Je, mfumo wa vyama vyingi Tanzania ni kwa ajili ya kupata msaada kutoka kwa wafadhili?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Je, mfumo wa vyama vyingi vya siasa nchini tanzania ni kwa ajili ya kuapata misaada kutoka kwa wafadhili?

Je, mfumo huu wa vyama vyingi vya siasa umepokelewaje na viongozi wa serikali hasa Serikali hii ya awamu ya 5?

Mkuu wetu wa majeshi je ni muumini wa demokrasia ya mfumo wa vyama vyingi vya siasa?

Matendo yake yakoje kwenye mfumo wa vyama vyingi vya siasa?

Kwanini watanzania ambao wanasapoti wanaonekana vyama vya upinzania kwanini wanaonekana kama maadui wa taifa?

Kwanini wanaonekana kama vibaraka wa mabeberu?

Je,ni kweli wanaosapoti vyama vya upinzani ni vibaraka wa mabeberu?Kama ni kweli kwanini tusifute huu mfumo wa vyama vyingi vya siasa?

Je, tulipopata uhuru tulijaribu kujenga mfumo wa demokrasia wa chama kimoja tukashindwa kutokana na majaribio ya mapinduzi ya kijeshi ndio maana miaka 1992 tukaamua kujenga mfumo wa demokrasia ya vyama vyingi vya siasa?

Je, katiba zetu zilibadilika kutoka kwenye mfumo wa demkrasia ya mfumo wa chama kimoja,kuja katika mfumo wa demkrasia vyama vyingi vya siasa?

Je, katiba yetu na Sheria zetu zinaruhusu mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa?

Je, demokrasia katika nchi za Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla inaenda mbele au inarudi nyuma?

Tutafakari tuchukue hatua
 
Yes. Ndio maana yake, tukiangalia historia ya mfumo wa vyama vingi ktk nchi nyingi za kiafrika ni kwamba walilazimishwa kuurejesha huu mfumo na wazungu mwanzoni mwa miaka ya tisini kufuatia kusambaratika kwa iliyokufa The Soviet Bloc.

Ili uwe na guarantee ya kuendelea kupata misaada ilikuwa ni lazima mkubali kuurejasha huu mfumo. Nchi kama Libya ambayo kimsingi ilikuwa haitegemei kutembeza bakuli haikuruhusu huu mfumo.

Hii inajidhihirisha wazi namna serikali nyingi za kiafrika zinavyozi- treat vyama vya upinzani kwani ktk nchi fulani fulani za kiafrika ni faraja zaidi kuwa fisadi au hata jambazi kuliko kujinasibisha kama mpinzani. Hizi nchi za Afrika ni hovyo sana nafuu wakoloni wasingeondoka.
 
Chanzo kikuu ni ubinafsi wa mwafrika yupo Kwa ajili ya tumbo Na si Kwa ajili ya jamii
 
Back
Top Bottom