Je, matumizi ya madawa ya kulevya ni uhalifu?

monomotapa

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
437
325
Nimewaza sana hii issues ya Drugs:
Ingawa ni suala la kibinadamu zaidi kusaidia wenye uhitaji, ila inaumiza kutumia pesa zetu walipa kodi kwaajili ya kununua madawa (Methadone) ya kuwatibu watu ambao kwa hiari yao wenyewe walijiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya (Ninavyojua mimi ni Hualifu)
Kama hakuna punishment yenye maumivu kidogo kwa wakosaji tutajifunza vipi? Hakutakuwa na lesson learnt hapa, inabidi washtakiwe wapelekwe magerezani wakafanye kazi ili wafidie gharama wao wenyewe. Pesa za walipa kodi zitumike kwa mambo mengine ya maendeleo. kuna wananchi wema huko vijijini wanaozalisha chakula hawana huduma ya maji safi, huduma za kliniki za akina mama na watoto, umeme, barabara nk wao wanastahili kupewa kipau umbele

Muda wa kuendekeza mambo ya hovyo hovyo na ya kujitakia haupo na hauna nafasi dunia ya sasa

Inatakiwa magereza pia yawe na uwezo wa kujilisha na kujiendesha, wafungwa lazima watengewe ardhi ya kutosha (Tanzania kuna ardhi kubwa sana) wajilishe na ikiwezekana wauze ziada kulisha jamii . Inatakiwa iwe institution inayojiendesha yenyewe, kama mtu anaamua maisha ya huko ni mazuri basi achague tu afanye mazabe mtaani apelekwe huko fasta....

Sio vyema kutumia ruzuku ya serikali (Pesa zetu za kodi kulisha waalifu) lazima wafanye kazi ngumu kidogo ili wajifunze kuwa na asiyefanya kazi halali na asile

Ni mawazo yangu tu.... Sina chuki na mtu yeyote bali nasikia kutotendewa haki jinsi ninavyopigika na maisha yangu ya kutafuta riziki kiuhalali kila siku na bado nalipa kodi ....Wengine wanaleta mchezomchezo na maisha na bado wanatibiwa bure. Tulishaambiwa hakuna tiba ya bure Tanzania lazima kuchangia
 
Back
Top Bottom