Uchaguzi 2020 Je, Membe katumwa na viongozi wandamizi wa awamu zilizopita au katumwa na nani?

Huu ni mwanzo tu wa pambano kati ya ccm mpya na ccm ya zamani. Jiulize ni kwanini Membe anajiamini mno kuliko hata aliyeko Madarakani yaani Magu??

Na pia jiulize kwanini hivi sasa ccm inahaha kupita miaka yote?? Kwanini ccm imewatuma Wazee kwenda kumuomba Membe asichukue form kupitia chama chochote cha siasa eti asubiri hadi 2025??
Kwa ushahidi up Mkuu. Bm ndo anahaha JP anafanya yake.
 
Yule mzee ameandaliwa na CCM akafanye kitu inaitwa divide and rule kwa wapinzani kama alivyofanya lowasa, mark my words
Bongo zenu ndogo tu kuchekecha mambo. Kama kweli unasema Lowassa alitumwa kugawa upinzani basi unatakiwa kuonewa huruma na hujui dunia inakoelekea. Lowassa alikamia hasa kupata urais na alihama baada ya kukataliwa CCM na kuja upinzania alikuja akidhamiria hasa. Na hata CCM amerudi kwa sababu tu ya afya yake la sivyo sasa hivi bado angekuwa ndiye mgombea tena wa Upinzani na pengine wangeungana na Membe.
 
Kwanini mnadhani ni serikali tu pekee yake ndio inajua "michezo"?

Mnaipa serikali na walio madarakani uwezo wa "kimungu"!

Watu walioko serikalini ni watu wenye IQ ndogo sana...sio kiivyo kama mnavyotaka kutuaminisha!

Maana tumesoma nao mashuleni,ni watu wajinga mno....they are not that capable bwana!
Mfumo. Ni wakawaida wakiwa nje ya mfumo, wakiwa ndani si wa kawaida. Kama ww ni shabiki wa mpira unaelewa tofauti ya timu nzuri isiyo na mastaa na timu yenye mastaa.
 
Kila awamu ilifanya mema na mabaya. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa katika awamu yake yako mema amefanya na yako mabaya amefanya pia. Akashauri kuwa unachukua mema unayandeleza mabaya unayaacha.

Sisi wananchi tumeshuhudia mema na mabaya ya kifanywa na awamu zote. Lakini ziko awamu zilibugi kupita kawaida. Na moja ya awamu ilibugi sana ni awamu aliyohudumu mh Membe akiwa waziri. Rushwa, ufisadi, Wanainchi kunyanyaswa wakienda ifisi ifisi za umma ilikuwa kawaida sana kiasi cha CCH kuitwa chukua chako mapema.ukisema wewe ni CCM ulionekana jambazi Fulani.

Yapo mengi yalikuwa yanatia hasira kiasi cha kwamba mpaka nchi majirani walituona sisi watanzania kama hamnazo kabisa kusema kuwa ni nchi maskini. Mfano ni rais wa Rwanda alithiriki kusema kuwa akipewa bandari ya Dar es salaam anaweza kuilisha Tanzania kama sio Afrika nzima.

Katika hoja za Mh Membe ni kwamba eti katika awamu zote NNE rais mpya anaheshimu watu aliyowakuta na anaongezea wa kwake kidogo. Kilichomuudhi eti kwa nini anasema kulikuwa na watu wa hovyo na mambo ya hovyo na nchi ilifanywa kuwa shamba la bibi.

Swali ni je anayoyasema Mh rais ni uongo? Makinikia yalibwebwa,twiga walibwebwa,bandarini mita feki,IPTL capacity charges za hovyo, Richmond,watu kutolipa kodi,vyeti feki,wafanyakazi hewa, miradi mingi kubinafsishwa hovyo nk. Sasa kama kulikuwa na mambo ya namna hii na yanafanywa na watu waliyoko serikalini na watu wa awamu zilizopita ulitaka mh rais afanyaje kwa mfano?

Unasema eti hamna Uhuru wa kujieleza mie sijaelewa ulitaka wapewe Uhuru was kutukana watu?wanasiasa wa vyama vya upinzani kuandamanisha watu kila kikicha?

Swali ni je kwa sababu maovu ya awamu zilizopita yaliwekwa bayana,na unajua utaratibu wa CCM rais aliyeko madarakani anaongoza kwa miaka kumi ,ni watu waliyohudumu awamu hizo ndiyo waliyokutuma kwamba umuondoe JPM iliwasiendeelee kuabishwa kwa kutokufanya vizuri katika uongozi wao? Na je ni wafanyabiashara wasiyolipa kodi na kuhujumu uchumi wamekutuma? Ni wenye vyeti feti na watumishi hewa wamekutuma? Ni nchi za mbali wamekutuma?kinachokufanya usisubiri hadi 2025 ni nini?umetabiriwa na mizimu kwamba lazima uwe rais before 2025?
Ametumwa na wezi na wasanii wenzake maana kwa mwendo huu watakufa maana hakuna pa kuiba kwa Sasa! Hawawezi kusubiri maana Kama Xi Jinping wetu tunaye, matumaini ya kurudi ulingo I kutuibia hivi karibuni yamepukutika! Na sisi tunajiandaa kumlazimisha aongeze 10 mwingine...matumbo yanawavuluga, lazima wafanye vurugu!
 
Kwani leo hii ccm imebadilika kitu gani cha kuisifia?
Kila awamu ilifanya mema na mabaya. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa katika awamu yake yako mema amefanya na yako mabaya amefanya pia. Akashauri kuwa unachukua mema unayandeleza mabaya unayaacha.

Sisi wananchi tumeshuhudia mema na mabaya ya kifanywa na awamu zote. Lakini ziko awamu zilibugi kupita kawaida. Na moja ya awamu ilibugi sana ni awamu aliyohudumu mh Membe akiwa waziri. Rushwa, ufisadi, Wanainchi kunyanyaswa wakienda ifisi ifisi za umma ilikuwa kawaida sana kiasi cha CCH kuitwa chukua chako mapema.ukisema wewe ni CCM ulionekana jambazi Fulani.

Yapo mengi yalikuwa yanatia hasira kiasi cha kwamba mpaka nchi majirani walituona sisi watanzania kama hamnazo kabisa kusema kuwa ni nchi maskini. Mfano ni rais wa Rwanda alithiriki kusema kuwa akipewa bandari ya Dar es salaam anaweza kuilisha Tanzania kama sio Afrika nzima.

Katika hoja za Mh Membe ni kwamba eti katika awamu zote NNE rais mpya anaheshimu watu aliyowakuta na anaongezea wa kwake kidogo. Kilichomuudhi eti kwa nini anasema kulikuwa na watu wa hovyo na mambo ya hovyo na nchi ilifanywa kuwa shamba la bibi.

Swali ni je anayoyasema Mh rais ni uongo? Makinikia yalibwebwa,twiga walibwebwa,bandarini mita feki,IPTL capacity charges za hovyo, Richmond,watu kutolipa kodi,vyeti feki,wafanyakazi hewa, miradi mingi kubinafsishwa hovyo nk. Sasa kama kulikuwa na mambo ya namna hii na yanafanywa na watu waliyoko serikalini na watu wa awamu zilizopita ulitaka mh rais afanyaje kwa mfano?

Unasema eti hamna Uhuru wa kujieleza mie sijaelewa ulitaka wapewe Uhuru was kutukana watu?wanasiasa wa vyama vya upinzani kuandamanisha watu kila kikicha?

Swali ni je kwa sababu maovu ya awamu zilizopita yaliwekwa bayana,na unajua utaratibu wa CCM rais aliyeko madarakani anaongoza kwa miaka kumi ,ni watu waliyohudumu awamu hizo ndiyo waliyokutuma kwamba umuondoe JPM iliwasiendeelee kuabishwa kwa kutokufanya vizuri katika uongozi wao? Na je ni wafanyabiashara wasiyolipa kodi na kuhujumu uchumi wamekutuma? Ni wenye vyeti feti na watumishi hewa wamekutuma? Ni nchi za mbali wamekutuma?kinachokufanya usisubiri hadi 2025 ni nini?umetabiriwa na mizimu kwamba lazima uwe rais before 2025?
 
Zitto nadhani kuna kitu anakifahamu siyo bure
Membe, Ccm wote lao moja tu wanajuwa wanachokifanya ndio maana namshangaa sana Zitto kutaka kuingia kwenye mtego yaani TISS tena iliyochini ya ccm aje upinzani kwa usalama? siwezi kumuamini mpaka naenda kaburini!
 
Jenerali Ulimwengu - Kila ajaye ana jipya, hatuendi kokote

source
: Jenerali Online

Katika makala yangu ya mwisho, wiki mbili zilizopita, nilionyesha jinsi ambavyo wakuu waliostaafu wanvyolalamikia mambo ambayo wao wenyewe waliyasababisha walipokuwa madarakani kwa kutotaka kusikiliza kilichokuwa kikisemwa na wengine, wakidhani kwamba maoni ya mkuu ni bora kuliko ya wale wasio na ukuu.

Marais wastaafu wawili walikuwa wametoa maoni yao kuhusu mporomoko wa viwango vya elimu, wakisema kwamba hili ni janga la taifa. Ni kweli kwamba elimu yetu imeporomoka kwa kiasi cha kutisha, kama ambavyo tafiti zetu zinavyoonyesha. Lakini hao wawili walikuwa madarakani wakati fulani, na kila aliyejaribu kuwaambia hayo ambayo wanayasema leo walimuona kama mwendawazimu, punguani, muongo au ‘mvivu wa kufikiri.’

Nachelea kufikiri kwamba mkuu tuliye naye sasa, kwa kufuata mfano wao, anaweza kuwaita hao watangulizi wake majina hayo. Natumai hatofanya hivyo bali atajifunza kutokana na kasoro zao ili naye asije akaanza kulalama baada ya kutoka madarakani kuhusu mambo ambayo alikuwa na uwezo nayo alipokuwa madarakani lakini akawabeza waliotaka kumshauri.

Tukumbushane akili: Serikali ina wajibu wa kutawala, na katika shughuli hiyo, ni serikali pekee yenye wajibu huo. Hakuna chombo kingine chenye wajibu wa, au haki ya, kutawala isipokuwa serikali. Minajili ya kufanya kazi hiyo, serikali imepewa vyombo vya utekelezaji, kama vile utawala wa raia, pamoja na asasi za kimabavu, kama vile majeshi, idara za upelelezi na ujasusi, vitengo vya makachero na wachunguzi.

Lakini, pamoja na nguvu zote hizo ilizopewa serikali kwa ukiritimba, haiwezekani serikali yo yote ikatamba kwamba ina ukiritimba wa akli, maono ama ujuzi katika mambo yote. Idadi yote ya watu waliomo serikalini katika ngazi ote ni ndogo mno, na uwezo wa kila mmoja wao kumiliki akili, maono, taarifa na weledi ni huo anaoweza kuwa nao mtu mmmoja, na uwezo wao wote ukichanganywa pamoja bado utakuwa ni kidogo ukilinganishwa na uwezo wa pamoja wa raia wa nchi husika.

Ndiyo maana ni hatari kwa watawala kudhani kwamba wanao uwezo wa utambuzi na uelewa kuwazidi wananchi wao. Na ndiyo maana, baada ya karne nyingi za mapambano baina ya matabaka hasimu, wenzetu walioendelea walitambua kwamba hawana budi kujenga mifumo na michakato inayotambua upungufu wa uwezo wa watawala, na kuweka utaratibu wa kurutubisha uwezo huo kwa kuukutanisha na uwezo unaopatikana miongoni mwa wananchi wasio na dhima ya kutawala.

Kutokana na kutambua hivyo, wenzetu waliweka utaratibu kama vile uwakilishi katika halmashauri na mabunge ambamo wawakilishi wao walipeleka hoja zao na kuzishindanisha, maslahi ya hawa yakikinzana na maslahi ya wale, huku pande zote zikizingatia maslahi ya pamoja ya kitaifa. Miundo na mifumo hiyo tulirithishwa na wakoloni wakati wakiondoka, na hadi sasa tunayo, hata kama tumeifanya ni kama mazindiko hasi yasiyokuwa na faida yo yote kwetu.

Lakini wenzetu wamekuwa wakiendelea na mifumo na michakato yao, ambayo wameipa uzima na kuifanya hai. Mabunge yao yanafanya kazi ya kuzikosoa, kuzielekeza na kuzidhibiti serikali zao. Halmashauri zao zinafanya vivyo hivyo. Inapofikia kwamba watawala wameonekana hawana usikivu, mabunge haya na halmashauri hizi inao uweo wa kuwaondoa madarakani.

Kwetu sisi tumebaki na mabunge na halmashauri magarasa, mapambo ambayo yanapendeza kuyaangalia na kumuonyesha mgeni, lakini huwezi kuyatuma sokoni. Ni mpangilio ulio ghali mno, lakini ambao hautuzaliii matunda tuliyotaraji.

Hata hivyo, hali kama tuliyo nayo, kimsingi siyo ya kwetu peke yetu. Wakati katika historia ya binadamu kumekuwapo na misuguano baina ya matabaka mbali mbali, au makundi mbali mbali, kila moja likipigana ili kuongeza manufaa yake, lakini kila muhula wa mapambano hayo hulizipeleka jamii husika katika ngazi mpya juu ya pale zilipokuwa awali.

Sisi tunaelekea kuwa tofauti. Ni kama vile tunatembea kinyumenyume. Mahali ambapo tulikwisha kupitia jui ndiko tunakotaka kurejea leo. Ni mithili ya watu wazima wanaotaka kunyonya vidole, kama watoto. Hatuelekei kama watu wanaojua hatua za kihistoria walizozipitia.

Mojawapo ya matatizo yanayotukwaa ni kutokuwa na utaratibu unaoeleweka na unaoufuatwa wa kupokeana utawala (achana na uongozi kwa sasa). Alipoondoka Julius Nyerere na kumwachia urais Ali Hassan Mwinyi, kwa miaka mitano Mweinyi alionekana akifanya kazi nzuri mno, kwa sababu, kimsingi, Nyerere alikuw ahajaondoka moja kwa moja.

Kwanza Nyerere ndiye alikuwa bado mwenyekiti wa chama-tawala. Maamuzi yote yalipitia mikononi mwachama kabla hayajatekelezwa serikalini. Lakini pia, waziri mkuu wa Mwinyi alikuwa Joseph Warioba, ambaye mtazamo wake ulifanana sana na ule wa Nyerere, hata kama alikuwa hapokei maelekezo yo yote toka kwa Mzee. Muhula wa wa pili wa Mwinyi ukaja kuwa tofauti kabisa na ule wa kwanza kwa sababu, kwanza Nyerere aliachia uenyekiti na Warioba akaondolewa kwenue uwaziri mkuu, na hapo ndipo tukaziona sura halisi za Mwinyi.

Tangu hapo tunachoshuhudia ni kila anayekuja kuja na lake, na hakuna mwendelezo way ale aliyoyakuta. Wakati mwingine wakuu wanatoa taswira kama vile utawala mpya umeingia kwa kuupindua utawala uliopita, au kama vile chama kipya (kilichokuwa upinzani) kimeingia madarakani. Kila anayeingia anaingia na timu yake ambayo lengo lake kuu ni kufutilia mbali yale yote yaliyofanywa na mtangulizi wake.

Katika awamu inayoitwa ya tano (binafsi naona awamu imekuwa ni moja tu tangu 1961), mambo mengi makuu ya ‘awamu’ ziliopita yametupwa nje, hata yale yenye manufaa ya dhahiri, kwa sababu wakuu wapya wana upendeleo kwa mambo mengine tofauti. Najiulia iwapo ‘awamu’hii itakapopita hakutakuja wengine naao wakayatupilia mbali haya tunayoyaona yakifanyika hivi sasa? Hili nitalieleza kwa kina huko mbele.

Kwa jinsi hii, hatuendi ko kote, kwa sababu hatulimbikizi matendo, ujuzi, uzoefu na manufaa; kila siku sisi ni watu wa kuanza upya.
Source : Kila ajaye ana jipya, hatuendi kokote
 
Membe, Ccm wote lao moja tu wanajuwa wanachokifanya ndio maana namshangaa sana Zitto kutaka kuingia kwenye mtego yaani TISS tena iliyochini ya ccm aje upinzani kwa usalama? siwezi kumuamini mpaka naenda kaburini!
Zitto na Chama chake watakuwa ni wajinga na wachumia tumbo kama wanaweza kumpa nafasi yoyote Membe ya juu.
 
Angalau kuna watu wako fair kwani tunahitaji kumjadili huyu aliyechukua fomu na alikuwakwenye Serikali zilizopita pia! Why attack just Membe as if he was the former Presida?
 
Back
Top Bottom