Habari wana jf! Najua mtakuwa mshawahi kusikia au kuona wanandoa au wapenzi wakiamua kupeana mapumziko kidogo baada ya kuanza kuhisi hali ya kuchokana inayotokana na kushuka kwa hisia za mapenzi kati yao. Je,mapumziko hayo yanaweza kuzirudisha hisia zao kileleni kiasi wakajikuta wanarudi kwenye uhusiano ulioimara kama awali walivyoanza? Nawakilisha hoja.