Je, Mbunge Shibuda alikuwa wapi wakati makamanda wetu wengine wakiwa katika harakati za ukombozi?

Soki

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
1,303
279
Sikumsikia kabisa Arumeru East. Je alikuwa na makamanda wetu katika kampeni za udiwani? Wakati tunafurahia ushindi bado kuna mambo muhimu ya kujiuliza ili kuimarisha Vuguvugu hili la Mabadiliko! Najua kuna watu mnaweza kutupa ufafanuzi wa hili
 
Huyu jamaa tatizo haeleweki, inaonekana yuko mguu mmoja nje mwingine ndani! acha aendelee kuwa mtazamaji!
 
Alikuwa chimwaga akikamilisha kujaza form ya kurudi kwa akina Makamba!
 
Kwa mwenendo wake wala sishangai kwa kutokuwepo kwake. Hana msaada wowote kwa M4C
 
Yupo katika kukiimarisha kile chama chao kipya,mbona tulisha mtosa longtime huyo bwana mipasho...." chadema hatutaki wanafiki waongo,mamluki na yeyote atakaekwenda tofauti na misingi na kanuni za chama.tukikubaliana hapana tunakua tunamaanisha hivyo wote,ukileta zako za kuleta tunakupa chafu wala hatukusubiri kukupotezea muda na wala wewe kutupotezea muda.angalia selasini yuko wapi nae,alileta mambo yake ya k.i.s.e....ge tukamuweka pending .chadema tuna inteligensia ya ukweli na uhakika,sio ya kinafiki kama magamba.ukileta zako hatukukopeshi wala kukuchelewesha.chadema alwayz is people power.bora ukimwi kuliko chadema na shibuda.
 
Chama chenye nguvu hakiwezi kabisa kuhangaika wala kutikishwa na mtu mmoja tu, hususan hawa wanaijiunga kwa kuimarisha 'nguvu ya umma'. Ukiona mtu mmoja anakisumbua sana chama ujue chama hicho hakiko imara
 
Huyu jamaa tatizo haeleweki, inaonekana yuko mguu mmoja nje mwingine ndani! acha aendelee kuwa mtazamaji!

Watu wa aina hii ni hatari mno kwenye taasisi yoyote ile. wanatakiwa kudhibitiwa mapema kabla hawajasababisha madhara
 
Shibuda ni mtalii tu Chadema , muda ukifika itabidi arudi alikotoka kwani sidhani kama atahitajika tena chadema pengine yeye na aliyemleta waanzishe chama chao na wote wagombee urais!!
 
2015 Hawezi kupitishwa na m4c kugombea Maswa. ahamie ADC maana rangi za bendera zinafana kidogo japo malengo tofauti
 
sijui kapeleka wapi tumbo lake,minyoo aliyotoka nayo c.c.m inamsumbua hana kukaa cdm maana huku mwiha na mipasho marufuk
 
alikata tamaa akijua kwamba magamba yatabebwa tena arumeru kama ilivyokuwa igunga,kumbe hata kubebwa tu haya bebeki.
 
Huyu jamaa ni bonge la snich kwa kifup hatumuhitaj kwa vyovyote vile. Tunataka watu wenye hoja na sio mipasho.
 
Uzuri ni kuwa sasa amegundua kuwa kila Mtanzania anajua kuwa ni tycoon wa siasa. CDM haiigiliki ovyo kama ambavyo NCCR ilivyoingiliwa na vibaraka! Lile lilikuwa somo tosha sana kwa vyama vya siasa! Shibuda ni kibaraka wa kuogopwa kama ukoma! Good enough Watanzania wamemjua na mikelele yake ya mipasho ya ufitini
 
ni bora SHIBUDA ambaye alikuwa kimya kuliko ZITTO KABWE ambaye alikuwa busy na uraisi 2015 ili kuvuruga attention za uchaguzi ARUMERU ,hawa wote ni hatari mbaya zaidi ni huyo ZITTO ambaye ana cheo kibwa ndani ya chama
 
Wajameni vibaya hivyo,mwenzenu alikuwa makao makuu akilinda ofisi kwani mnadhani nani aliachwa kulinda!
 
Amewakimbia kwa uhuni wenu na mtaipata kisawa sawa 2015 pale Mbowe atakaposhindwa vibaya na Zitto Kabwe katika nafasai ya Kugombea Urais
 
Back
Top Bottom