Je Mashujaa wa Tanganyika ni wakina nani?

Articulator

Senior Member
Sep 21, 2011
194
141
Jana rafiki zetu wa nchi jirani ya kenya walikua wakisherehekea sikukuu ya Mashujaa waliopigania ukombozi na hatimaye kufanikiwa kulipatia uhuru taifa hilo kutoka mikokononi mwa mkoloni.Mashujua hawa ni wale walioshiriki 'directly'katika vita ya Maumau(Mzungu arudi ulaya,Mwafrica apate uhuru) na wale waliochochea kwa namna moja au nyingine kuhumasisha vuguvugu hilo la kumuondoa mkoloni kwenye ardhi ya kenya.Wengine wanaotambulika na kukumbukwa na taifa la Kenya kama ni mashujaa ni watu walioshiriki katika ujenzi wa taifa baada ya nchi yao kupata uhuru.Baada ya kuona shamrashamra za sherehe hizo katika magazeti na runinga swali lililonijia kichwani ni Kweli taifa letu la Tanganyika linao watu ambao tunaweza kujivunia na kustahili kupewa jina la mashujaa wa taifa hili?Tukiwa tunaadhimisha miaka hamsini ya uhuru na utawala uliooza wa "chama cha mafisadi",taifa hili bado linalia na matatizo ambayo yameshindwa kupatiwa suluhu kutokea kuanzishwa kwa taifa hili mpaka sasa.Inatia uchungu sana ukifikiria tatizo la umeme linavyo zidi kutikisa uchumi hafifu wa taifa hili huku watu wanaotuhumiwa kutufikisha katika "nightmare" wakiendelea kufurahia uhuru na kujiongezea ukwasi kwa biashara mbalimbali ambazo chimbuko lake ni kodi ya mtanganyika ambapo kwa mujibu wa takwimu asilimia chache ya watanganyika ndio walio privileged enough kuweza kuishi kidogo beyond the poverty line.Swala la bad governance or rather poor governance limekuwa kitendawili kikubwa ambacho kimeshindwa kuteguliwa kutoka uhuru mpaka sasa na ndio kwanza limezidi kushika hatamu ndani ya serikali inayoendeshwa na chama hiki.Ukosefu wa ajira,ukosefu wa maji safi na salama kwa maeneo mengi ya mijini na vijijini licha ya taifa hili kubarikiwa na vyanzo lukuki vya maji na kupata ufadhili wa miradi ya uchambaji visima kutoka kwa wahisani mbalimbali wenye nia njema na taifa hili but asilimia kubwa ya fedha hizi imekuwa zikiishia mifukoni mwa wachache wasio na huruma wala chembe ya uzalendo na taifa hili.Huduma mbovu za afya,rushwa,uhaba wa shule,mishahara mibovu kwa walimu kitu kinachosababisha kudorora kwa elimu.Nikiendelea kuyaorodhesha matatizo yanayokabili taifa hili najua wengine mtachoka kusoma kwani hayana mwisho nikiamua kuyadadavua kwa undani licha ya upeo wangu kuwa mdogo kwani sikumbuki the last time i took an IQ test(utani),nasema hivi ili nijipe solace niondokane na fikira hizi kwani zina nipa hasira mno.Its about time watanganyika tuamke na tukatae udhalimu huu,muda tuliowapa wa kuabuse public offices na kumisuse public funds umeisha.Saa ya mapinduzi ni sasa na pamoja tutafanikiwa kuwaondoa na ni imani yangu baada ya ukombozi ipo siku tutasherehekea mashujaa wetu na kufurahia uongozi uliotukuka. Please excuse my poor writing skills kwani sijapitia mafunzo yoyote ya uandishi,naomba kutoa hoja!
 
Back
Top Bottom