Je masharti ya kukopa kwenye taasisi za fedha kupitia title deed/hati ya kiwanja yakoje?

pachanya

JF-Expert Member
May 20, 2012
1,983
2,087
Ndugu wanajamvi naomba kujuzwa taratibu za kukopa Katika taasisi zetu za kifedha upoje kwa dhamana ya title deed/hati ya Kiwanja..
1: Je nahitaji kuwa na business plan ili nikopesheke?
2; Je. Naweza kukopeshwa kiwango cha fedha Mara ngapi ya thamani Ya kiwanja changu?
3;Je naweza kukopeshwa ili nikaanzishe biashara mwanzo kabisa?
4;Ni taasisi gani nzuri kwa kukopa yenye terms nzuri kwa customers.
Natumaini majibu yenu yatanipa mwanga wa wapi pa kuanzia....Nina title deed.
 
Taasisi za kifedha haziangalii dhamana. Wao hukopesha kutegemeana na biashara yako. Zaidi wataangalia unavyojiendesha kama hiyo biashara inaweza kukopa kiasi gani lakini inategemea na mahitaji yako pia sema hawawezi kukupa zaidi ya uwezo wa biashara yako kulipa. Dhamana inakaa tu pale kama in case likitokea la kutokea.
 
Nashukuru sana kwa majibu yako....vp kwa sisi ambao hatuna biashara zinazoendelea? Tunategemea huo mkopo ndo uwe cha chanzo cha biashara? Tunaweza kopesheka?
 
Lazima kuwe na biashara ambayo imedumu kwa miez sita na kuendelea ndio uweze kupata mkopo wa biashara,labda ukope mkopo wa uwekezaji(investment loan).
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom