NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,458
- 17,282
Nawasalimia ndugu zangu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Moja kati ya salamu bora kabisa ya nyakati zetu.
Mama tangu ashike madaraka amekuja na surprise nyingi sana mojawapo ni uteuzi wa Makamu wa Rais ndugu Philip Mpango,tulitarajia uteuzi wa mtu mkongwe kwenye chama tena mwenye sauti ndani na nje ya chama lakini mama kamteua Mpango ambae hana mizizi ndani ya chama tena hana mtandao. Kwa jicho la tatu Mama kaogopa kumezwa na wanamtandao wa chama Tz Bara, ili awe na sauti ndani na nje ya chama kama kiongozi wa nchi.
Katika moja ya hotuba zake Mama alikosea kwa kusema Bunge la Katiba badala ya Bunge la Bajeti. Kwa mtazamo wa kawaida mama hakukosea kabisa bali amefikisha ujumbe anafikiria Katiba Mpya tena ya Serikali tatu ili kuipa mamlaka kamili Zanzibar.
Ikumbukwe vigogo wa CCM wameondolewa na mwendazake pale Bungeni hivyo basi itamsaidia mama kuleta mjadala wa Katiba Mpya tena rasimu ya Warioba ndani Bunge ambayo itapitishwa na kundi la wabunge wengi wachanga wa CCM wasio na mizizi na sioni kikwazo kwa Mama kwenye hili kwani kina Chenge, Sitta na vigogo wengi wa CCM hawamo Bungeni.
Naiona rasimu ya Warioba ikiwa Katiba Mpya na Mamlaka kamili ya Serikali ya Zanzibar.
Je, kama Zanzibar ikipewa mamlaka kamili itakubali kuburuzwa na Tanganyika?
Je, itakubali Majeshi ya Bara kuikalia Zanzibar tangu mapinduzi hadi leo?
Zama hizi hazina Maalim Seif wa kumfitini mama wala hakuna Baba wa taifa wa kumuweka mama kizuizini.
Nadhani kilio cha muda mrefu cha mamlaka kamili kitajibiwa na Mama yetu na adhma ya siri ya kifua cha Aboad Jumbe cha kuifanya Zanzibar kama Serikali yenye mamlaka kamili itatekelezwa katika awamu ya sita ya Mama yetu.