Je, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Mahakama zetu yanatekelezwa au yamepuuzwa?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,119
7,701
Jitihada za kipekee zilizo fanywa na hayati JPM kataka kuhakikisha vyombo vyetu vya utoaji Haki yaani; Mahakama, DPP na Polisi vinatumia kiswahili badala ya kiingereza.

Msukumo mkubwa ulifanyika na kisha sheria zilibadilishwa ili kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inatumika kikamilifu ktk Kusikiliza kesi na uandishi wa hukumu.

Pamoja na mabadiliko ya sheria, Je, Majaji wetu na Mahakimu wetu wapo tayari kukitumia kiswahili au wameamua kukinyanyasa kiswahili na kuendelea na matumizi ya kiingereza?

Malengo na Makusudio ya kubadilisha sheria ili kuruhusu kiswahili kitumiwe katika kusikiliza kesi na uandishi wa hukumu dhumuni lake ni kuhakikisha sisi watanzania tuweze kuelewa kwa urahisi haki zinazo tolewa, sasa kama kiswahili kina puuzwa na kuendelea kutumia lugha ya kiingereza maaana yake ni nini haswa? Je, Majaji na Mahakimu ni raia wa kigeni au ni waswahili wenzetu?

Bado tunaona Hati za mashitaka zinaandikwa kwa lugha ya kiingereza badala ya kiswahili, jamani shida ni nn?
kama walio ajiriwa hawajui kiswahili bora waondolewe na kisha wawekwe wanao au waajiriwe watu wazalendo wanao enzi na kuthamini lugha na tunu yetu ya Kiswahili.

Tunaomba matumizi ya Lugha ya Kiswahili mahakamani yazingaitiwe na yawekewe mkazo kamwe yasifanyiwe mzaha na kejeli.

Sisi raia wa tanzania ndio tunapaswa kupewe kipau mbele, karibu asilimia 99 ya watanzania wote wanao kwenda kupata huduma mahakamani ni watanzania, hivyo hakuna sababu ya kuendekeza matumizi ya kiingereza na kukidharau kiswahili.

Vyombo vyetu vya utoaji wa Haki Mahakama zingatieni matumizi ya kiswahili kwa masilahi ya Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania.

Kazi iendelee
 
Kamba ndiyo imekatikia pabovu hivoooo!!! Aiseee!!! Miaka 60 tena tumepiga hatua kurudi tulikotoka. Jamani Magu alikuwa bonge la kiongozi. Amefanya mpaka South Afrika, Kenya, Uganda, Kongo, Malawi, Msumbiji, na nchi nyingi za Afrika na nje ya Afrika kukipenda Kiswahili na kuingiza kwenye mitaala yao ya ufundishaji. Sasa Bi Mkubwa kazi kuhutubia kwa Kiingereza tuuu, mara utasikia ^Ooooooooohh^ ^Ooooooooohh^ ^Ooooooooohh^ nyingiiiiiiiiiiiiiii
 
Kuandika kwa Kiswahili hakumfanyi mtu aelewe sheria sababu sheria ni lugha ya kitaalamu (kitaaluma), ina wataalamu wanaojua kuisoma na kuitafsiri. Mwendazake alichukulia kama watu wanaonewa sababu ya sheria kuwa katika kiingereza kitu ambacho sio kweli.

Mahakamanikesi zinaendeshwa kwa Kiswahili ila kumbukumbu zinaandikwa kwa Kiingereza, hata hukumu zinaandikwa Kiingereza lakini zinaposomwa na hakimu au jaji kwa wenye kesi, zinasomwa kwa Kiswahili.

Kiswahili kitumike mahakamani kwa lengo la kukuza lugha na sio kwa kujidanganya kuwa kitasaidia watu wasionewe, watu tunajua sheria na makosa vyema kabisa, tusijifiche kwenye lugha pale tunapofanya makosa.
 
sheria zipo tayari zimesha tungwa kilicho baki ni utashi wa kuzitekeleza sheria hizo za matumizi ya Lugha ya kishwahili ktk taratibu zote za utoaji wa haki.
 
Back
Top Bottom