Je, Marine ni imara, naweza jengea fremu ya biashara?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Kwa wasio yajua, au pengine unayajua lakini hujui kama ndio nayazungumzia.

Ni haya picha.
Screenshot_20200615-035524.jpg
Screenshot_20200615-035710.jpg
Screenshot_20200615-035358.jpg
Screenshot_20200615-035437.jpg
Screenshot_20200615-035057.jpg
Screenshot_20200615-034921.jpg


Yanakua ya urefu wa 8Ft na upana wa 4ft,
Unene wa 12mm au 18mm

Naomba Wazoefu ya haya ma Board, au Kuyaona popote yakiwa yametumika kwa ujenzi(najua yanatumika sana kwenye utengenezaji wa madaraja, karavati Magorofa n.k katika kumwaga zege) Jee ni imara kiasi naweza jengea nikayatumia kama ukuta na floor chini?

Nimepata eneo la biashara, naweza jenga fremu lakini Siruhusiwi na siwezi kujenga kwa kutumia Tofali, Inatakiwa nijenge juu juu, na nikitakiwa kuhamisha nifanye hivyo..

Kuna option ya mbao, lakini kuachana tuu na gharama, lakini haya naona yana muonekano mzuri hasa nikizingatia aina ya biashara,

Na jee Bei yake unayoijua wewe ni sh ngapi?
Yanatengenezewa hapa nchini?
Ma dealers wa kubwa wa haya madude ni akina nani, ili niende hata godauni kwa bei nzuri zaidi..
Namaanisha wale wauzaji wa kwanza.

Fremu yangu ni ya 16ft kwa 8ft,
Nimepiga mahesabu, naweza yahitaji kama 16..
Kuna mtu kaniambia elf 45 napata moja tena la 18mm, nimepiga mahesabu, kwa 1M nasimamisha fremu, Nikiwa nimeua finishing na floor humo humo..na ni suala la Siku moja kama sio masaa..

Je kuna ujenzi wowote unaweza kuja chini ya hapo, ukiwa umemaliza finishing na floor? na uwe na ubora?(zingatia ukubwa wa chumba)..

Hii idea imenijia baada ya kuumiza kichwa, kila option nikaona mahesabu yanagonga ukuta.
 
Yapo vizuri cha muhimu ni usalama wa nje tu maana kama unaweka mali ndani wahuni wanayatoboa kama wanatoboa mkate tu.

Yanatengenezwa kwa wingi sana Iringa Mafinga
 
Back
Top Bottom