.

Ama kweli wana akili!!!!
 
Maji yameongezeka katika mabwawa ya kuzalisha Umeme kwa sababu ya hizi mvua zinazoendelea kunyesha takribani nchi nzima.
 
Mvua zanyesha uko uko Pwani nasikia iringa,mbeya bado na ndiko Mtera liliko
 
Umeme kuwaka mfulilizo kwa wiki nzima Tanzania ni muujiza wa kutolea sadaka ya shukrani!huo ni umeme tu,bado maji!
Ndo maana vijana waliokata tamaa wanatami wangekuwa watumwa Ulaya na sio huru Tanzania
Hii nio hatari kubwa kwa taifa.
 
Itakuwa ya IPTL si ndio? Maana nasikia ile ya Symbion inatumia mafuta malaini sijui ndio yapi hayo, halafu hadi yajaribiwe kwanza

IPTL bado haijawashwa...inatumia mafuta mazito HFO, sidhani hata kama yameagizwa.
Yawezekana mgawo kwako umepungua kwa sababu...huenda unaishi maeneo ya Kinondoni, hasa maeneo ya Sinza na majirani zake, yaani kaskazini mashariki mwa jiji.

Aggreko wamewasha mitambo yao na sasa wanazalisha takribani 50MW japo bado wapo kwenye majaribio....umeme huu hauingii kwenye gridi bali unaingizwa moja kwa moja kwenye 33kV feeder ya mkoa wa Kinondoni...yawezekana ndo sababu mmepata ahueni huko kwenu, siye wengine bado tunaumia.
 
Wananunua support ya wabongo kwa muda. Tukipewa kaumeme kwa tusiku tuwili sisi kama kawaida yetu tunasahau yote yaliyopita
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom