Je, Marekani ina nia ya dhati kujenga Miundombinu barani Afrika ama ipo kwenye ushindani tu na China?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG31N1238270074.jpg

Na Pili Mwinyi

Ni miaka tisa sasa tangu rais wa China Xi Jinping atangaze pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” duniani, ambalo mbali na mambo mengine pia linajikita zaidi katika uwekezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu. Pendekezo hili lilitolewa kwa ajili mahsusi ya kuanzisha zama mpya ya biashara na ukuaji wa uchumi katika bara la Asia, Ulaya, Afrika na kwengineko. Baada ya kipindi chote hicho cha utekelezaji wa miradi mbalimbali, mafanikio makubwa yameonekana hasa katika nchi za Afrika.

Lakini mafanikio haya sio kwamba yanawaridhisha watu wote, kuna baadhi ya nchi ikiwemo Marekani, zimekuwa na roho ya kwanini na kukosoa kila wanapoona China inazidi kusonga mbele na kupiga hatua kubwa kupitia pendekezo hili.

Katika kipindi hiki cha majira ya joto tumekuwa tukishuhudia safari nyingi zinazofanywa na rais wa Marekani Joe Biden pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa nchi hiyo, wakitangaza ahadi ya mamia ya mabilioni ya dola kwa nchi maskini zaidi. Lakini ahadi zote hizo ni bure tu, madhumuni yake hasa ni kuhakikisha inaidhibiti China, kwa kuwa sasa ndio imekuwa mfadhili mkubwa wa miradi ya miundombinu katika Afrika.

Hatukatai kuwa ushindani kawaida unaleta chachu kubwa katika kutimiza jambo kwenye nyanja yoyote ile, lakini kinachosisitizwa ni ushindani mzuri na wa kiujenzi, na wala sio ushindani wa kubomoa na kuharibu. Ni karibu muongo mmoja sasa China imekuwa ikitoa mabilioni ya pesa kwa ajili ya maendeleo ya nchi za Afrika ikijenga barabara kuu, reli, bandari miundo mbinu ya umeme na mawasiliano ya simu, kupitia pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na “Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika” FOCAC.

Juni mwaka huu, Biden na viongozi wa kundi la nchi 7 (G7) waliahidi kuanza kufanya uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 600, ambapo bilioni 200 kati ya hizo zinatoka kwenye mfuko wa Marekani pekee, na kuahidi kwamba hadi ifikapo mwaka 2027 watawasilisha miradi mikubwa na ya aina yake ili kuziba pengo la miundombinu kati ya nchi.

Kama haitoshi, ili kuwafanya watu wa Afrika wavutike na kushawishika zaidi na ahadi zao za kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya miundombinu, mara nyingi Marekani imekuwa ikikosoa miradi inayojengwa na China barani Afrika. Katika ziara yake nchini Afrika Kusini, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitangaza mipango yake kwa Afrika alitoa shutuma nyingi dhidi ya miradi ya China.

“Tumeona matokeo yake, wakati mikataba ya kimataifa kuhusu miundombinu inapokuwa mibovu na ya kulazimisha, inapojengwa vibaya au kuharibu mazingira, inapoagiza wafanyakazi kutoka nje au kunyanyasa wafanyakazi wenyeji, na kuzibebesha nchi madeni makubwa,” alisema Blinken.

Waswahili wana msemo mmoja maarufu usemao “mwenye macho haambiwi tazama”. Marekani sio kwamba haioni maendeleo inayopata Afrika kwa sasa, bali ina nia mbaya ya kuichafua China kwa kila inachofanya, ili tu kuzibia riziki zake na kuvuruga ushirikiano na undugu uliopo baina ya China na Afrika.

Nikitolea mfano nchini Ethiopia, hivi sasa maelfu ya makontena yanasafirishwa kutoka bandari ya Djibouti na kupelekwa hadi kwenye bandari kavu ya Ethiopia, na kazi hii yote inafanikiwa kutokana na reli ya kisasa iliyojengwa na China kutoka Djibouti hadi Ethiopia, na kubadilisha kabisa historia ya Ethiopia ikiwa kama nchi isiyo na bahari. Mkuu wa Kampuni ya pamoja ya Reli ya Ethiopia-Djibouti Tilahun Sarka anasema reli hii imewakomboa sana Waethopia.

“Ethiopia ni nchi isiyo na bahari, na reli hii kati ya Djibouti na Ethiopia inatuunganisha na bandari ya Djibouti. Kwa hiyo kwa sisi, reli hii imetubadilisha kutoka nchi isiyo na bahari na kuwa nchi inayounganishwa na bahari.” Anasema Sarka.

Huu ni mfano mmoja wa waziwazi ambao hauhitaji kuulezea kwa mapana ili mtu auelewe, kwa walengwa wa miradi hii ya miundo mbinu ni faraja kubwa sana kwao na wanaisifu China kwa kubadilisha maisha yao, lakini cha kuchangaza na kujiuliza ni kwamba kwanini nchi baki ndio zinakuwa wa kwanza kulaumu?

Wakati umefika sasa kwa Waafrika ambao ndio walengwa wakuu, kuamka na kujua nani mwema kwao na nani mbaya kwao. Na kutambua kuwa kama kweli Marekani ina nia ya kuisaida Afrika kwenye masuala ya maendeleo na miundombinu basi ingeshaisadia zamani. Wahenga wanasema mti wenye matunda mazuri ndio unaopopolewa zaidi kwa mawe, hivyo kwa upande wa China ni vyema ichukulie lawama hizi kama chachu ya kuimarisha ushirikiano wake na Afrika, pia China inapaswa kukumbuke kwamba kawaida “kelele za mlango huwa hazimnyimi usingizi mwenye nyumba”.
 
Hakika muhenga umenena yaliyo sahihi kabisaaa...

Naheshimu mawazo yako nitaongezea point zangu baada ya kusoma mengineyo ya wadau.
 
Hizi ni mentality za kimasikini, yaani miundombinu yako ije ijengwe na mataifa mengine? Na unakuja mbele kuandika uzi, kweli? Pathetic
 
Back
Top Bottom