Je! Mashine za kunyolea (za saloons) zinaweza kukuambukiza virusi vya UKIMWI?

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,902
3,077
Jamani wakuu, ningependa kujua ukweli wa hili swala...

Kiukweli, unapoenda kunyoa saluni.. Unakuta mashine za kunyolea zimeshawanyoa watu wengi, tuchukulie mfano imeshanyoa mtu mwenye virusi vya ukimwi, alafu mashine hiyohiyo ikatumika katika kukunyoa nywele na kukuchonga. Baada ya kunyolewa unapopakwa spirit unahisi maumivu katika maeneo hasa uliyochongwa, hii inaonyesha kuwa kuna vidonda vidogo vidogo katika maeneo hayo yanayouma baada ya kuweka spirit...

Je unaweza kupata virusi vya ukimwi kama mashine iliyotumika iliwahi kumnyoa mtu mwenye virusi vya ukimwi?

Tufanyaje ili kuepukana na maambukizi (kama yapo) katika masalooni?

NB! Maana mimi huwa nakataa kuchongwa au kunyolewa nywele zote, huwa napunguza tu nywele kwa vitana (hasa cha namba 1) vya mashine.
{jamani sijawa nyanyapaa waathirika}
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,522
6,494
Wajuzi hebu tufahamisheni kisayansi na kama kuna utafiti uliofanyika ni vyema tukajuzwa kilichojiri
 

Hubeb

Senior Member
Mar 21, 2017
166
237
Umeuliza jambo muhimu mkuu huwa napataga ukakasi sana nikiwa saloon!
wajuzi mkuje huku tafadhali!
 

Kirisongo

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,778
7,630
Actualy Tunaposemaa Maambukizi ya VVU Njia kuu Hasa Ni Ngono zembe yaani Ngono Bila Kinga, ila kupitia njia ya haja kubwa pia rate ya maambukizi ijulikane kwamba inakuwa kubwa kutokana na kwamba hakuna vilainishi asili kama vya kwenye uke Na Pia Hiyo Ngono Bila Kinga ni Probability Pia Kupata kutokana na viral Load aliyonayo mwathirika, kama ana viral load kubwa basi mtu 1 kati ya watu 100 anaweza kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU ila kama ana viral load ndogo basi mtu 1 kati ya watu 1000 anaweza kupata maambukizi, kwa mfano mtu anayetumia ARV anakuwa na Undetectable viral Load na ukifanya nae ngono yaani bila Kinga inakuwa Salama sawa na Kutumia Condom, Basi kwa Mantiki Hiyo Viral Load kwenye Mashine ya Kunyolea ni Ndogo sana Kiasi kwamba Hatari yake ni ndogo sana (Hapa naomba ieleweke kwamba uwezekano wa kupata upo ila ni mdogo sana sana)

Note: Ni Vema Kumuuandaa Mwanamke Vema Kabla ya sex Maana Hupunguza Hatari ya Maambukizi!
 

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,799
6,307
Hii thread haikuwahi kujibiwa!?
2011-2016 watu walishasahau kuhusu ukimwi na kuonekana ni kama malaria tuu. Hivi karibuni yamezuka magonjwa hatari zaidi hivyo kuwafanya watu wapotezee mambo ya VVU nadhani ndiyo sababu ya hii post kutupiliwa mbali.
 

kingsize25

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
229
350
Kwa uelewa wangu virus vya ukimwi haviwezi ku'survive kwenye atmosphere ya kawaida yani tofauti labda na kwenye mwili au damu, once vikiwa exposed kwenye mazingira ambayo siyo yao vinakufa.....

Ila usiniamini sana mimi maana sina uhakika saaana....BTW kama ingekua vinasambaa kwa namna hiyo ya mashine....nahisi nusu yetu tungeshakufaga
 
  • Thanks
Reactions: 7ve

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom