Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,056
Salaam wana Jukwaa,
Niende kwenye mada moja kwa moja.
1) Je, Mamlaka ya Rais yanatoka kwa nani hasa? Wananchi wa JMT au kwa vyombo vya dola?
2) Je, Nchi inapaswa kuongozwa na Ilani (ya chama chochote cha siasa) au Katiba ya JMT? (Kwa nini?)
3) Katika hali ya jumla (practically) je Rais anawajibika kwa nani hasa? Kwa Dola au Wananchi? Au kwa Chama chake? (Kwanini?).
Baada ya maswali hayo hapa juu kupata majibu sahihi, nina maswali madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
a) (Pamoja na madhaifu na mapungufu yaliyo kwenye Katiba yetu ya sasa toleo la 1977) Je Huu sio wakati wa Busara na Hekima kutumika/kuhitajika kuliko wakati wowote kwa viongozi wa Awamu ya Tano?
b) Je, Mh. Rais (na Serikali kwa ujumla) hawaoni wanajitenga na Wananchi (alienation)? [ bila kujali itikadi za kisiasa, kijamii au kiimani?]
c) Kwa vile hali ya uchumi wetu kwa sasa ni mkwamo (stagnate economy) Je Serikali ina mpango gani wa muda mfupi kuuamsha (stimulate) uchumi wetu? Uhalifu huongezeka ktk hali/mazingira kama hayo mfano utapeli, fedha bandia, vibaka mitaani hata asubuhi na mchana nk
d) Nini ipi hasa mipaka ya Ilani za chama/vyama na Katiba (pamoja na sheria za nchi)? Je! Ikiwa kuna mtanzuko (contrasts) je mwongozo sahihi ni upi?
Naomba tuchangie bila jazba, matusi, vijembe. Karibuni