Je mfano huu wa Mwalimu J. K. Nyerere umekuwa mfano halisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mfano huu wa Mwalimu J. K. Nyerere umekuwa mfano halisi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 25, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wan chi, maana wana sifa mbili muhimu: kwanza, wana uwezo wa kutawala, na pili, hawapendi kutawala. Kwa hiyo, Jamhuri ya Plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikisha, atafurahi sana kurudiashughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazipenda. Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala, na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala (Nyerere, 1993, p.8)
  Reference
  Nyerere, Julius K. (1993). Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Harare: Zimbabwe Publishing House

   
 2. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ukiangalia kwa undani Kauli za baba wa taifa zilizo nyingi huwa zinamsema JK tu, jamaa hajakaa pake huyu. Na alishawahi kutamkiwa nadhani kifo cha yule mzee alikisherehekea maana urais angeusikia kwenye bomba tu, he is running on empty
   
 3. e

  ejogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii nukuu!
   
Loading...