Je, Mbowe ndiye Zamoyoni Mogela aka Golden boy wa Hai?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,761
141,627
Wale wahenga mnakumbuka namna Zamoyoni Mogela alivyokuwa anapaniwa na walinzi wa Yanga pindi timu ya Yanga ikutanapo na Simba miaka ile ya 80.

Nakumbuka picha moja ikimuonyesha Mogella akiwa amezungukwa na walinzi " wote" wa Yanga yaani Yusuph Bana, Ahmed Amasha, Rashid Chama, Isihaka Hassan na mkongwe Juma Mkambi ili asilete madhara kwa kipa wao Hamis Kinye.

Wiki Mbowe yuko ziarani huko Moshi katika jimbo la Hai lakini ni kama vile shughuli zote zimesimama ili asilete madhara.

Je, unajua Yanga walifanyaje ili kuondokana na tishio la Zamoyoni Mogella?.......Walimsajili.

Niishie hapo, CCM nadhani mmenielewa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbowe hana umalaya huo chukueni tu hao changudoa wenu wasiojitambua.
FB_IMG_1583215115657.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai!
Sasa huo mkate miaka nenda rudi hauyeyuki tu?Tusubirie mpaka lini?Maana kila ukiingia kwenye chai na kutoka bado uko vilevile tena unazidi kuonekana mgumu!Labda huo mkate tuuyeyushe kwenye "smelter" maana chai naona imegonga mwamba!
 
Subiria bunge livunjwe na ruzuku itamatike bwashee!
 
Sasa huo mkate miaka nenda rudi hauyeyuki tu?Tusubirie mpaka lini?Maana kila ukiingia kwenye chai na kutoka bado uko vilevile tena unazidi kuonekana mgumu!Labda huo mkate tuuyeyushe kwenye "smelter" maana chai naona imegonga mwamba!
Naona huo mkate ni "very special" kama hata kwenye chai hauyeyuki? Jawabu nikukaa pembeni na kufanya upembuzi hakinifu aina gani ya huo mkate then implementation process.
 
Akipata nafasi ajibu yale maswali kabla kusema wale ni watu waliotumwa kumharibia maana watu wa siku hizi hata akijikwaa atasema jiwe limetumwa bila kutafuta sababu ni nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom