Rebeca 83
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 14,840
- 31,583
Hello JF,
Ningependa kujua kama ushawahi kupata tiba, kati ya hizo mbili (Tradition Medicine au Modern Medicine)
Ipi ili work?
Au zote?
Kipi kilichokusukuma utumie kimoja wapo?
Nini kilikusukuma utumie vyote?
Unatushaurije?
----------
Maoni ya Mdau
Ningependa kujua kama ushawahi kupata tiba, kati ya hizo mbili (Tradition Medicine au Modern Medicine)
Ipi ili work?
Au zote?
Kipi kilichokusukuma utumie kimoja wapo?
Nini kilikusukuma utumie vyote?
Unatushaurije?
----------
Maoni ya Mdau
Matumizi ya dawa za asili sambamba na zile za hospitalini na pia kuzichanganya kunaweza kusababisha matokeo hasi kwa mtumiaji hususani pale zinapotumika kutibu ugonjwa wa aina moja.
Dawa ni kemikali na kuna vitu vinavyohitajika kuzingatiwa ili ziweze kufanya kazi yake, na zinaweza kushindwa kufanya kazi yake vizuri pale ambapo zinapokutana na kemikali zingine kwa maana kila dawa ina namna yake ya utendaji kazi.
Mfano, baadhi ya dawa hususani za hospitalini hufanya kazi mwilini kwa kuzuia uzalishaji wa baadhi ya vitu ndani ya mwili ili kuweza kutengeneza mazingira ya kuudhoofisha ugonjwa na ikitokea ingizo la kemikali nyingine itakayofanya kinyume chake ndipo dawa ile hushindwa kufanya kazi vizuri.
Ndiyo maana hizi dawa tena hasa za hospitalini zina kitu kinaitwa 'Side Effects' na maelekezo maalumu ya jinsi ya kuzitumia ikiwemo pia vitu vya kuepukana navyo.
Jambo la msingi ni kuyasoma kwa makini maelekezo yanayokuja na dawa husika na pia kuzingatia ushauri wa Daktari atakayekupatia dawa kwa ajili ya matibabu.