UZUSHI Mapovu yanayokuwa kwenye mimea mbalimbali porini au vichakani ni mate ya nyoka

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Tangu nikiwa mdogo nilisikia na kuamini kwamba ute/ mapovu yanayokuwa kwenye mimea ni mate ya nyoka. Mpaka kufika wakati huu bado sijajua kama suala hili lina ukweli ama la.

Naomba wataalamu mnisaidie kujua uhalisia wa jambo hili

1683974449172.png

Kielelezo 1: Picha ikionesha mmea umeachiwa mapovu

1683975760431.png

Kielelezo 2: Picha ikionesha mdudu aina ya Spittlebugs anayetengeneza Povu kwenye mimea

Video ikionesha namna wadudu aina ya Spittlebugs wanavyotengeneza povu
 
Tunachokijua
Imekuwa ni imani ya wengi katika jamii mbalimbali wakihusisha mapovu yanayopatikana kwenye mashina na matawi mengi ya miti iliyo porini au vichakani na mate ya nyoka. Watu wengi wenye imani hii wamekuwa wakichukua tahadhari kubwa wakiamini kwamba ukiona mmea una mapovu hayo ni ishara kwamba nyoka wapo maeneo ya karibu.

Je, mapovu yanayokuwa kwenye mimea mbalimbali porni au vichakani ni mate ya nyoka?
Jamiiforums imefuatilia katika makala na tafiti za kisayansi kubaini ukweli wa jambo hili ambapo tumebaini yafuatayo

Texas Naturalist wataalamu wa Mazingira na Chuo Kikuu cha Florida nchini Marekani wamefanya utafiti na kubaini kuwa mapovu hayo yanayokuwa kwenye mimea hayahusiani na nyoka isipokuwa ni mapovu yanayozalishwa na wadudu waitwao spittlebugs ambao wanatoka kwenye familia ya Aphrophoridae na superfamily Cercopoidea.

Wataalamu wanaeleza kuwa Wadudu hawa hutembea kwenye mimea na huzalisha mapovu kama mbinu yao ya kujilinda wasishambuliwe na wanyama wengine wakati wananyonya utomvu wa mmea husika.

The New York Times wanaeleza kuwa Povu la spittlebugs hutokana na kuchanganya hewa na maji iliyopo tumboni mwao hivyo kulitoa povu hilo kama mkojo. Inaelezwa kuwa Wadudu aina ya spittlebugs wapo zaidi ya makundi (species) takriban 930 katika nususpishi 160 duniani.

Je povu hili ni sumu au hatari?
Wataalamu wa masuala ya mimea RHS wanaeleza kuwa Povu lenyewe halina hatari kwa asili yake na haliwezi kumuathiri binadamu, lakini wadudu aina ya spittlebugs wanaweza kubeba na kusambaza bakteria ya aina ya Xylella fastidiosa, ambayo husababisha magonjwa hatari ya mimea.

RHS wanaeleza kuwa bakteria hawa hula Mirija/njia inayotumiwa kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi ya mmea kwenda kwenye sehemu za shina, matawi na majani ambayo hupelekea majani kuwa kama yamechomwa moto, kuoza, kupukutika au mmea mzima kufa.

Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo JamiiForums inaona hoja inayoeleza kuwa mapovu hayo ya kwenye mimea ni mate ya nyoka si ya kweli.
Tulio kulia vijijini mambo mengine tuliyajua zamani sana, miaka ya 94 tukiwa tunachunga mbuzi tumewachezea sana leo wamarekani wamegundua! Dah hizi pesa hizi!
 
Yap! Mi mwenyewe nimekua nikijua hivyo, tena wakati bado nikiwa mdogo kulikua na matunda Fulani hivi tuliyaita mapumbu ya paka. Na yenyewe tulikua tunaamini ni chakula cha nyoka kwaiyo ukiyaona mate kwenye tunda hilo ujue nyoka yupo karibu.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom