Je, Matusi ya Mbunge wa CCM Tarime ndio ustaarabu unaotukuzwa na viongozi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Matusi ya Mbunge wa CCM Tarime ndio ustaarabu unaotukuzwa na viongozi wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Silas Haki, Mar 13, 2011.

 1. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kati ya vitu vinavyotia kichefuchefu mbele ya wananchi ni unafiki unaofanywa na viongozi wa CCM kusema kuwa vyama vya upinzani vinatumia lugha chafu na ya uchochezi vinapowaelimisha wananchi kuhusiana na haki zao zinapopokwa na watawala. Viongozi wa CCM na serikali yake huwa wepesi wa kukurupuka na kukemea vitendovya kuwafumbua macho wanyonge.

  Je, matusi haya ya Nyambari Nyangwine tuyaite ni ustaarabu wa CCM? Je, matusi hayo hayajengi chuki kutoka kwa wananchi waliotukanwa? Soma habari hii ujue matusi hayo.

  "CCM yamkana mbunge wake kwa matusi"


  Source: Tanzania Daima 13 Machi, 2011 by Ambrose Wantaigwa, Tarime  SAKATA la Mbunge wa Tarime, Nyangwine Nyambari (CCM) la kudaiwa kutoa lugha ya matusi kwa wanachama wenzake na wapiga kura wakati akihutubia mkutano wa hadhara wiki moja iliyopita wilayani hapa limechukua sura mpya baada ya chama chake kuibuka na kudai "matusi ya mbunge huyo yasichukuliwe kuwa matusi ya chama."

  Badala yake chama hicho kimelaani matumizi ya lugha za matusi zinazotolewa na baadhi ya makada na viongozi wake kwa maelezo kuwa kauli kama hizo zinachochea chuki na migawanyiko ndani ya chama na wananchi kwa ujumla.
  Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, Rashid Bogomba, amewaambia waandishi wa habari mjini hapa leo kuwa wanalaani kwa nguvu zote kauli zilizotolewa na mbunge huyo na kusisitiza kuwa zilikuwa ni kauli zake binafsi na hazikuwakilisha chama hicho.

  "Sisi kama chama hatuungi, hatujawahi na hatutawahi kuunga mkono kauli kutoka kwa mtu yeyote mwenye itikadi yoyote kutumia lugha zinazoashiria matusi wala uchochezi kwa wananchi na kwa sasa tunachukulia kauli ya mbunge wetu kama yake binafsi na si vinginevyo," alisema mwenyekiti huyo.

  Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa kuwa jitihada za vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara CCM vilivyofanyika wiki hii kujaribu kumnusuru mbunge huyo kwa kumtaka aombe radhi kwa wananchi zilishindikana.

  Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kililidokeza gazeti hili kuwa mbunge huyo aligeuka mbogo kwa wajumbe baada ya kutamba kuwa yeye ni shujaa aliyelikomboa jimbo hilo kutoka kwa wapinzani hivyo wamuache hivyo hivyo.

  "Unajua mwandishi, mbunge aliwageukia wajumbe kwa kuwaeleza ugumu aliopata katika kukomboa Jimbo la Tarime lililokuwa ngome ya CHADEMA na kudai alitumia nguvu na rasilimali nyingi kiasi cha kuwabwatukia wajumbe kuwa wamwache jinsi alivyo," alieleza mtoa taarifa wetu.

  Wiki iliyopita mbunge huyo akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Sabasaba wilayani hapa alitoa kauli iliyoonekana kuwa ya matusi kwa wapinzani wake kutoka ndani na nje ya chama chake kwa kudai kuwa wote waliompinga wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wakimuita mbunge wa briefcase waende wakawaambie hivyo mama zao.

  "Briefcase ni mama zenu," alisikika akisema hivyo mbunge huyo wakati wa hotuba yake hiyo
   
 2. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kwanza amesababisha wanafunzi wetu wawe wavivu wa kusoma kwa mtindo wake wa kutunga madesa ya kuwakaririsha.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bwana malkiory, una uhakika kwamba ana uwezo wa kutunga madesa huyo jamaa? Dodosa kwa waliosoma naye shuleni/ chuoni utasikia mengi> Ni ajabu kama mtunzi wa madesa mwenyewe ni muoga wa mitihani, yaani bimgwa wa kudesa! The so called madesa hayo ni full of plagiarism!
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  yupko stresssed up alitoa mil 70 kwa maofisa wa mkuru ili apate uwaziri,uwaziri kakosa na imekuuuura kwake jivo kachanganyikiwa.....................
   
 5. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Acha wagombane ili iwe kazi rahisi kwa CHADEMA kulirudisha jimbo uchaguzi ujao.Vita vya panzi furaha ya kunguru.
   
 6. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu la kuvunda halina ubani.." siku si nyingi ukweli utaonekana, mkwere chama kitamfia mikononi
   
 7. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  piga chini nyambari, akazidi kuwaambukiza ngoma wanafunzi pale ubungo kwake
   
 8. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duu! huyu jamaa kweli ni mkali wa matusi. Anatukana kama kuli.
  Big up CCM kwa kumkana, endeleeni kuwakana hata wazee wavijisenti, RA, ED kwa matendo yao ya kufilisi nchi.
   
Loading...