Je, mawasiliano mfululizo kati ya China na Afrika yana uhusiano na mgogoro wa Ukraine?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
坦桑尼亚.jpg


Je, mawasiliano mfululizo kati ya China na Afrika yana uhusiano na mgogoro wa Ukraine?



Hivi karibuni, wakati macho ya watu wengi yanaelekezwa kwenye mgogoro wa Ukraine, mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya China na Afrika pia yamekuwa ya mara kwa mara. Sadfa hiyo imetafsiriwa na baadhi ya watu kama ishara kwamba China inatafuta nchi za Afrika kuunga mkono msimamo wake katika mgogoro huo.

Ni wazi kuwa, huu ni uvumi wa upande mmoja, tena ni wa kisiasa. Kama tunavyojua, shughuli hizi za kidiplomasia lazima ziwe zimepangwa mapema. Pia kuna ushahidi kwamba mawasiliano haya ya ngazi ya juu hayana masharti kwa msimamo wa nchi za Afrika kuhusu mzozo wa Ukraine, bali yanaonyesha kwamba ushirikiano wa hali ya juu wa China na Afrika unarejea polepole katika viwango vya kabla ya kuibuka kwa janga la COVID-19.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alikutana na wenzake kutoka nchi saba za Afrika. Miongoni mwao, mawaziri wa mambo ya nje wa Algeria na Zambia walitembelea mkoa wa Anhui, China, na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania alikuwa na mazungumzo ya video na Wang Yi. Wakihudhuria kikao cha 48 cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC mjini Islamabad, mawaziri wa mambo ya nje wa Somalia, Misri, Gambia na Niger nao walifanya mazungumzo ya pande mbili na Wang Yi. Mapema tarehe 18 Machi, Rais Xi Jinping wa China alizungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, na kujadili uhusiano wa China na Afrika, nafasi ya BRICS na G20 katika masuala ya kimataifa, bila shaka pamoja na mgogoro wa Ukraine.

Kwa hakika, kabla ya kuzuka kwa janga la COVID-19, mawasiliano hayo ya mara kwa mara ya ngazi ya juu kati ya China na Afrika yalikuwa ya kawaida. Takwimu zinaonyesha kuwa ziara za mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika nchini China ziliongezeka kutoka wastani wa nne kwa mwaka kati ya 2014 na 2019 hadi 28 kwa mwaka 2019 pekee, na baada ya hapo shughuli za kidiplomasia za mara kwa mara za ana kwa ana zilisitishwa kwa muda kutokana na janga hilo. Halafu mtu anauliza, kwa nini mawasiliano yanarudi wakati huu? Je, mikutano hii inahusu Ukraine? Ili kujibu maswali haya, tunapaswa kuangalia China na Afrika zilijadili nini katika mazungumzo hayo.

Ajenda ya kwanza ni kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika ili kufuatilia maafikiano yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika nchini Senegal mwishoni mwa mwaka 2021. Kwa mfano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Liberata Mulamula alijadili jinsi ya kuimarisha uhusiano kati ya Mpango wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025, na kupanua ushirikiano katika kilimo, biashara, uwekezaji, miundombinu na nyanja nyinginezo. Kuimarisha ushirikiano pia ni ajenda aliyotaja waziri wa mambo ya nje wa Zambia, Stanley Kakubo, ambaye alielezea nia ya Zambia kudumisha "mazingira tulivu ya biashara" na "sera nafuu za kodi" kwa makampuni ya China yanayoendesha biashara nchini Zambia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry na Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Abdisaid Muse Ali walieleza umuhimu wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kusisitiza nafasi muhimu ya China katika kuzisaidia nchi zinazoendelea kuimarisha uwezo wa kuhimili hali ya hewa, wakiishukuru China kuzisaidia kupambana na athari za ukame wa muda mrefu katika Pembe ya Afrika. Wang Yi naye alidokeza kuwa China itatoa msaada wa dharura wa chakula kwa Somalia na nchi nyingine katika eneo linaloathiriwa na ukame mkali.

Ajenda ya pili ni kusaini mikataba. Kwa mfano, China na Algeria hivi majuzi zilitia saini mkataba wa kuwekeza dola bilioni 7 kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea katika jimbo la Tebessa nchini Algeria, ambao unatarajiwa kutoa nafasi za ajira 12,000. Wiki iliyopita nchini Misri, Eneo la Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara la Suez la China na Misri lilikubali kushirikiana na kampuni moja ya China kujenga kituo cha kutengeneza muundo wa chuma. Aidha, hivi karibuni serikali ya Zambia ilitiliana saini mkataba wa makubaliano na kampuni ya China ya Huawei kuanzisha kituo cha ubunifu wa kidijitali na kutoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi 5,000 katika teknolojia na mawasiliano ya habari ifikapo mwaka 2025.

Ajenda ya tatu na ya mwisho ni masuala ya kisiasa. Bila shaka mgogoro wa Ukraine umo ndani, lakini Waafrika pia wana vipaumbele vyao vya kitaifa na kikanda vya kujadili, likiwemo suala la Sahara Magharibi, kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi na Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance.

Hali halisi ni kuwa nchi saba za Afrika zina maoni tofauti kuhusu mgogoro wa Ukraine. Misri, Gambia, Niger, Somalia na Zambia ziliipigia kura Ukraine katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika Machi 2, wakati Tanzania na Algeria hazikupiga kura, kama ilivyofanya China. Ni wazi kwamba mawasiliano haya ya mfululizohayategemei iwapo nchi za Afrika zina maoni sawa na China. Tukizungumzia hilo, hatuna budi kusema kwamba hii ni kinyume kabisa na jinsi baadhi ya nchi za magharibi zilivyoshughulikia suala la Ukraine. Kwa mfano, hivi majuzi Uingereza ilighairi ujumbe uliopangwa kwenda India kutokana na msimamo wa India kuhusu mgogoro wa Ukraine.

China inafanya shughuli za kidiplomasia na nchi za Afrika bila kuweka masharti yoyote, na kuifanya China kuwa mshirika thabiti na muhimu wa maendeleo wa nchi za Afrika. Bila shaka, mikutano hii pia ilifanyika katika muktadha wa utekelezaji thabiti wa China wa sera ya kupambana na virusi vya Corona, ambayo inaruhusu watu kutarajia zaidi mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika kurejea zaidi na kuendelea kukuzwa.
 
China =Ma snitch wa kiwango cha SGR. Mnaambiwa na wamarekani kwa siri, baada ya kuonyeshwa taarifa za inteligensia, mkawazuie warusi wasiishambule Ukraine kwa sababu ni rafiki yenu.

Kwanza mnabisha kuwa si kweli halafu na ninyi kwa siri mnawaambia Warusi eti US wanasema mnataka kuishambulia Ukraine. Wachina wapuuzi sana.

Shame on you.
 
Back
Top Bottom