Je, Mamlaka ya Rais yanatoka kwa Wananchi au Vyombo vya Dola?

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,299
3,055
Salaam wana Jukwaa,

Niende kwenye mada moja kwa moja.

1) Je, Mamlaka ya Rais yanatoka kwa nani hasa? Wananchi wa JMT au kwa vyombo vya dola?

2) Je, Nchi inapaswa kuongozwa na Ilani (ya chama chochote cha siasa) au Katiba ya JMT? (Kwa nini?)

3) Katika hali ya jumla (practically) je Rais anawajibika kwa nani hasa? Kwa Dola au Wananchi? Au kwa Chama chake? (Kwanini?).

Baada ya maswali hayo hapa juu kupata majibu sahihi, nina maswali madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

a) (Pamoja na madhaifu na mapungufu yaliyo kwenye Katiba yetu ya sasa toleo la 1977) Je Huu sio wakati wa Busara na Hekima kutumika/kuhitajika kuliko wakati wowote kwa viongozi wa Awamu ya Tano?

b) Je, Mh. Rais (na Serikali kwa ujumla) hawaoni wanajitenga na Wananchi (alienation)? [ bila kujali itikadi za kisiasa, kijamii au kiimani?]

c) Kwa vile hali ya uchumi wetu kwa sasa ni mkwamo (stagnate economy) Je Serikali ina mpango gani wa muda mfupi kuuamsha (stimulate) uchumi wetu? Uhalifu huongezeka ktk hali/mazingira kama hayo mfano utapeli, fedha bandia, vibaka mitaani hata asubuhi na mchana nk

d) Nini ipi hasa mipaka ya Ilani za chama/vyama na Katiba (pamoja na sheria za nchi)? Je! Ikiwa kuna mtanzuko (contrasts) je mwongozo sahihi ni upi?

Naomba tuchangie bila jazba, matusi, vijembe. Karibuni
 
Je, mamlaka ya yohana mbatizaji yalitoka kwa mungu au kwa wanadamu ,wanakuja kukujibu wako taifa saivi
 
c) Kwa vile hali ya uchumi wetu kwa sasa ni mkwamo (stagnate economy) Je Serikali ina mpango gani wa muda mfupi kuuamsha (stimulate) uchumi wetu? Uhalifu huongezeka ktk hali/mazingira kama hayo mfano utapeli, fedha bandia, vibaka mitaani hata asubuhi na mchana nk

Uchumi uliokuwepo haukuwa halisia.Ulikuwa uchumi uliokuwa ukiendeshwa na pesa zinazomwagwa mitaani na vibaka wa maofisini na wafanyabiashara vibaka waliokuwa wakimwaga pesa za kifisadi walizokwapua maofisini kwa njia za mbalimbali.Magufuli alichofanya ni kubana tu vibaka wa maofisini walio maofisi mbalimbali iwe serikalini,Tra,Bandari nk

Baada ya tumbua tumbua ndipo uchumi halisia utaanza kuibuka sio huo uchumi wa kuendeshwa na vibaka wa maofisini waliokuwa wakikwapua na kujenga,vibaa,grocery ,vihoteli nk na kuvitumia na vibaka wenzao wa maofisini na wafanyabiashara vibaka wanaoshirikiana nao kama wateja!

UHALIFU ULIOKUWEPO NI MKUBWA KULIKO WA VIBAKA WA PANYA ROAD ambao wapo siku zote wao wakikwapua ni labda simu ya laki auze shilingi elfu tano anywe kiroba.
 
Je mamlaka ya yohana mbatizaji yalitoka kwa mungu au kwa wanadamu ,wanakuja kukujibu wako taifa saivi

"Hatutajua chochote iwapo hatutahoji" Nukuu.

Asante kwa mchango, tuwasubiri waje watuambie.
 
Uchumi uliokuwepo haukuwa halisia.Ulikuwa uchumi uliokuwa ukiendeshwa na pesa zinazomwagwa mitaani na vibaka wa maofisini na wafanyabiashara vibaka waliokuwa wakimwaga pesa za kifisadi walizokwapua maofisini kwa njia za mbalimbali.Magufuli alichofanya ni kubana tu vibaka wa maofisini walio maofisi mbalimbali iwe serikalini,Tra,Bandari nk

Baada ya tumbua tumbua ndipo uchumi halisia utaanza kuibuka sio huo uchumi wa kuendeshwa na vibaka wa maofisini waliokuwa wakikwapua na kujenga,vibaa,gocery ,vihoteli nk na kuvitumia na vibaka wenzao wa maofisini na wafanyabiashara vibaka wanaoshirikiana nao kama wateja!

UHALIFU ULIOKUWEPO NI MKUBWA KULIKO WA VIBAKA WA PANYA ROAD ambao wapo siku zote wao wakikwapua ni labda simu ya laki auze shilingi elfu tano anywe kiroba.
Asante kwa majibu mazuri. Wakati wa majumuisho nitazingatia majibu yako haya.

Vipi kuhusu swali Namba 1-3 rafiki, tunaweza kusaidiana kupata majibu?
 
[QUOTE="YEHODAYA,
Baada ya tumbua tumbua ndipo uchumi halisia utaanza kuibuka sio huo uchumi wa kuendeshwa na vibaka wa maofisini waliokuwa wakikwapua na kujenga,vibaa,gocery ,vihoteli nk na kuvitumia na vibaka wenzao wa maofisini na wafanyabiashara vibaka wanaoshirikiana nao kama wateja![/QUOTE]

Ndugu Yehodaya, unaweza kutoa makisio ya muda ya ni lini hasa huo uchumi mpya tutaanza kuuona? Just a probable time-frame of sort.
 
Majibu unayo yooote katika kila swali lako,kipengele cha kwanza kabla ya au.kasoro swali la tatu tuu.
 
Uchumi uliokuwepo haukuwa halisia.Ulikuwa uchumi uliokuwa ukiendeshwa na pesa zinazomwagwa mitaani na vibaka wa maofisini na wafanyabiashara vibaka waliokuwa wakimwaga pesa za kifisadi walizokwapua maofisini kwa njia za mbalimbali.Magufuli alichofanya ni kubana tu vibaka wa maofisini walio maofisi mbalimbali iwe serikalini,Tra,Bandari nk

Baada ya tumbua tumbua ndipo uchumi halisia utaanza kuibuka sio huo uchumi wa kuendeshwa na vibaka wa maofisini waliokuwa wakikwapua na kujenga,vibaa,gocery ,vihoteli nk na kuvitumia na vibaka wenzao wa maofisini na wafanyabiashara vibaka wanaoshirikiana nao kama wateja!

UHALIFU ULIOKUWEPO NI MKUBWA KULIKO WA VIBAKA WA PANYA ROAD ambao wapo siku zote wao wakikwapua ni labda simu ya laki auze shilingi elfu tano anywe kiroba.
Duh! Kama ulibahatika kwenda shule utakuwa ulipata A+ ya uchumi! unatisha........
 
Je mamlaka ya yohana mbatizaji yalitoka kwa mungu au kwa wanadamu ,wanakuja kukujibu wako taifa saivi
Walioulizwa na Yesu swali hilo walijikuta wametegwa, wakamwambia hatujui na Yesu akawaambia na mimi siwaambii ni kwa mamlaka gani natenda haya.
Mimi kwa kujibu tu kuhusu mamlaka ya raisi kwa nchi yoyote ya kidemokrasia yanatoka kwa wananchi, hivyo raisi anachaguliwa na wananchi na anawajibika kwao. Yaani wananchi waweza kumwajibisha rais
 
Asante Ndigwa kwa majibu yako mazuri.
Sasa basi kwa vile mamlaka yake yanatoka kwa wananchi (katika nchi yoyote), na pia anawajibika kwao; Je unaweza kuainisha ni kwa namna anavyowajibika na/au kuwajibishwa kwa/na wananchi?
 
Asante kwa majibu mazuri. Wakati wa majumuisho nitazingatia majibu yako haya.

Vipi kuhusu swali Namba 1-3 rafiki, tunaweza kusaidiana kupata majibu?

1) Je Mamlaka ya Rais yanatoka kwa nani hasa? Wananchi wa JMT au kwa vyombo vya dola?

YANATOKA KWA WANANCHI KUPITIA SANDUKU LA KURA.Magufuli alishapata kura za kumpa hayo mamlaka na kayapata kisheria na kikatiba

2) Je! Nchi inapaswa kuongozwa na Ilani (ya chama chochote cha siasa) au Katiba ya JMT? (Kwa nini?)

Nchi inaongozwa na vyote viwili ilani na katiba.

Katiba haionyeshi viwanda vitajengwaje,maendeeleo yatakujaje hiyo inaonyeshwa kwenye ilani ya CHAMA kilichopewa ridhaa ya kuongoza na wananchi kwa kipindi husika .Ni wapi katiba inasema mwaka huu elimu itakuwa bure!! Hakuna hayo yanapatikana kwenye ilani ya chama

3) Katika hali ya jumla (practically) je Rais anawajibika kwa nani hasa? Kwa Dola au Wananchi? Au kwa Chama chake? (Kwanini?).

Raisi anawajibikla kwa wote kwa dola na wananchi.Sababu yeye ni kiongozi mkuu wa dola na wananchi
 
Uchumi uliokuwepo haukuwa halisia.Ulikuwa uchumi uliokuwa ukiendeshwa na pesa zinazomwagwa mitaani na vibaka wa maofisini na wafanyabiashara vibaka waliokuwa wakimwaga pesa za kifisadi walizokwapua maofisini kwa njia za mbalimbali.Magufuli alichofanya ni kubana tu vibaka wa maofisini walio maofisi mbalimbali iwe serikalini,Tra,Bandari nk

Baada ya tumbua tumbua ndipo uchumi halisia utaanza kuibuka sio huo uchumi wa kuendeshwa na vibaka wa maofisini waliokuwa wakikwapua na kujenga,vibaa,grocery ,vihoteli nk na kuvitumia na vibaka wenzao wa maofisini na wafanyabiashara vibaka wanaoshirikiana nao kama wateja!

UHALIFU ULIOKUWEPO NI MKUBWA KULIKO WA VIBAKA WA PANYA ROAD ambao wapo siku zote wao wakikwapua ni labda simu ya laki auze shilingi elfu tano anywe kiroba.
ndugu yangu mi naona watu kama wewe ndo tatizo la taifa, mlishinda humu mkitetea selekali hiyo iliyo jenga uchumi wa vibaka, vibaka wakaiba bila kuguswa mkiimba mapambio!, amekuja mwengine katumbua tumbua vibaka kinyume na aliye pita mapambio yakapambamoto zaidi. Naye ataondoka muda ukufika, akija mwengine akafanya kinyume na huyu mapambio yataendelea tuuuuu...............kuusaidia uongozi si kuupamba tu, uongozi wa sasa umefanya mengi ndani muda mfupi ambayo binafsi nayakubali lakini pia kuna makosa!! ambayo hampendi kuyakubali......
 
Ninaweza asante kwa mchango. Hilo ni tatizo kubwa, kwa sababu kila awamu itakuwa na "excuses" zake. Hivyo inatulazimu tujiulize maswali magumu ili tupate majibu sahihi ya kutukwamua hapa tulipokwama kwa miaka zaidi 50 sasa.
 
Back
Top Bottom